Statistics
JF-Expert Member
- Sep 22, 2013
- 3,666
- 7,788
Ongezea sukari wewe
Hahaha nmekaa Sana kule Kama 14 yrs maeneo tofauti. Vijijini tulienda na gari masikini watoto wanakimbia huku wanalia sijui wanawaza mnyama gani huyu mkubwa hivi😄😄, yaani hata pasi ya umeme wanauliza "na haka Ni ka Nini? Hahah!
Kiboko Ni pale tumetoka mwanza mjini kuelekea kwimba barabara ya vumbi sio kijijini kivile Sasa tupo kwenye haisi njiani tunaona abiria wawili walikuwa wadada wanasimamisha gari, konda kafungua mlango hahah! Wakwanza akavua viatu akaingia amevishika mkononi, wapili na yeye anamwangalia wa kwanza kafanyaje hahah! Na yeye pia akavua viatu akashika mkononi Sasa gari ikaondoka watu wote kwenye gari tukaanza kucheka vibaya mno, konda akawaambia hebu vaeni viatu vyenu, wakavaa nakumbuka dreva wa gari aliendesha anacheka hadi tunafika kwimba🤣🤣🤣🤣