Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Duuu! Sasa tutafanyaje mbona Mie nipo Ulaya Saizi. Ila connection na wadau kibao bongo, wameniaidi Kuwa siku nikirudi tu,watanipa Dili ya maama.
Masuala kama connections kwa shughuli za maana zenye kuleta tija kwa jamii na taifa hayana shida.

Dili likiwa kwenye mstari mmoja na connections kama nilivyosema hapo juu pia hakuna shida ila ikiingiza masuala kama dili za akina Seth basi hayo ni maisha ya kubahatisha.
 

usinichekeshe,kuna mmoja alirudi bongo na bsc in motorsport engineering.

nilipomuuliza degree yake inahusu nini, akaniambia ni uhandisi wa magari ya michezo kama yale yanayotumika kwenye formula one.

sasa issue ikawa kwenye kutafuta kazi, alisota sana.

ashukuru Mungu familia yake kidogo ilikuwa inajiweza, wakampa mtaji afungue gereji. kwa sasa ana miliki gereji yake na car wash maeneo ya kirumba, mwanza.
 
KABISA KABISA WENYE MALENGO NA NIDHAMU WANA TUSUA SEMA KWA JASHO SANA SANA SIYO LELEMA , UJANJA , WIZI NA RUSHWA KAMA BONGO,
ILA KATIKA KUMI NI WAWILI TU!!!!!!!!!!!!!!!
Katika 10 wawili...kunahitajika nguvu za ziada
 
Vijana wa Kitanzania na Afrika kwa ujumla waanze kula samaki khasa yule Goldfish.

Huyu samaki ana madini muhimu sana kuimarisha ufanisi wa ubongo wa binadamu.
 
Aisee tuko tofauti Sana,Kama Mambo yenyewe ndio hivyo nimekubali kweli Sina mapenzi ya dhati, siwezi kaa na mwanaume asiye na malengo Wala mwelekeo kisa penzi la dhati Hapana, NO!..Mimi binafsi naumiza kichwa mchana na usiku nalala masaa machache ili nitoboe maisha eti nikae nampenda mtoto wa mtu asiyeshughulisha kichwa chake...Hapana dada...Imani yangu yenyewe ya kiroho inamtaka mwanaume atafute kwa jasho mimi ni nani sasa nikae namvumilia mwanaume asiyetafuta.....we endelea na wapambanaji wanaozunguka duniani na kurudi na cheni na laptop ukiwaita mashujaa.
 
Yupo jamaa yetu mmoja aliishi UK miaka 10 bila kurudi home.
Siku amerudi kwao Choo cha nyumba ya uswahilini.
Haingii bila kupuliza air freshener kopo zima.
,na haogi maji ya bomba anasema mavumbi.
Ananunuwa chupa kubwa la litres 15.

Kibunda cha noti kilipokwisha mbwembwe zote ziliyeyuka.[emoji3][emoji3][emoji3].
Watu wa Ng",ambo,,vituko vitupu.
 
🤣🤣🤣🤣Ila Bora hata alirudi na ujuzi
 
Unaona Mambo yao ya ajabu hayo!kilichomfanya asijenge akiwa huko nje Ni nini?wakiambiwa ukweli Ni wakali kwelikweli
 
Hao ndo wenye nidhamu na kujielewa...wengi wao ulimbukeni tu
 
Wewe ni global citizen...Hali yako kwa Sasa niaje lakini?
 
Kuna mwamba mmoja alitoka bongo 2000 hadi leo hajarudi haijulikani kama mzima au kafa

Mama na dada yake walishakufa kitambo sana yeye hata simu hapigi duuuh sijui kama mzima au alishakufa kitambo
Ukute Hana hata hela ya voucher🤔🤔🤔
 
Kiranga mbona Kama umeamka na hasira?relax mkuu.hayo maneno ya umbeya wanatupa wenzenu wanaorudi na kutupiga virungu sisi na kutumia vizungu vigumuuu ili tuwaamini 🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…