Hivi kuna wanaofanyabiashara ya Umachinga wenye Degree pale Mbezi Mwisho?

Hivi kuna wanaofanyabiashara ya Umachinga wenye Degree pale Mbezi Mwisho?

Mohamedex121

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2022
Posts
1,725
Reaction score
3,271
Lengo la swali langu hili ni kupata company kutoka kwa hawa wamachinga wa mbezi maana nami ninampango wa kufungua meza yangu ya biashara hapo mbezi mwisho. Nilishapata eneo na nimeongea na mmiliki na amenipa hadi details za ushuru ili niweze kufanya biashara yangu mpya kama mmchinga.

Ok anyway mnajuwa kabisa kuna ile hali ambayo waswahili wanasema kuona aibu. Yes kabla ya kufikilia hili wazo langu nimekuwa muoga na mtu wa aibu hasa nikitaka kujaribu biashara ya umachinga. Huwa nafikiria sana nikiwepo pale mbezi na meza yangu ya biashara halafu ukicheki pale kuna mkusanyiko mkubwa wa watu, baadhi ya watu wanaonifahamu ni rahisi kukutana nao pale mbezi, sasa hofu yangu ni kwamba nitawaambia nini pindi wakiniona nimekuwa mmchinga na hii degree yangu??

Ila hili wazo nimepotezea kutokana na hali yangu ya kiuchumi na biashara yangu ya mara ya kwanza kukumbana na changamoto za kukosa wateja, maana hapa nilipo hakuna mkusanyiko mkubwa wa watu ukilinganisha na mbezi.

Hivo nimekuja mbele yenu mnipe courage (ujasiri) namna ya kuhimili hili wazo langu la biashara ya umachinga ukiachilia mbali degree niliokuwa nayo ili nisione aibu na nisijihisi niko pekee yangu tunaopitia hii hali ngumu ya kiuchumi hasa wale degree holder ambao tumeamua au wameshaanza kufanya biashara ya umachinga

#Natanguliza_shukurani_wakuu
Screenshot_20230721_192246.jpg
 
Mimi namfahamu mmoja driver wa Bajaj anaendesha hiyo barabara ya Morogoro rout za Mwenge na Manzese.

Siku ya kwanza kuzungumza nae alisema anajutia muda aliopoteza kuta nne kwani alipomaliza alikaa mtaani miaka sita huku hana ramani yoyote tofauti na matarajio yake.
 
Kabla hata sijamaliza kusoma thread yako nakushauri maisha hayana degree iyo kofia ya degree uliyovaa ivue piga kazi hujangundua kuwa wasio na degree ndio wanamiliki maisha bila stress ,wewe na uliemaliza nae std 7 akachakarika na mishe badala ya elimu amekuzidi parefu sana
 
Mkuu degree hailiwi, degree hailipi bill yoyote, degree haitakupa pesa ya matibabu na mahitaji yako yote. Amka...jitose fanya shughuli halali kwa weledi mkubwa.

Mungu ni mwaminifu atakupa fungu lako. Huwezi jua unaweza kukutana na mtu akakupa mchongo wa kazi ya hiyo degree yako...Mungu ni Mungu
 
Mkuu degree hailiwi, degree hailipi bill yoyote, degree haitakupa pesa ya matibabu na mahitaji yako yote. Amka...jitose fanya shughuli halali kwa weledi mkubwa. Mungu ni mwaminifu atakupa fungu lako. Huwezi jua unaweza kukutana na mtu akakupa mchongo wa kazi ya hiyo degree yako...Mungu ni Mungu
Sawa mkuu nashukuru sana kwa kunitia moyo
 
Kabla hata sijamaliza kusoma thread yako nakushauri maisha hayana degree iyo kofia ya degree uliyovaa ivue piga kazi hujangundua kuwa wasio na degree ndio wanamiliki maisha bila stress ,wewe na uliemaliza nae std 7 akachakarika na mishe badala ya elimu amekuzidi parefu sana
Nashukuru kwa maoni ya ujasiri kama haya nitayafanyia kazi
 
Lengo la swali langu hili ni kupata company kutoka kwa hawa wamachinga wa mbezi maana nami ninampango wa kufungua meza yangu ya biashara hapo mbezi mwisho...
Utoto unakusumbua mm nafanya kazi zote nabeba zege ...Nalima bustani...Nabeba maji kwenye madumu. Nasaidia fundi...Kibarua chochote halali nafanya. Hapa nilipo nina degree ya upper second class with honour.

Nilipata 2 ya 10 pcb form six ifunda tech. Nilipata division one form four ...Na kama iyo haitosh nilipata a hesabu form four..Ety unaona aibu ivi ni hadithi unaleta au uhalisia ..Nb...Na miaka mi4 ...Mtaani toka nimalize udsm
 
Lengo la swali langu hili ni kupata company kutoka kwa hawa wamachinga wa mbezi maana nami ninampango wa kufungua meza yangu ya biashara hapo mbezi mwisho...
kafanye kazii watu wana degree za medicine wanafanya umachinga wewe unaogopa nini

kama vipi nipe hio meza nikapige kazii japo nina bachelor , bachelor haina maana kama huna hela*
 
Back
Top Bottom