Hivi kuna Wilaya inaipiku Liwale kutotembelewa na Viongozi wa Kitaifa?

Hatimaye yametimia yale niliyokua nayawaza na kuwazua.

Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale asimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha za ujenzi wa Hospitali

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Bw.Omary Chingwile ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Liwale na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo.

"Hatuwezi kufanya mchezo na fedha ya Serikali, tunahitaji kila mradi uende vizuri, fedha iliyoletwa lazima itumike kama ilivyokusudiwa".

Mhe.Majaliwa amesema Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza matumizi mazuri ya fedha za umma ili zikamilishe miradi ya maendeleo ya wananchi na kwamba Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote anayetumia vibaya fedha za umma.

Waziri Mkuu amemsimamisha kazi mtumishi huyo wakati akizungumza na madiwani, watumishi na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Lindi.

ITV
 
Ipo mkoa gani hyo wilaya
Duh...sijui Kama unauliza kwa kejeli au ndio jiografia ya nchi yetu ipo kando kwa upande wako...Liwale ni wilaya mojawapo ya mkoa wa Lindi wenye wilaya zifuatazo...Lindi, Ruangwa, Nachingwea na Liwale...
 
Hiyo wilaya naifahamu fika..! Na nilichokiandika ni kweli isiyo na chembe ya shaka. Huu ni uzi wa muda kidogo.., nimefurahishwa kuina leo hii Mhe. KMM (PM) amefanya ziara huko na kukuta baadhi ya mambo yanavyofanywa kiholela. Kama nilivyokua nimewaza kwamba wilaya zisizotembelewa na viongozi wa juu wa kitaifa kwa muda mrefu kuna sababisha baadhi ya watendaji kubweteka na kufanya kazi kwa mazoea (business as usual)
 
Asante Sana Ndugu....Binafsi mikoa ya Lindi na Mtwara naifahamu kwa kiwango kikubwa ingawa sitoki huko...Historian ya nchi yetu kuanzia ukoloni na awamu za uongozi zote ndiyo iliyofanya mikoa hii na hasa maeneo yake kutopewa kipaumbele katika maendeleo....ni mikoa ambayo ilikuwa Kama imetengwa ingawa in raslimali nyingi Kama virgin land, madini, gesi na kadhalika...barabara mbovu na miundombinu mingine ndiyo iliyosababisha mikoa hii kuonekana imefungwa....upo wakati kabla ya kuwekwa lami kwa barabara ya Lindi Dar watu walikywa wanayumia hadi siku nne kutoka Lindi kuja Dar ..wilaya ya Liwale ndiyo imetengwa zaidi kutoka Nachingwea hadi Liwale barabara ni mbovu kabisa na sijui Kama siku hizi wameweka lami...halafu Liwale ni mji wa kihistoria na Kuna boma la wajerumani pale na Mambo mengine ya kihistoria ya wangindo na Vita vya majimaji...hata kutoka Nachingwea kwenda Masasi (wilaya katika mkoa wa Mtwara) ingawa ni chini ya kilomita 100 sudhani Kama Kuna lami pale...inasikitisha Sana kwa kweli....ingawa kwa kiwango kikubwa watu wenyewe wa mikoa hii inabidi pia walaumiwe kwa kutochangamka kimaendeleo kwa kushindwa ku-invest kwao na hata kushindwa kujenga nyumba kwao
 
Ni matumaini yangu mu wazima..!?

Hizi wilaya zetu pamoja na changamoto za miundombinu ya barabara kuna ulazima wa viongozi wa kitaifa kufanya ziara ikiwezekana mara baada ya mara. Lakini hali ikiwa hivi kama ilivyo huko wilayani Liwale inaleta shida katika utendaji wa baadhi ya watumishi wa ngazi za juu katika halmashauri. Hufanya kazi kiholela kwa kujua viongozi hawawezi fika huko...!

Jambo hili ni huko Liwale tu au kuna wilaya zingine zina changamoto hii??
Umewahi kusikia sehemu inaitwa Manda? Ipo ludewa unavuka ziwa huko hata gari kuiona ni bahati. Yani ni rahisi kuona ndege angani Ila gari no ngumu sana😃😃
 
Umewahi kusikia sehemu inaitwa Manda? Ipo ludewa unavuka ziwa huko hata gari kuiona ni bahati. Yani ni rahisi kuona ndege angani Ila gari no ngumu sana[emoji2][emoji2]
Km hiyo ni kata kuna kata nyingi sana zenye changamoto ya aina hiyo tena angalau huko wanaziona ndege
 
Asante Sana Ndugu....Binafsi mikoa ya Lindi na Mtwara naifahamu kwa kiwango kikubwa ingawa sitoki huko...Historian ya nchi yetu kuanzia ukoloni na awamu za uongozi zote ndiyo iliyofanya mikoa hii na hasa maeneo yake kutopewa kipaumbele katika maendeleo....ni mikoa ambayo ilikuwa Kama imetengwa ingawa in raslimali nyingi Kama virgin land, madini, gesi na kadhalika...barabara mbovu na miundombinu mingine ndiyo iliyosababisha mikoa hii kuonekana imefungwa....upo wakati kabla ya kuwekwa lami kwa barabara ya Lindi Dar watu walikywa wanayumia hadi siku nne kutoka Lindi kuja Dar ..wilaya ya Liwale ndiyo imetengwa zaidi kutoka Nachingwea hadi Liwale barabara ni mbovu kabisa na sijui Kama siku hizi wameweka lami...halafu Liwale ni mji wa kihistoria na Kuna boma la wajerumani pale na Mambo mengine ya kihistoria ya wangindo na Vita vya majimaji...hata kutoka Nachingwea kwenda Masasi (wilaya katika mkoa wa Mtwara) ingawa ni chini ya kilomita 100 sudhani Kama Kuna lami pale...inasikitisha Sana kwa kweli....ingawa kwa kiwango kikubwa watu wenyewe wa mikoa hii inabidi pia walaumiwe kwa kutochangamka kimaendeleo kwa kushindwa ku-invest kwao na hata kushindwa kujenga nyumba kwao
Hii route haina lami mpaka kesho

Mtwara, Nanyamba, Tandahimba, Newala, Masasi, Nachingwea, Liwale.

Hata ile lami ya Mtwara-Masasi ni mwamba mmoja alipinduka sarakasi akafanya figisu ikajengwa. Sijui ndio huyo Sijaona Nangwanda!!!???
 
Ni matumaini yangu mu wazima..!?

Hizi wilaya zetu pamoja na changamoto za miundombinu ya barabara kuna ulazima wa viongozi wa kitaifa kufanya ziara ikiwezekana mara baada ya mara. Lakini hali ikiwa hivi kama ilivyo huko wilayani Liwale inaleta shida katika utendaji wa baadhi ya watumishi wa ngazi za juu katika halmashauri. Hufanya kazi kiholela kwa kujua viongozi hawawezi fika huko...!

Jambo hili ni huko Liwale tu au kuna wilaya zingine zina changamoto hii??
Nahisi SI hiyo TU Mpwapwa je!?
 
Hii route haina lami mpaka kesho

Mtwara, Nanyamba, Tandahimba, Newala, Masasi, Nachingwea, Liwale.

Hata ile lami ya Mtwara-Masasi ni mwamba mmoja alipinduka sarakasi akafanya figisu ikajengwa. Sijui ndio huyo Sijaona Nangwanda!!!???
Mimi sijui serikali huwa inafikiria Nini ...hata ile barabara ya Nachingwea Hadi maeneo ya mtama sijui Kama Kuna lami pale..hovyo kabisa...
 
Umewahi kusikia sehemu inaitwa Manda? Ipo ludewa unavuka ziwa huko hata gari kuiona ni bahati. Yani ni rahisi kuona ndege angani Ila gari no ngumu sana[emoji2][emoji2]
Hiyo ni fix.
Manda ni kamji kabisa Sasa magari hayaonekani kivip? Na kuna ruti za ludewa town hadi Manda Kwa siku Mara tatu.
Acha uongo bwana mdogo.
 
Mimi sijui serikali huwa inafikiria Nini ...hata ile barabara ya Nachingwea Hadi maeneo ya mtama sijui Kama Kuna lami pale..hovyo kabisa...
Pale hamna barabara ya Nach-Mtama bali ipo Nach-Ndanda na Nach-Nanganga, ipo pia Nanganga-Rwangwa zote hizo ni vumbi
 
Ni matumaini yangu mu wazima..!?

Hizi wilaya zetu pamoja na changamoto za miundombinu ya barabara kuna ulazima wa viongozi wa kitaifa kufanya ziara ikiwezekana mara baada ya mara. Lakini hali ikiwa hivi kama ilivyo huko wilayani Liwale inaleta shida katika utendaji wa baadhi ya watumishi wa ngazi za juu katika halmashauri. Hufanya kazi kiholela kwa kujua viongozi hawawezi fika huko...!

Jambo hili ni huko Liwale tu au kuna wilaya zingine zina changamoto hii??
Tatizo la Liwale ni uchawi ndiyo unaowasumbua kule. Mtu kama haswali swala 5 kwa siku basi ni mchawi, nani anataka kwenda sehemu kama hii?
 
Back
Top Bottom