Hivi kuna wimbo mzuri wa mapenzi na mahusiano wa Kiswahili mzuri na wenye ujumbe konki kuliko huu?

Hivi kuna wimbo mzuri wa mapenzi na mahusiano wa Kiswahili mzuri na wenye ujumbe konki kuliko huu?

Long time aisee
Memories kipindi hicho tunasikiliza sedioDaah old is gold
Mkuu hii ni English ,za kiingereza mbona zipo kibao.
Issue ni hizi za lugha yetu pendwa ambapo ikipigwa ukumbini kila mmoja lazima moyo utetemeke.
Mkuu kipindi hicho wema sepetu ni miss Tanzania 2006 ndiyo tulikuwa tunaskiliza nyimbo kama hizi za emanuel nkulila sijui huyu mtu hata yupo wapi sasa hivi
 
MB Dogg - Latifah
MB Dogg - Ina Maana
MB Dogg - Si Uliniambia
FA + Linah - Yalait Remix
Tabora Jazz - Rangi ya Chungwa
Les Wanyika - Kasuku
 
Kuna ule wimbo wa the kilimanjaro band "mpenzi wangu naomba nikueleze pendo langu lililo moyoni mmh moyoni mwangu, mapenzi niii kuheshimiana nami mpenzi nimekuheshimuuu"🎵🎼




Anyway nimeachwa sitaki tena maswaliiii, naenda beach kula upepo wa bahari, naumwagilia moyo mziki kwa mbaliiii, jimbo lipo wazi sema nitakubali....unantaka basi ntongozeeee🎵🎼🎼🎼🎼
Hivi unajuwa hao ni wana ndoa halisi?

Wote wapo The Kilimanjaro band.
 
Wimbo wa Bob Rudala alicopy sana wimbo wa I believe in you wa Joe Thomas.
 
kuna ile "kund'uchi juu anifikishe kwetu, kwetu kwetu" kaimba Asake, nayo naskia inafanya bomba sana kwenye harusi.
 
Jina la wimbo lipo sahihi?

Ndiyo.

SNFNW.jpg
 
Back
Top Bottom