TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
Hello wakuu.
Nina mpango wa kumvisha pete mtarajiwa wangu. Swali langu ni je, lazima kualika watu au naweza kumuita ghetto tu nikamvalisha na mchezo ukaisha?
Watanzania tume kompliketi sana swala zima la ndoa. Kiasi kwamba kwa sasa mtu ukitaka kuoa yaani lazima ujipange utadhani unaenda India kufanyiwa upasuaji. Kila hatua ya mchakato ni sherehe!
- kwenda kujitambulisha - sherehe
- kujitambulisha ukweni - sherehe
- kupeleka barua ya posa - sherehe
- kwenda kuchukua majibu ya barua - sherehe
- kupeleka mahari - sherehe
- kuvalishana pete - sherehe
- kuitisha kamati - sherehe
- send off - sherehe
- sijui nini tena - sherehe
- photoshoot - sherehe
- harusi - sherehe
- hanemun - sherehe
- kuvunja kamati - sherehe !