Nitakujibu kwa maandiko kuwa kuna watu kama viongozi wamepewa dhamana ya kuwapa watu baraka za Mungu ( sio mashoga)
NARUDIA...UFIRAJI NA USHOGA KIBIBLIA NI DHAMBI HIVYO PAPA WENU NI MPOTOSHAJI SOMA HAPA...
(Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
1 Wakorintho 6:9
na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;
1 Timotheo 1:10)
SASA TUANGALIE WANADAMU KUWABARIKI WENGINE
Labani akaondoka asubuhi na mapema, akawabusu wanawe na binti zake, akawabariki; kisha Labani akaenda zake, akarudi kwao.
Mwanzo 31:55
Kisha Haruni akainua mikono yake na kuielekeza kwa hao watu, akawabariki; kisha akashuka akisha isongeza sadaka ya dhambi, na sadaka ya kuteketezwa, na sadaka za amani.
Mambo ya Walawi 9:22
Basi Yoshua akawabarikia, na kuwapa ruhusa waende zao; nao wakaenda mahemani kwao.
Yoshua 22:6
Basi Musa alikuwa amewapa hiyo nusu moja ya kabila ya Manase urithi katika Bashani; lakini hiyo nusu ya pili Yoshua aliwapa urithi kati ya ndugu zao, ng'ambo ya Yordani upande wa kuelekea magharibi. Zaidi ya hayo Yoshua, hapo alipowapeleka waende zao mahemani kwao, akawabarikia,
Yoshua 22:7
Kisha Daudi alipokwisha kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani akawabarikia watu kwa jina la Bwana wa majeshi.
2 Samweli 6:18
Mfalme akageuza uso wake, akawabarikia mkutano wote wa Israeli; na mkutano wote wa Israeli wakasimama.
2 Mambo ya Nyakati 6:3
Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa.
Luka 2:34
NINA MAANDIKO MENGI YA EATU KUWABARIKI WATU, UNAHITAJI ZAIDI?