Hivi kwa umri wa miaka 41 niliofikisha naweza kutoboa maisha au ndio basi tena?

Mkuu unaweza kutufafanulia hiyo no.3?
 
3. Kusubiri kusudi la Mungu na hatma ya maisha yako.
Hapa kuna walakini.
Sina shida na imani zetu na wala sipingi ila kuna shida na tafsiri.
Ukimwambia mtu asubiri kusudi la Mungu wakati Mungu alimwambia adamu akawajibike na ale kwa jasho lake, sasa kusudi gani tena asubiri?

Halafu iweje Mungu awe na makusudi tofauti kati ya mzungu na mwafrika??
Tuchapeni kazi kwa bidii hapo ndipo Mungu ataweka kusudi lake.
 
Kusudi la Mungu ni kufanya Mapenzi na amri zake hila kuchoka.
Fanya kazi Kwa bidii bila kuangalia muda upo au umeisha.
Weka akiba hata Kwa kidogo upatacho.
Alafu hayo mengine muachie Mungu
Asante
 

Anaegawa rizki ni Mwenyezi Mungu peke yake, na sio binadamu. Muhimu fanya kazi kwa bidii/jitume/pambana mwanawane, Allah akujaalie ufanikiwe!!
 
Unaweza kufanya juhudi katika kazi na usifanikiwe pia
Sio kwamba hujafanikiwa, bali kusudi na mapenzi ya Mungu bado kwa wakati huo. Kwahiyo, usihesabie kuwa hautafanikiwa, ongeza bidii ya mapambano. Halafu tukumbuke kuwa kazi ni ibada, na hakuna ibada isiyo na faida kwakuwa Mungu wetu ni muadilifu.
 
Unaweza Mkuu
 
Inasikitisha kukata tamaa mapema hivyo!
 
Miaka 41 michache sana, ndani ya miaka 5 unaweza kufanya makubwa kama una nia.

Wife mfungulie biashara apambanie chakula, watoto peleka shule za kawaida halafu wewe tafuta mbishe yoyote, epuka kuishi maisha ya watu.

Kama una nyumba na pesa ya kula wewe ni tajiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…