Hivi kwa umri wa miaka 41 niliofikisha naweza kutoboa maisha au ndio basi tena?

Wana JF hivi kuna uwezekano wa kufanikiwa kiuchumi unapokuwa na umri wa kuanzia 41?

Mpaka sasa nina mke na watoto watatu. Sina shughuli rasmi, nabangaiza tu.

Naanza kuona Kama ndoto yangu ya kuwa na mafanikio kiuchumi inafifia.

Swali langu ni kwenu ninyi Wana JF. Hivi Kuna possibility ya kutoboa kwa umri huo? Au ndio nishazeeka Tena!
Dah...kwanza tukibaliane....kutoboa ni kuwa vipi? Maana wengine tunadhani tumetoboa tayari 🤣🤣🤣🤣
 
...Babu wa Kikombe Loliondo alituokota akiwa na Miaka Mingapi???
 
Wana JF hivi kuna uwezekano wa kufanikiwa kiuchumi unapokuwa na umri wa kuanzia 41?

Mpaka sasa nina mke na watoto watatu. Sina shughuli rasmi, nabangaiza tu.

Naanza kuona Kama ndoto yangu ya kuwa na mafanikio kiuchumi inafifia.

Swali langu ni kwenu ninyi Wana JF. Hivi Kuna possibility ya kutoboa kwa umri huo? Au ndio nishazeeka Tena!
Viwango vya Mafanikio vinatofautiana kutegemea historia za watu walikotoka.
Kuna wengine akiwa mwenyekiti wa mtaa tayari katoboa,inategemea unavyo define mafanikio
 
Mada kama hizi utakuta mfano wa mtu mmoja tu mzee wa KFC hawezi kukosekana......ila kiukweli mzee 41 yrs meli inazama inaelekea Nungwi.
Acha kumkatisha tamaa Jamaa yetu,kwa umri huo Bado ana muda wa kutosha.Ikiwa mzee Mwinyi mwenye miaka 95,sasa hivi bado anapanda Mikorosho,sasa utasemaje kwa mwenye 41?.
 
Wana JF hivi kuna uwezekano wa kufanikiwa kiuchumi unapokuwa na umri wa kuanzia 41?

Mpaka sasa nina mke na watoto watatu. Sina shughuli rasmi, nabangaiza tu.

Naanza kuona Kama ndoto yangu ya kuwa na mafanikio kiuchumi inafifia.

Swali langu ni kwenu ninyi Wana JF. Hivi Kuna possibility ya kutoboa kwa umri huo? Au ndio nishazeeka Tena!
Mchungaji Mwaisapile alitoboa akiwa na miaka 75
 
41 bado sana,pambana,mi babaangu mkubwa angekata tamaa,sijui angekua maskini kiasi gani,lakini kakomaa,alikua hana nyumba,kajenga nyumba ya kisasa,alikua hana usafiri,kanunua gari mbili,moja yake jingine mamkubwa analitumia.Yupo kwenye late 50's na bado anapambana.Usikate tamaa.Na nikwambie tu,alishagundulika kua ana UKIMWI,lakini hajawahi kukata tamaa.Just imagine,mtu yuko kwenye hiyo status ya afya,na anapambana haswa,je wewe?Komaa.
 
Jiulize Jo Biden ana umri Gani? ama huyu Mfalme mpya wa Uingereza ana umri gani? japo bado alikua anakaa kwao, maisha hayana fomula kutoboa ilimradi unaendelea kukomaa bila kukata tamaa Laizer mzee wa Tanzanite naye unamkumbuka? katoboa akiwa na umri gani , yani wabongo kwa kujikataa mapema hamjambo, komaa
 
Maisha yanachanganya Sana! Muda wa utafutaji ni mfupi sana- tunatumia muda mwingi Sana shule.

Miaka 41 ni mingi kiasi, umri huu kwenye mpira ni Kama kipindi Kwanza dk za nyongeza! ukipiga hesabu kwa mtu aliesoma mpaka chuo, ni takribani una miaka 15 katika utafutaji.

Miaka 15 ni michache sana, hasa ukitokea hizi familia zetu za Tozo! - na huna kipaji- hebu chukulia ulimaliza chuo ukiwa na 25, ukapata kazi baaada ya miaka miwili. Mshahara laki nane!

Utafute chumba, ununue kitanda , ununue TV, ulipe mkopo, ukarabati nyumba ya wazazi, ujirushe kidogo- ukishituka miaka 30.
Unaingia kwenye ndoa- Kisha familia , mtoto akifika la tatu tu, tayari una miaka 40.
Hapo bado hujajenga na kusomesha! na bado miaka 20 usitaafu!
Ukifika 55- hicho ni kipindi Cha pili, 60 ni dk za nyongeza,- 60+. ni penati

Alafu ni kamzunguko sasa- watoto wako nao wanakuja fata mtiririko huu huu!

Mwisho wanasema eti , inawezekana kufanikiwa kiuchumi ila Inahitaji muda, Afya njema, jitihada, mipango, na kumuomba Mungu akupe umri mrefu

Sijui kina Bakhresa walifanyaje! Maana jamaa tajiri kitambo!
 
Vipi gari je lipo? Au ndo ushakua mwana israeli? Mambo ya kutembea miaka 40+ kwa miguu...🤣🤣🤣🤣
Duh mkuu mbona wengi tu wana umri huo na zaidi wanatembea kwa miguu?
 
Maisha yanachanganya Sana! Muda wa utafutaji ni mfupi sana- tunatumia muda mwingi Sana shule.

Miaka 41 ni mingi kiasi, umri huu kwenye mpira ni Kama kipindi Kwanza dk za nyongeza! ukipiga hesabu kwa mtu aliesoma mpaka chuo, ni takribani una miaka 15 katika utafutaji.

Miaka 15 ni michache sana, hasa ukitokea hizi familia zetu za Tozo! - na huna kipaji- hebu chukulia ulimaliza chuo ukiwa na 25, ukapata kazi baaada ya miaka miwili. Mshahara laki nane!

Utafute chumba, ununue kitanda , ununue TV, ulipe mkopo, ukarabati nyumba ya wazazi, ujirushe kidogo- ukishituka miaka 30.
Unaingia kwenye ndoa- Kisha familia , mtoto akifika la tatu tu, tayari una miaka 40.
Hapo bado hujajenga na kusomesha! na bado miaka 20 usitaafu!
Ukifika 55- hicho ni kipindi Cha pili, 60 ni dk za nyongeza,- 60+. ni penati

Alafu ni kamzunguko sasa- watoto wako nao wanakuja fata mtiririko huu huu!

Mwisho wanasema eti , inawezekana kufanikiwa kiuchumi ila Inahitaji muda, Afya njema, jitihada, mipango, na kumuomba Mungu akupe umri mrefu

Sijui kina Bakhresa walifanyaje! Maana jamaa tajiri kitambo!
Watu wote duniani tuna masaa 24 kwa siku.
 
kitendo cha namna ulivyouliza tu hauwezi fanikiwa ata ukiwa na miaka 20 umeshakata tamaa tatizo sio umri.
 
Jiulize Jo Biden ana umri Gani? ama huyu Mfalme mpya wa Uingereza ana umri gani? japo bado alikua anakaa kwao, maisha hayana fomula kutoboa ilimradi unaendelea kukomaa bila kukata tamaa Laizer mzee wa Tanzanite naye unamkumbuka? katoboa akiwa na umri gani , yani wabongo kwa kujikataa mapema hamjambo, komaa
Labda umwambie Joe Biden wakati ana 41yrs alikuwa wapi na ana nini.
 
Back
Top Bottom