Hivi kwani Mungu anajibu maombi mabaya?

Hivi kwani Mungu anajibu maombi mabaya?

Wakuu habari za kuamka....

Mwenzenu najiskia vibaya sana sana sana yaani vibaya mnooo.. Natamani hata nisingekua nimeshika simu leo,. Kuna mtu kaweka status "Forever in our hearts" kampost mtu ambaye alifariki 2012 hadi nilishamsahau,. Nilikua mtoto lakini huyu mtu kila siku nilikua namuombea kwa Mungu afe,.

Ilikua hivi,. Nakumbuka Kabla ya likizo ya pasaka nlikua darasa la nne by then.. Tulikua tunafanya mitihani ya Joint shule nyingi nyingi na wale wanaokuwa topten mnaitwa mnapewa zawadi mnashangiliwa na kombe mnapewa kurudi nalo shuleni

Hiyo siku na mimi nilipass nikawa nominated kati ya ambao wataenda kuchukua zawadi,. Mda tunajiandaa tukaanza kujisafisha yaani kama kufuta viatu, kujiweka tu vizuri, nikatafuta lesso yangu nifutie viatu sikuiona.. Huyu binti ambae ni marehemu Alitoa lesso watu wote wakawa wamefutia viatu mimi nlikua wa mwisho ikafika zamu yangu huku najifuta nikaangalia vizuri nikaijua ni lesso yangu ambayo nlikua naitafuta, nikamwambia hii mbona lesso yangu nlikua naitafuta umeipata wapi? Si akakasirika akaninyang' anya nikamwambia basi nikupa iwe yako niachie tu nimalizie kufutia maana ndio nlikua nimeitwa niende mbele Akagoma .

Imagine nimeenda Mbele yatu wengi wanafunzi wa karibia shule 10 na walimu ,kiatu kimoja kisafi kingine kina Vumbi halafu yeye na rafiki zake walikua wananicheka 😭😭😭,. Ile siku hata sikuifurahia nilivyotoka tu nikapiga picha (na kiatu changu kimoja kina vumbi mwenyewe) nikarudi zangu nyumbani hata sikuongea na mtu...

To be honest tangu sikuile nilikua namchukia , mda wa kusali sala za jioni au asubuhi au kanisani nlikua namwambia Mungu kwanini watu wenye Roho mbaya unawaacha waishi,. Nlikua namwomba Mungu kila siku yule binti afe,. nilikua simpendi yaani kila siku nlikua namwambia Mungu huyu mtu asipokufa mimi nitaacha kusali maana ni anaroho mbaya kwanini asife tu?

Wakati tunakaribia kufunga shule December alianzaga kuumwa akawa na vidonda vidonda,nywele zake zilikua zinayonyoka Alikua anababuka midomo, Mara shuleni haji,. kwa wiki anaweza aje siku moja na akifika basi kuna mda anaanza kuumwa mara anatapika mzazi wake anakuja kumchukua, tulikua tunaambiwa Fulani anaumwa mkipata nafasi mkamwone me sikwenda hata siku moja, Kwanza nlikua nafurahi rohoni namwambia Mungu saizi ndio muda wake huu wa kufa, Wakati tupo darasa la tano alifariki nikawa najiskia amani kwanza hadi nilishamsahau... Tulikujaga tu kujua baadae kumbe alikua ni HIV POSITIVE tangu alivyozaliwa,.

Hapa nimekaa najiskia tu huzuni maybe hatakama alikua HIV positive pangine angeishi mda mrefu ila maombi yangu yalikuwa yanapigilia misumari mpaka akafa mwee!!,. Nimetoka kumwambia Mungu kama maombi yangu yalihusika anisamehe maana sikua najua nafanya nini kwa kipindi kile ni utoto tu😒🙏🙏

Ila sidhani kama maombi mabaya huwa yanaskilizwa🤔🤔
OOBE\BYPASSTHREADWQ:Acha kutumia ChatGPT, utaharibika kisaikolojia
 
Leejay49 ni mtoto mdogo anayejua kusali. Ndio kwanzaa sahii ana miaka 24
Miaka sio kipimo cha uzee, hilo ni suala la saikolojia ya mtu husika.
Kuna watu wana miaka 20 ila Wanahisi ni watu wazima tayari na wamefeli kimaisha au kufanikiwa kulingana na maono yao, jambo ambalo ukithink in deep ni true...
 
Maisha yana siri kubwa sana hasa unapotamka kitu kwa uchungu... Kuna jamaangu nilizozana nae kipindi fulani nilifilisika nikamuuzia friji akanizulumu chenchi kidogo tu kwenye ile hela aliyotakiwa kunipa, sasa kwa hali ngumu niliyokua nayo nikajikuta nimemtamkia maneno fulani kwa uchungu kitu ambacho naona kimetokea kama nilivyomwambia.

Friji niliuza ili niweze kumhudumia mke wangu aliyeenda kujifungua.
Yule jamaa nae alikuja kufilisika na kanasa kwenye mtego kama wangu hadi namkwepa asije kusema mimi mchawi
Nina wiki ya pili sasa naomba Mungu anilipie kisasi kwa mtu mmoja hivi asiyekuwa na shukrani,Alikuwa na hali mbaya sana kiuchumi nikamsaidia kidogo nilichokuwa nacho pamoja na ushauri,Sasa hivi kafanikiwa dharau nyingi ananiona sina hata hadhi ya kupiga naye stori,Wale ambao hawakuweza kumsaidia kipindi ana hali mbaya ndio rafiki zake wakubwa.
Sasa naomba Mungu amshushe arudi kwenye maisha yale yale,ili aje asaidiwe na hao anao waona wa maana.
 
Nina wiki ya pili sasa naomba Mungu anilipie kisasi kwa mtu mmoja hivi asiyekuwa na shukrani,Alikuwa na hali mbaya sana kiuchumi nikamsaidia kidogo nilichokuwa nacho pamoja na ushauri,Sasa hivi kafanikiwa dharau nyingi ananiona sina hata hadhi ya kupiga naye stori,Wale ambao hawakuweza kumsaidia kipindi ana hali mbaya ndio rafiki zake wakubwa.
Sasa naomba Mungu amshushe arudi kwenye maisha yale yale,ili aje asaidiwe na hao anao waona wa maana.
Jifunze kusamehe na kuachilia ili baraka zitiririke kwako pia
 
Jifunze kusamehe na kuachilia ili baraka zitiririke kwako pia
Ni kweli,ila kuna watu hawawezi kukuheshimu mpaka wakumbuke wema wako,na hawawezi kukumbuka mpaka warudi kwenye mazingira yaleee ambayo uliwafanyia wema, kuna watu wanakera
 
Haya tunasubiri wewe mwenye roho nzuri tukuone unaishi milele
 
Miaka sio kipimo cha uzee, hilo ni suala la saikolojia ya mtu husika.
Kuna watu wana miaka 20 ila Wanahisi ni watu wazima tayari na wamefeli kimaisha au kufanikiwa kulingana na maono yao, jambo ambalo ukithink in deep ni true...
Mkuu mbona unataka kuukataa ukweli?, miaka ni kipimo cha uzee/ukubwa wa mtu hili lipo wazi kabisa. Mtu mwenye miaka 20 hata afanye nini hawezi kuwa ameishi muda mrefu kuliko mwenye miaka 21 sasa hapo ni tofauti ya mwaka mmoja tu.

Ukiniambia uzee sio kipimo cha maarifa ya mtu nitakubaliana na wewe kwa kiasi tena na hapo inategemea unalinganisha watu wenye tofauti za umri kwa miaka mingapi.

Mtoto wa mwaka mmoja kamwe hawezi kumzidi maarifa kijana wa miaka 10.
 
Ndo mfumo uliokuwepo duniani taarifa mbaya zinasambaa haraka speed ya 5G ila taarifa njema mwendo wa kobe,so kabla hujataka kuongelea mabaya tafakari ilo hata huu uzi wako utatrend kutokana umezungumzia mabaya ila uzi wa fursa na habari njema wala.
 
Karibia unakuwa Rastafarian🫡

Hata mimea ni viumbe Mkuu, sasa tuwe tunakula nini😃
Dunia haina usawa, wewe unafurahia kula nyama huku mnyama amepoteza uhai akiwa akitegemewa na jamii yake
 
S

So mlimpa kazi?

2) mnamiliki kampuni halafu unashindwa kununuliwa hata sukari shuleni?
hujanielewa kabisa, nadhani ni changamoto yako ya uelewa. nimesema kipindi nasoma sekondari nilisoma na mtu wa aina hiyo, ila tulivyomaliza shule tukatawanyika kila mmoja akatafute maisha kumbe yeye aliishia pale form four, mimi nimesoma hadi ulaya, na alikuja kuomba kazi kwetu. kipi kigumu hapo kuelewa? au si ukute ndio wewe!
 
Back
Top Bottom