Uchaguzi 2020 Hivi kwanini baadhi ya watu wanataka Aidah Khenan wa CHADEMA ajiuzulu Ubunge alioshinda?

Uchaguzi 2020 Hivi kwanini baadhi ya watu wanataka Aidah Khenan wa CHADEMA ajiuzulu Ubunge alioshinda?

Ninashauri awaachie Hilo jimbo au ajiunge nao. Ili Wananchi wafurahie mfumo wa chama kimoja Kama wait ndivyo walivyotaka. Ila Hadi 2025 watanzania ninawaonea huruma Sana kwenye huo mfumo wa chama kimoja.
unawaonea huruma ukiwa upande gani wa dunia?
 
Nadhani kuna wabunge wawili watatu kutoka pemba ACT.

Otherwise kuna viti maalum kma slots 5 maybe kwa CHADEMA.

So kma hawatasusia ina maana wapinzani watakua at least 25 bungeni. So mawaziri kivuli watagawana tu, kumbuka bado kunahitajika mwenyekiti PAC atoke upinzani, kuna mnadhimu mkuu n.k watatosha tu!!
Watatu kutoka Pemba, wawili waliopo, watano wa viti maalum jumla ni 10, sio 25.

Amandla...
 
Wamuache,tukumbuke ubunge sio uwakilishi tu pia ni ajira! Ni nani yuko tayari kuacha ajira nono kiasi hiki ambayo huenda asiipate maisha yake yote yaliyobaki?

Mimi nashauri aachwe aende achukue hizo posho,ikibidi awe bubu asichangie wala kuongea chochote hapo pia atakuwa amewaunga mkono bila kuathiri masilahi yake ya kiuchumi.
 
Hakuna haja ya Dada kujiuzulu. Aende akawakilishe wananchi waliomchagua. Pia ikumbukwe kwa hapa nchini siasa ni ajira... asiache hiyo ajira tamu inayoliliwa hata na wanaCDM. Kimsingi CHADEMA ilishajiharibia toka mwaka 2015 ilipobadili gia angani. Ndani ya hii miaka mitano ya kwanza ya Magu, CHADEMA hakikuwa na watu wenye weledi wa kisiasa hivyo kukosa mwelekeo. Nikiri kwamba hii damage iliyotokea lazima ingetokea sema isingekuwa ya kiasi hiki kama CDM ingebaki kwenye uelekeo wake kabla ya kubadili gia angani. Dada aachwe akawakilishe wananchi.
 
Ubunge aendelee nao maana at the end politics is business like other business, tunamuonea tu huruma jimbo lake litakosa connection ya kupata maendeleo.JPM voice
Itabidi tu apeleke huduma zote licha ya yeye kupita kwake chadema lakini bado wapo wq ccm waliompigia kura lakini hazikutosha kumpitisha mbunge wa ccm.
 
Uko sahihi mkuu!...ila unakumbuka sakata la Mwambe na maamuzi aliyochukua Ndugai?
Yule alikiuka kanuni wazi kabisa ila kwa kuwa ilikua bunge ni lao afu lipo mwishoni wakaona wamuachie tu.

Otherwise mahakamani angevuliwa asubuhi tu maana huwezi kuwa mbunge bila kudhaminiwa na chama.
 
Ccm hapana. Utasikia tu hao wamama wameunga mkono juhudi. Na ndio mwisho wa upinzani Bara kwa miaka mitano ijayo
 
Mwacheni dada wa watu aende bungeni ajiuzulu kwa sababu gani?
Kima Jussa walisusia serikali ya umoja wa kitaifa ilihali wangepewa wote uwaziri. Ni sign of protest kuwa hukubaliani na matokeo yaliyotangazwa.
 
Huyo Dada atapata wenzake wa viti maalum kama 10+. Mwenyekiti anaweza kupata michango kwa hao.
 
Wakuu Salaam:

Nazunguka kila site kufatilia kinachojiri kuhusu matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika juzi.

Mh.Aidah Khenan ameshinda kupitia CHADEMA dhidi ya Kessy kule Nkasi Kaskazini. Sasa kinachoshangaza ni baadhi ya watu ambao pia wana Profile nzuri tuu kwa namna fulani wanapendekeza hata huu Ubunge alioshinda huyu Mh. aupige chini.

Ubunge ni kazi kama kazi zingine na yeye pia anao wanaomwangalia na ndicho alichokua anapigania muda wote wa kampeni.

Ule ulikua ni uchaguzi na yeye ndiyo katangazwa, kwanini watu wanapendekeza na kutoa maoni kabisa asikubali na wala asiende bungeni wakati ndiyo yeye katangazwa?
Kina nani hao wanaopendekeza ajiuzulu
 
Mbunge anadhaminiwa na chama sio wananchi. Hta bungeni mnakaa kwa mfumo wa kichama, same to kamati. Na ndio maana Leo Mbowe akimfuta uanachama huyo dada ndio ubunge wake unafia hapi hapo.
Na utaratibu/kanuni inasemaje juu ya kumvua mtu uanachama bila kutumia hisia binafsi?
 
Wakuu Salaam:

Nazunguka kila site kufatilia kinachojiri kuhusu matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika juzi.

Mh.Aidah Khenan ameshinda kupitia CHADEMA dhidi ya Kessy kule Nkasi Kaskazini. Sasa kinachoshangaza ni baadhi ya watu ambao pia wana Profile nzuri tuu kwa namna fulani wanapendekeza hata huu Ubunge alioshinda huyu Mh. aupige chini.

Ubunge ni kazi kama kazi zingine na yeye pia anao wanaomwangalia na ndicho alichokua anapigania muda wote wa kampeni.

Ule ulikua ni uchaguzi na yeye ndiyo katangazwa, kwanini watu wanapendekeza na kutoa maoni kabisa asikubali na wala asiende bungeni wakati ndiyo yeye katangazwa?
 
Wakuu Salaam:

Nazunguka kila site kufatilia kinachojiri kuhusu matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika juzi.

Mh.Aidah Khenan ameshinda kupitia CHADEMA dhidi ya Kessy kule Nkasi Kaskazini. Sasa kinachoshangaza ni baadhi ya watu ambao pia wana Profile nzuri tuu kwa namna fulani wanapendekeza hata huu Ubunge alioshinda huyu Mh. aupige chini.

Ubunge ni kazi kama kazi zingine na yeye pia anao wanaomwangalia na ndicho alichokua anapigania muda wote wa kampeni.

Ule ulikua ni uchaguzi na yeye ndiyo katangazwa, kwanini watu wanapendekeza na kutoa maoni kabisa asikubali na wala asiende bungeni wakati ndiyo yeye katangazwa?
Mimi nadhani kama anauwezo anaweza kuachia ngazi. Akishindwa aende tu bungeni atoe hoja zinazohusu jimbo lake, akimaliza achape usingizi.
 
Bado mkangamyiko upo Mr BAK.
Jacob kasema anashukuru katangazwa ameshindwa, sasa hii hali inamueka huyu Mama matatani bure.
IMG_20201030_185847_462.JPG

Mama aende bungeni, pamoja na kwamba vyama vipo ila kila mtu ana maisha yake na anatafuta maisha.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom