Hivi kwanini bidhaa za Apple ni ghali?

Hivi kwanini bidhaa za Apple ni ghali?

Uko nyuma sana ki technology, nimekuwekea mfano hiyo snap card, kwenye apple inafanya mautundu kibao sio sawa na hii ya android.
Pia apple utalinganisha na simu za bei range yake yaan kama apple ya milioni basi italingana na android device ya milioni ila huwezi linganisha apple na itel, tecno, infinix nope
Hapo hata suala la bei utaona sio huge difference
yani hujajibu nilicho uliza nimeuliza baada ya ku install hiyo app unagusisha hilo tunda kwenye sensor ipi ili kujia kuwa dawa iliyo puliwa ni kiasi gani?

nijibu ili nikuabliane na wewe kua nipo nyuma kiteknolojia
 
Wakuu kichwa cha habari chahusika.
Nataka kufahamu kwa nini bidhaa za ki electronic za kampuni ya Apple ni ghali sana, kuanzia simu, ipad desktop nk. Kwa nini ni ghali ukilinganisha na zinazotumia windows, android.
Kwa sababu zina ubora wa hali ya juu kabisa.
 
Hapo no3. acha kabisa Password uso au fingerprint mchezoo haha lazma mchepukaji atunze usalama wake lol

hahahah.... very risk (finger print) mtu anakuvizia umelala anagusisha midole yako... bora PIN CODE
 
Bidhaa za apple zmetengenezwa special kwa consumers wenye uwezo wa kuzi afford sio kwa kila binadamu.
 
hahahah.... very risk (finger print) mtu anakuvizia umelala anagusisha midole yako... bora PIN CODE
I believe Apple watakua wamefikiria hilo
Na fingerprint sio kwamba inatumika pekeake na passcode pia inatumia
iPhone X na facial recognition bila shaka wanataka uso uwe active pia nadhani
 
ni vizuri wakifanya hivyo... mie napenda PIN CODE... hizo ndio uhakika.. mambo ya facial.. recognation.. unaweza ukaungua uso.. ikala kwako
 
Shukrani...

naona kwasababu toka mwanzo swali halikuwa lako tumeshindwa kuelewana.

mimi bwana nilifeli G.S... sijui sina akili sijui nini.. nilikuwa simkubalii mwalimu Wangu causes za poverty eti ni Poor education..low income...sasa si ndiyo umaskini wenyewe tunaoujadili..

basi nikafeli bwana...sasa hapa naona napelekwa kule kule. asante.
Brand ni kitu chochote kinachoitambulisha bidhaa na kuitofautisha na bidhaa nyinginezo zilizopo katika soko kwa mfano jina, logo ,design ,ladha,harufu ,sound,design na vyote hivi huunda brand etc...

Brand kwa namna nyingine ni mahusiano kati ya mteja na kampuni au muuzaji yaani ,muuzaji anatengeneza wazo au utambulisho ambao anataka mteja auhusianishe pindi anapokutana na bidhaa au nembo yake kwa mfano mtu anapopoishika simu ya apple anaona ameshika kitu cha kipekee chenye ubora na ghali.... mtu anayeitumia hujiona bora na wa kisasa zaidi ...

Brand hutengenezwa kwa kuangalia aina ya mteja, jinsi kampuni inavyotaka kuhusiana nae, kutengenezwa kwa kitu kinachoendana nae na mwisho ..hutengeneza njia kama matangazo ili kumfikishia ujumbe wenye malengo tofauti...

Ukimuona clouds kafika pale hakufika kwa bahati mbaya maana walikuwepo wenginr pia kabla yake na hata ujuzi wa marketing wa Ruge unamfanya kuwa na advantage kubwa kulingnisha na wengineo...

Natumai umenisoma japo kwa uchache
 
nimeona watu wengi wana base katika QUALITY (display,sijui TUNDA lina bei and other things) kwa upande wangu BIDHAA za APPLE ni ghari kwa sababu zisizo zidi 4..

1-SECURITY (ULINZI) mtumiaji wa bidhaa za apple ana ulinzi wa DATA zake kwa asilimia 95%... tofauti na bidhaa zingine

2-Natural INSUARANCE ... huwezi kutoa icloud bila kuingia gharama... hata kama ukiikota au kuiba.. na BADO unaweza kukamatwa popote endapo mmiliki akiamua kutafuta kifaa chake... ina (TRACKING SYSTEM) ambayo kwa simu kama HUAWEI hawana... ushahid ninao.. wenyewe HUAWEI wamekili kuwa hawana TRACKING SYSTEM ya kurudisha device iliyopotea au kuibiwa kwa OWNER (MMILIKI) ila kwa apple devices ipo..

3-PRESTIGE.... (UFAHARI) ukizingatia APPLE imeshika soko la marekani na wamerakani hawapendi mfanano na nchi za dunia ya tatu na wapo updated.. ndio maana TECHNOLOGY yao wanauza kwa bei ya juu.. so kwa sisi watu wa dunia ya TATU mfano TANZANIA kumiliki bidhaa ya apple uwe vizuri mfukoni.. hivyo basi unajiona na wewe unaenda na wakati...

4-QUALITY (UBORA) sio bidhaa za APPLE tu ndio zina ubora tujikumbushe kampuni kongwe kama SONY-BLACKBERRY enzi hizo..mpaka leo wakitoa device inakuwa na quality (kwa waliowahi kutumia hizi brands wananielewa)..

-quality apple wapo vizuri katika maeneo nyeti na yanayopendwa

-CAMERA zao zina mega pixels kibao na wanampango wa kutengeneza camera yenye uwezo wa kukabiliana na TABIA/UWEZO/UBORA wa jicho la binadamu..

-POWER STORAGE inakaa na charge kwa muda mrefu.. ndio maana hadi charge zinauzwa bei na hazizagai hovyo

-SCREEN QUALITY/SIZE

-software yake HAIINGILIWI NA VIRUS kirahisi

-mpangilio wa applications zake nao umekaa vizuri na mengine mengi.

kwa upande wangu hayo ndio yanafanya bidhaa hii kuwa na BEI kubwa ingawa kuna bidhaa zina ubora zaid ya APPLE au zinalingana..

Kwa maelezo hayo nakupa Tano. Hasa kwenye virus, natumia ipad ya apple lakini sioni kama kuna dalili za kuingiliwa virus, kwa device nyingine tahadhari za mara kwa mara zinatakiwa.Afu ni laini sana kutumia hakuna stac wala nini wakati device nyingine hata Sumsung hufanya magumashi sometime
 
Kwa maelezo hayo nakupa Tano. Hasa kwenye virus, natumia ipad ya apple lakini sioni kama kuna dalili za kuingiliwa virus, kwa device nyingine tahadhari za mara kwa mara zinatakiwa.Afu ni laini sana kutumia hakuna stac wala nini wakati device nyingine hata Sumsung hufanya magumashi sometime
processor za apple huwa neat sana..... yaan ila Blackberry software yao ni mbovu kupindukia... nilikuwa nayo moja blackberry BOLD daah unaflash leo.. kesho wadudu wamerudi..

ukiangalia siku hizi TECNO wanajifanya kukopi IPHONE wakaja na ANDROID version ya LOLIPOP ni nzuri sana.. ila ni mbaya vilevile.. maana sometimes simu inajipiga FACTORY reset.. muda mwingine inajipeleka katika WIFI activation na inastack mpaka uende kuflash ktk computer.. hasa hasa hizi W3/4
 
Wakuu kichwa cha habari chahusika.
Nataka kufahamu kwa nini bidhaa za ki electronic za kampuni ya Apple ni ghali sana, kuanzia simu, ipad desktop nk. Kwa nini ni ghali ukilinganisha na zinazotumia windows, android.

Sana sana wanachouza ni brand name, prestige, coolness, exclusivity(wachache wenye uwezo).

Kwenye security, quality, wako vizuri kama wadau wengine walivyosema.
 
Mku
Bidhaa za apple zmetengenezwa special kwa consumers wenye uwezo wa kuzi afford sio kwa kila binadamu.

Mkuu umemaliza! Sema wabongo wengi ambao hawana uwezo wanang'ang'ania. Repair simple tu Apple Store sio chini ya $300 coz wanajua kama mtu unaweza kuafford zaidi ya $1000 kununua product, huwezi shindwa repair.
 
snapcard inahusika na nin. sorry nakuomba unisaidie
Inapima kiasi cha dawa kilichopulizwa shambani, unanunua cards ziko halafu wakati unapiga dawa unaviweka sehemu tofauti tofauti shambani, ukimaliza unazikusanya kisha unatumia hii app kuanalyse, itakupa majibu kama ulipiga zaidi au kidogo pia itakuelekeza mwanzo wa shamba mpaka mwisho kama ulitumia dawa sawa
 
swali hili niliwahi kumuliza lecturer wangu wa IT, akanijibu kuwa Apple hawatengenezi products zake kwa ajili ya Africa, ni America na Europe tu! Sa sijui ukiwa USA hizi iPhone zinakuwa cheap ama vp
 
Inapima kiasi cha dawa kilichopulizwa shambani, unanunua cards ziko halafu wakati unapiga dawa unaviweka sehemu tofauti tofauti shambani, ukimaliza unazikusanya kisha unatumia hii app kuanalyse, itakupa majibu kama ulipiga zaidi au kidogo pia itakuelekeza mwanzo wa shamba mpaka mwisho kama ulitumia dawa sawa
ahsante kwa kunijuza
 
Back
Top Bottom