Hivi kwanini harakati za kumjua Mungu kupitia Ukristo na Uislamu zimeambatana na vurugu na mateso yasiyoisha?!

Hivi kwanini harakati za kumjua Mungu kupitia Ukristo na Uislamu zimeambatana na vurugu na mateso yasiyoisha?!

Dr wa Manesi

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2024
Posts
997
Reaction score
1,220
Habarini!

Hongereni kwa michango yenu kabambe inayoendelea humu ingawa mingi yenu, haswa siku hizi, imeathirika mno kwa itikadi za kisiasa na dini. Nimeona hii iwe mada yangu ya kwanza kabisa tangu nijiunge humu. Nawaomba muishiriki ipasavyo na kunipatia michango yenu🙏🙏

Kama kichwa Cha habari kilivyo, ukweli ni kuwa ninashangazwa mno na hizi vurugu, mauaji na mihangaiko isiyoisha anayopitia binadamu katika kumuelekea Mungu wa kweli na namna yake sahihi aliyoamrisha tuishi. Kwa kifupi, nitajaribu kutoa mifano kadhaa...

Huko Palestina na Israel Kila siku, na kwa miaka mingi, wanauana tu. Kisa dini (Mungu). Tuliobaki, tukiwemo humu JF tumejichagulia upande kulingana na Imani zetu na hapo hatusikii wala kuona lolote......ni kutetea tu upande wako. Kifo Cha upande wa usio wako unakichekea hata kama ni Cha mateso kiasi gani.
Mkristo anaitwa kafiri na Waislamu Ili kumpatia mateso ya kumkera.
Muislamu anaitwa mfuga majini na Mkristo

Mwekezaji wa kiarabu kwa Sasa hapa Tz anaitwa 'Mwarabu' au 'Mjomba' wa mama Huku mmarekani, muingereza au mzungu yeyote akiitwa vizuri tu 'Mwekezaji'.

Angalia unyanyapaa wanaopitia Sunni kutoka kwa Washia au Washia kutoka kwa Sunni. Hapa Tz kwa Sasa unamea kupita maelezo. Ukiwa ndani ya jukwaa la siasa unauona dhahiri ubaguzi wa kidini.

Mbona watu walielewa kiurahisi tu matumizi ya fedha bila shuruti?!!! Hivi ilikuwa vigumu kiasi gani kumshawishi mmasai achukue sarafu badala ya ng'ombe?!!! Lakini mbona walielewa bila hata kuuliwa?!!!

Mungu ni nuru, nuru ni amani na Upendo daima; Sasa inakuaje Huku Kuna Kila aina ya hila, uongo, upendeleo na Hadi mauaji?!!!!
 
Back
Top Bottom