Ni kweli lakini si unaweza ukazisajili mali zako na kuzikabidhi kwa wataalamu wa biashara kama unaona watoto wako hawana uwezo wa kuziendelezaKutokuandaliwa toka utotoni ili kuja kuendeleza biashara za wazazi wao,wazazi kua wasiri kwenye biashara zao na kutowashirikisha watoto wao,
Waarabu,wahindi na hao wengineo,huwaandaa watoto wao kuja kuendeleza biashara zao,
Wazazi wengi wa kibongo hawana tabia hiyo,watoto hawaandaliwi kuja kushika biashara za wazazi wao,
So,kwavile hawana maandalizi wala experience,hiyo biashara huishia kufilisika tu na kufa,
Pia biashara inahitaji nidhamu ya hali ya juu sana,na hayo yote hupatikana kuanzia kwenye malezi ya mtoto mpaka makuzi yake.
Wana gubu kama baba wa kambo 😃Unawajua mashangazi kweli na baba wadogo na wakubwa wasio na haya wala utu,,
Kila mtu apambane na mzgo wake
Hahahaha hatare sana,,Wana gubu kama baba wa kambo 😃
Sasa tutaanza kila siku hadi lini? Inawezekanaje mzee kaacha hekalu ambapo kila mwanafamilia anaweza akaishi humo lakini niteseke kuanza kutafuta hela ya kiwanja, nijenge nitafute na pesa za biashara kwa vibarua wakati mzee aliacha biashara nzuri ni kuendeleza tu. Na sasa mkigawana hata pesa ya boda haitoshi
Unampa fursa yeye anawaza ufe ili aone hapo unapotolea hizo fursa.Unawajua mashangazi kweli na baba wadogo na wakubwa wasio na haya wala utu,,
Kila mtu apambane na mzgo wake
Sio zote zingine zimefanikiwa na hadi kupita hicho kiwangoKwanza inabidi tujenge uwezo wa kuendesha biashara kwa miaka zaidi ya 20. Hakafu ndio tuangalie uwezekano wa kurithisha. Sasa biashara haitoboi miaka 10 itaendelezwa vipi na kizazi kijacho?
(Je wewe watoto wako unawaandaaje?)_usirudie tena kuniuliza mambo haya tutapigana .Nini kifanyike kiongozi ni kweli tuendelee kuwa masikini na kuanza upya kila siku ilhali wazazi wetu waliteseka kwa ajili yetu?
Je wewe watoto wako unawaandaaje?
😃😃 nimecheka kwa sauti sio kwa biti hilo, niseme sitarudia kiongozi ila pia shukran kwa ushauri mzuri maana elimu ya kuajiriwa nayo ni kikwazo kwa watoto ni bora wafanye vyote kama ulivyoshauri hapo(Je wewe watoto wako unawaandaaje?)_usirudie tena kuniuliza mambo haya tutapigana .
Sasa nitoe ushauri baada ya biti kali kwa rafiki yangu .
Naona iwe ni jukumu mama kwa wazazi kukiandaa kizazi chao kurithi mali na kuziendeleza lakini hapo pia nikukumbushe kwa uchache japo sio kwa umuhimu kuwa shida ya hayo yote mbali na habari za ndugu pande za wazazi kuingilia watoto lakini suala kubwa la wazazi kuamini kwenye elimu kuwa mpe mtoto elimu ili akimaliza aajiriwe ndiyo sababu kuu ya uzorotaji wa maendelezo wa mali za urithi
Kivipi hii inakuwa ,ni pale mtoto unamtupa shuleni hakuna habari ya hata siku moja ushinde naye dykani walau aone vipi unabembeleza wateja au unajinyenyekeza ili watu wanunue bidhaa sasa mtoto wa hivyo hata kesho ukifa haelewi aanzie wapi
Watoto wapate elimu ila wafundishwe pia kuwa mbali na ajira kuna ajira binafsi pia kama wanazofanya wazazi .
Nafurahi kuona jamii kwasasa imeanza kuamka kwa kuamini kuwa kwenda shule hakumfanyi mtoto kuwa tajiri ila juhudi ,ujuzi na bidii ndiyo msingi wa mafanikio .
Ahsante kaka ,karibu tena kaka Kazanazo
Sisi tunachojua tu ni kukata mauno tajiri anapofilisika ama kugongewa mke.Kwanza inabidi tujenge uwezo wa kuendesha biashara kwa miaka zaidi ya 20. Hakafu ndio tuangalie uwezekano wa kurithisha. Sasa biashara haitoboi miaka 10 itaendelezwa vipi na kizazi kijacho?
Hili nalo neno.Kwanza inabidi tujenge uwezo wa kuendesha biashara kwa miaka zaidi ya 20. Hakafu ndio tuangalie uwezekano wa kurithisha. Sasa biashara haitoboi miaka 10 itaendelezwa vipi na kizazi kijacho?
Hili nalo ni tatizo tunaishi kibepari zaidi na sio kijamaaMimi Nadhani inachangiwa pamoja na mfumo wa makazi. Jamii ulizozitaja zina desturi ya kuishi pamoja kama familia hata kijana anapooa. Wanaishi kiukoo. Hii inarahisisha upangaji wa mipango ya kifamilia na pia inarahisisha kudhibiti tabia chonganishi/tawanyishaji toka kwa walioingia ukoo wenu kupitia ndoa. Sisi wabantu wengi tunaishi tofauti. Ukikomaa tuu huyoooo kaishi kuleeee na mkeo. Inakuwa vigumu kufanya vitu kama biashara ya familia pamoja.