Hivi kwanini jamii ya kitanzania hatuwezi kufanya biashara ya kifamilia

Hivi kwanini jamii ya kitanzania hatuwezi kufanya biashara ya kifamilia

Mtu anayemuua Baba yake ili arithi hiyo mali,hawezi kuendelea coz hana akili,mtu mwenye akili timamu hawezi kumuua Baba yake kisa mali,

Hao walisha feli baada ya kumuua Baba yao,pia mali ya dhuluma hua haina baraka,hupukutika na kupotea na itakutesa sana mpaka umauti utakapo kufika.
Laiti wangejua

Jamii zetu Ndio maana umasikini hauishi
Ukienda Uarabuni na Ulaya kote huko mtu akifa lazima maiti ipelekwe hospital ikathibitishwe mtu huyo amekufa kwa nini

Sasa njoo kwetu kwenye dhiki hata serikali haiwezi kufanya hivyo kwa ajili ya gharama

Unasikia tu kelele na watu wanalia
Wanaweka maturubali halafu ngoma maleloni hakuna kuhoji wala nini

Kumbe kanigwa mpaka kafa au kawekewa sumu na watu au mtu wa karibu.

Sisi tunaamini hata wakisema kafa kwa malaria

Fikiria wangapi wameuwawa kwenye jamii zetu
Na Je wangepimwa wote
 
Mfano mzee kaacha nyumba moja center ambayo Ina fremu za kupangisha kama kumi na nyingine ya kuishi pamoja na shamba. Watoto akawa nao 15

Kwa idadi hiyo hao watoto wanashindwa vipi kuweka Mali za mzee wao kwenye uangalizi na wakazisajili na kuziendeleza, wakapangisha fremu zote na mashamba (kama hamlimi) mkaanza kukusanya mitaji na kuwekeza zaidi huku mkiendelea kupeana gawio yani mnaishi kama alivyokuwa anaishi mwenye Mali

NB, hii inawezekana kama wote 15 mtaamua kujishughulisha na mambo mengine zaidi ya kutegemea mali ya baba pekeake kwani wengi kati yenu 15 mtakuwa niwatu wazima mnaojitegemea

Huu ni mfano

Huu ni mfano tu
Linganisha watoto 15 kila mmoja ana interest zake jinsi itakavyo kuwa ngumu ku-manage ukilinganisha na wawili au 3

Wachache ni rahisi kufikia makubaliano,

Nasisitiza idadi ya watoto ni sababu mojawapo tu katika nyingi zaidi kama vile makuzi na tamaduni n.k
 
Hili nalo ni tatizo tunaishi kibepari zaidi na sio kijamaa

Lakini tuchukue mfano wa familia za kizungu kama vile Gates, Rockefeller na Ford ambazo zinaishi kibepari kama sisi lakini zimeweza kudumisha tamaduni ya biashara za kifamilia toka kwa muasisi hadi sasa, wao wanafanyaje?

Kuna kitabu nimesoma kuwa huwa wanasajili Mali zao na kuziweka under trust au Foundation ambapo wataalamu wa uchumi huajiriwa kwa ajili ya kusimamia mali na biashara za warithi huku warithi wenyewe wakiwa kama wasimamizi wakuu na wenye maamuzi

Kwa njia hii hata kama huyo mtoto atakuwa anaishi kivyake haizuii uendelezwaji wa mirathi na haki zake pia hazipotei
Tunaishi kibepari sio kweli, ni kutokuwa na elimu hususan katika suala zima la umiliki mali na biashara
 
Mada inazungumzia mali kutokugawanywa kwa warithi!!

Mali za marehemu Mengi ni LAZIMA zitagawanywa kwenye hiyo kesi yao ya mirathi.

Means hawatatoboa kuwa miongoni mwa familia ambazo mali haikugawanywa kwa warithi.
Hapa mada ni kuendeleza boashara vizazi na vizazi. IPP imeanzishwa zaidi ya miaka 35 iliopita na hadi leo ipo na itaendelea kuwepo. Hiki ndio mleta mada anasema waTz hatuna.
 
Linganisha watoto 15 kila mmoja ana interest zake jinsi itakavyo kuwa ngumu ku-manage ukilinganisha na wawili au 3

Wachache ni rahisi kufikia makubaliano,

Nasisitiza idadi ya watoto ni sababu mojawapo tu katika nyingi zaidi kama vile makuzi na tamaduni n.k
Upo sahihi kuwepo wengi pia kunaongeza ukinzani wa mawazo nakubaliana nawewe

Ila vipi kwa familia zilizodumu zaidi ya karne zimefanyaje wakati jinsi muda inavyozidi kwenda warithi wanaongezeka
 
Tunaishi kibepari sio kweli, ni kutokuwa na elimu hususan katika suala zima la umiliki mali na biashara
Jamii za kitanzania siku hizi tushatoka kwenye ujamaa kila mtu na familia yake na watoto wake hata chumvi hatuombani
 
Hapa mada ni kuendeleza boashara vizazi na vizazi. IPP imeanzishwa zaidi ya miaka 35 iliopita na hadi leo ipo na itaendelea kuwepo. Hiki ndio mleta mada anasema waTz hatuna.
Familia nyingi za kitanzania baada ya kufa muasisi awe Baba au mama wa familia watoto huanza kugombania Mali na kugawana assets au kuziuza kabisa na kugawana hela. Yani hawawezi kuthubutu kutunza na kuendeleza alipoishia muasisi na kufanya biashara hizo au uwekezaji kuwa mkubwa kwa ajili ya kunufaisha kizazi kilichopo na kuandaa warithi kwa ajili ya vizazi vingine

Itaendelea kuwepo wakati hujui kesi ya mirathi itaamua nini!

Au hujui kama kuna kesi mahakamani.
 
Sawa.
 
Back
Top Bottom