Kujenga kwanza foundation imara za hizo familia --- wawe na mshikamano kwelikweli sio waonekane wanamshikamanoNini kifanyike au ndio hivyo kila kizazi kipambane na hali zao
Tatizo ni malengo, jamii za mtu mweusi zinashindwa sababu hakuna umoja kuanzia ngazi ya familia, baba anaamini katika yake, mama nae upande wake ikitokea mtoto amepata hela katuma nyumbani wazazi wanshindwa kujua nini wafanyaje maana hawana unit, kila mmoja anaamini katika biashara yakeWatanzania tulio wengi tumeshindwa kabisa kufanya biashara ya pamoja kama wanafamilia au watu wa ukoo mmoja kwanini?
Tofauti na jamii za kiarabu, kihindi na hata familia nyingi za kizungu hudumisha tamaduni hii ya biashara za kifamilia. Yani kutoka kwa muasisi (hasa alieleta mageuzi ya kiuchumi) familia huendeleza biashara hizo na kurithishana kizazi hadi kizazi bila kuuza wala kugawanywa kwa warithi. Hii husaidia familia hizi kutoanza kutoka mavumbini kama tulivyo wengi wetu hapa tz,
Familia nyingi za kitanzania baada ya kufa muasisi awe Baba au mama wa familia watoto huanza kugombania Mali na kugawana assets au kuziuza kabisa na kugawana hela. Yani hawawezi kuthubutu kutunza na kuendeleza alipoishia muasisi na kufanya biashara hizo au uwekezaji kuwa mkubwa kwa ajili ya kunufaisha kizazi kilichopo na kuandaa warithi kwa ajili ya vizazi vingine
Wengi wa walioacha uwekezaji mkubwa mali zao huishia kuuzwa au kugawanywa au tena kama kaacha wosia mali zisiuzwe basi watoto hawawezi kuendeleza kutoka moja kwenda mbili na tatu bali watabweteka na macho yote yatakuwa kwenye mirathi hiyo iwafanyie kila kitu wala hawatashughulika kuitunza wala kuiendeleza na kuwekeza zaidi mwisho wa siku wanaishia kugombana na kesi zisizoisha mahakamani
Je, elimu ndio tatizo?
Je wewe kama mwanafamilia unaona nini kikwazo?
Je ni kweli biashara za kifamilia hazina tija kwa familia za kitanzania?
Kama ipo tija nini kifanyike?
Umeweka mikakati gani kuhakikisha kizazi chako kinaendeleza unachokifanya?
Karibu tujadili.
Ni kweli lakini pia tuwe na utaratibu wa kusajili mali tunazochuma na watoto au wahusika wa mirathi hiyo pamoja na kuacha wosia wa kisheria ili kuzilinda mali dhidi ya matumizi holela, kuuzwa au kugawanywa, hii pia itapunguza migogoroKujenga kwanza foundation imara za hizo familia --- wawe na mshikamano kwelikweli sio waonekane wanamshikamano
Naam mkuuNi kweli lakini pia tuwe na utaratibu wa kusajili mali tunazochuma na watoto au wahusika wa mirathi hiyo pamoja na kuacha wosia wa kisheria ili kuzilinda mali dhidi ya matumizi holela, kuuzwa au kugawanywa, hii pia itapunguza migogoro
Shida mbongo kusajili mali ni kasheshe kwanza mke na mume hawaaminiani watu wanaogopa kusajili kuepusha kugawana endapo ikitokea talaka hata kama atasajili atatumia jina la mwingine
Hahahaha hamna kazi make hamna mwenye muda na mwingine,,,, imeisha hiyoAiseee. Kazi unayo. Hahaahaa.
Kwa Serikali hii tutasubiri sana haya mawazo yatekelezwe kwenye familia husika yatasaidia sanaSerikali ingeanzisha biashara darasa ambapo vijana wangekuwa wanaomba nafasi za kujifunza ili kupata ujuzi kama ilivyo kwa kada nyingine za kiujuzi.
Hii itasaidia hata kwa vijana walio na urithi wa biashara kutoka kwa wazazi wao kuendeleza biashara zao vizuri kwa ujuzi.
Hatuna umoja ndio maana familia zetu ni masikini zenye uafadhali haziwezi kudumisha hata kwa vizazi vitatu zimepoteaMentality za kubaguana ,kila mtu anajifanya ana maisha yake ya ukubwani ..kama mnavyoamini uchawi basi mnaamini kukaa sehemu na ndugu zako hauwezi kutoboa..
Na kubadilisha ubongo wa mwafrika uwe wa mwarabu, mhindi au mzungu ni kazi sanaMTU mweusi hajitambui na hana vision , tamaduni zao ni kurithishana magonjwa, uchawi, na majina ya ukoo Ila sio Mali .
So sababu ni mentality kuamini ktk kuanzia sifuri.
Ni kweli watoto nao wabinafsi, wavivu na mambumbuWazazi wa kiafrica mioyo ya korosho
Jay Z anakuambia MTU mweusi hayupo serious kwenye Ku-keep wealth kwakuwa MTU anaamini katika currency(Pesa) na sio wealth (Mali).Na kubadilisha ubongo wa mwafrika uwe wa mwarabu, mhindi au mzungu ni kazi sana