Hivi kwanini kuna watu wakisikia jina la January Makamba wanapatwa na hofu?

Hivi kwanini kuna watu wakisikia jina la January Makamba wanapatwa na hofu?

ku
Unachosema unaweza kuwa sahihi kuliko mimi lakini bro nataka ujue kuwa nishati ndio roho ya nchi na wala hili sio suala binafsi la makamba ila ni Nchi nzima. Nachelewa kuamini pingine unaitaji neema ya Mungu kuamini kuwa mchawi wa wizara nimakamba, kama Kuna hujuma zimefanyika kufitini uzalishaji wa umeme nchini anaewajibika ni Rais ambaye ndio mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao niwajumbe. Hili suala kaka sio issue binafsi ya makamba linagusa mamlaka zote za ulinzi nchi na taasisi mkuu. Kumbuka mtendaji mkuu wa wizara by professional ni katibu mkuu. Kuna mengi ya kujiuliza tusimbebeshi zigo la mavi makamba peke yake
kudhani kwamba hii message inamhusu makamba ndo unapokosea..ushasikia kitu kinaitwa syndicate?
 
ku

kudhani kwamba hii message inamhusu makamba ndo unapokosea..ushasikia kitu kinaitwa syndicate?
Ndio nikifahamu even kwenye military trainings kuna kitu kinaitwa "syndicate" nimekuelewa unamaanisha nini likini still staki kuamini kwamba kwenye msafara wao wa mamba hakuna kenge, kama kuna harufu ya manipulation tutajua tu kuna information zita leak
 
Kwa siku kadhaa sasa nikipitia humu JF naona jina la January Makamba linatajwa sana, hasa kwa mabaya. Lakini cha kushangaza watu hao wanaomsema kwa mabaya hawana ushahidi wowote.

Kitu kingine ambacho sikielewi ni kwamba huyu kijana amekuwa waziri kwa takribani miezi mitatu sasa lakini watu wanataka mambo yabadilike ki miujiza bila ya kumpa nafasi ya kuleta mabadiliko.

Hii inapelekea mimi kujiuliza, hivi hawa watu ni kweli wanachukia utendaji wake au kuna jingine?
Hakuna kitu pale ni kubebea bebwa tu, hata ushindani jimboni hawezi, sisi tuloenda shule sawa sawa tunamwona ni mediocre
 
Sitaki maneno tupe ushahidi wa upigaji wake! Vinginevyo wewe ni vuvuzela tu
Unataka ushahidi gani toka kwa huyo tapeli ambaye hata dada yake aliweka rehani utu wake kwa ajili yake?! anajua kucheza na maneno kuwadanganya wajinga kama wewe, hebu muulize huyo bosi wako ile winchi ya tani 26 inakuja lini?
 
Usitukane wenzako wajinga kwa sababu ana mawazo tofauti na wewe. Makamba is an individual hawezi kuwa mkubwa zaidi ya Tanzania, hata akiteuliwa ndugu yako anaweza kufeli. Hakuna kiongozi mzuri kwenye mifumo mibaya hata awe na nani hatoboi. Fitina hazitatusaidia kumbuka makamba ni muajiriwa anaweza kufutwa kazi na boss wake ambae ni Rais na kama kijana ana makandokando leteni data kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika utasaidia mamlaka za uteuzi kufanya maamuzi sahihi. Kwa sabaya watu walitema Nyongo na vielelezo waliweka leo si yuko sero
 
Achana nae imeshazoeleka watu kupakana matope bila sababu wala ushaidi wowote. Jaribu kusoma comment nyingi utagundua kuna watu kama wameshachanganyikiwa

Yeye ndiyo hajielewi. fuatilia haya yafuatayo:
1. Hakuna kreni ya kubeba tani 26.
2. Walitishwa kufanya matengenezo ya mitambo kwa miaka mitano.
3. Mabwawa yamekauka kwa sababu ya ukame.
Wewe huoni jinsi anavyojichanganya mwenyewe!!?

CC: denooJ
 
Viongozi wetu kuna wakati wanajisahau na kuropoka vitu ambavyo havipo, tatizo la kujimwambafai linawakosesha detailed information ili kuuambia umma vitu vinavyoeleweka mwisho wanabaki kuwa suspicious kuwa wanainajisi wizara. Tumpe mda kijana atuoneshe ukomavu wake
 
Wewe uko na maoni yaliyo katika mizani sawia. Ni mtazamo mzuri. Lkn huyu mtu aache mtazamo ya kuwania urais, badala ya kuchapa kazi yeye anawaza urais, hataweza, maana wahenga walisema mshika mawili.... Lkn pia kumponda mwendazake JPM si jambo zuri, yeye hayupo, uzuri wake, ubaya wake, udhaifu wake, uhodari wake, upendo wake na chuki yake vyote vilishakoma. Kwa hiyo kumnanga ni jambo ambalo halina tija, maana hakuna anayeweza kujibu hayo anayoyasema.
 
Reputation ya January iliharibika zilipovuja sauti zao na nape wakimteta Rais na magazeti ya msiba yalichangia kumpaka matope. Lakini pia ugumu wa wizara ya nishati kuhusika sana na ufisadi awamu ya nne ambayo ilimkuza sana kisiasa. Ila kijana Yuko smart sana japo ni opportunist kama wengine.

Kuna kiongozi flani alipanda chuki sana ili kujifaidisha yeye kisiasa na kundi lake wachache tuliliona hili, kiongozi hiyo hakuwa na compromise na baadhi ya watu ambao pengine alihofia umaarufu wao hivyo aliwasiliba kwelikweli Watanzania wakaishi nayo. Ukiwa na kiongozi ambae hajali kuhusu maridhion ( conciliation ) muogope kama ukoma anaweza kupasua nchi vipande
Sauti ya January Makamba ulisiikia au unachanganya madesa na baba yake Mzee Yusuf Makamba?
 
Wewe uko na maoni yaliyo katika mizani sawia. Ni mtazamo mzuri. Lkn huyu mtu aache mtazamo ya kuwania urais, badala ya kuchapa kazi yeye anawaza urais, hataweza, maana wahenga walisema mshika mawili.... Lkn pia kumponda mwendazake JPM si jambo zuri, yeye hayupo, uzuri wake, ubaya wake, udhaifu wake, uhodari wake, upendo wake na chuki yake vyote vilishakoma. Kwa hiyo kumnanga ni jambo ambalo halina tija, maana hakuna anayeweza kujibu hayo anayoyasema.
Umeongea ukweli mtupu maana yeye mwenyewe makamba na mwigulu hawaaminiki kwa sababu ya jinamizi linalowatesa la kuutaka urais. Sijui kwanini mamlaka za uteuzi (vetting group ) zinawapenda, wengi tulishangaa alivyomsagia kunguni jpm hii ni tabia ya kujikwenza coz yeye mtumishi wa umma Sasa anamkomoa nani. Ni kama alikuwa anatutukana sisi grass roots kwamba tutakoma. Nchi yetu Kuna family dynasty wanapeona uongozi kwa kauli ile ningekuwa Rais ningemfuka kazi siku hiyohiyo
 
Sauti ya January Makamba ulisiikia au unachanganya madesa na baba yake Mzee Yusuf Makamba?
Hapana kaka sijachanganya madesa kwenye ile voice note anasikika baba yake January anampigia simu , mzee makamba akaamuliza mwanae kuwa nape yupo. Kaka niko very keen kabla ya kuandika kitu, pia misigano yake na doctor kingwangala na tabia yake opportunism akampaka matope. In short January ana kibarua Kizito cha kujivua gamba
 
Nikishakupa utafanya nini?

Huyo mwizi wa mitihani atatetewa na wewe tu, hawezi kuwa mwizi wa makaratasi ya mitihani akaacha kuwa mwizi wa rasilimali za taifa, never.
Na kwa porojo hizi tu mtaendelea kuteswa sana na huyu kijana. Kusema flan ni mwiz nje ya uthibitisho ni ujinga tu. Msijikute mnapambana na kivuli cha mpakwa mafuta mbelen akawa top manyota a.k.a perezdaa🤣🤣🤣
 
Sina shida na huyu mheshimiwa lakini tangu aingie, shida za UMEME na MAJI zimerudi kwa kasi.

Mwambie ashughulikie hili eneo haraka , linatukera wote.
Halafu naona wanafocus Dar peke yake wakati ni shida ya Taifa zima.

UMEME UMEME UMEME
MAJI MAJI MAJI.

Vinginevyo sina shida nae, hata
25- 30 aendelee.
[emoji120]
 
Attachments

  • JamiiForums1117453574.jpg
    JamiiForums1117453574.jpg
    50.5 KB · Views: 1
Kaka usipende ku generalize vitu unakosea tena sana, utendaji wa wizara hautegemei mtu mmoja tena waziri ambae ni msimamia sera tu na utekelezwaji. Makamba hana professional ya mambo ya nishati ila ana moral authority ya kusimamia uwajibikaji.

Kumbuka bro wizara ni taasisi kuba viongozi wengi tu kuanzia katibu mkuu mpaka mameneja. Tuache chuki tukumbushane Watanzania wote kutimiza wajibu wetu kikamilifu ili kuliletea maendeleo Taifa letu tukufu. Narudia acha chuki
Waziri alianaza kwa uongo na uongo wake huo utamgharimu.

Hivi tatizo la mgao wa umeme ni kwa sababu ya scheduled repairs au ukame ?
 
Kaka usipende ku generalize vitu unakosea tena sana, utendaji wa wizara hautegemei mtu mmoja tena waziri ambae ni msimamia sera tu na utekelezwaji. Makamba hana professional ya mambo ya nishati ila ana moral authority ya kusimamia uwajibikaji.

Kumbuka bro wizara ni taasisi kuba viongozi wengi tu kuanzia katibu mkuu mpaka mameneja. Tuache chuki tukumbushane Watanzania wote kutimiza wajibu wetu kikamilifu ili kuliletea maendeleo Taifa letu tukufu. Narudia acha chuki
Hakuna anayemchukia mtu Makamba labda mwenye chuki ni wewe
 
Back
Top Bottom