Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeshakaa Tabora vijini? Kuna wanajeshi hao wakimbizi unatakiwa ujipange kuwadhibiti sio wakuwaendea kindezi unadhani hao polisi hawana hizo habari ama jeshi unajua kama kuna kikosi hapo cha 25KJ.Tunayo majeshi mengine mkuu, na nimeshaona JW TZ wakisaidia kwenye mambo mbalimbali nchini, sembuse hili la kuwadhibiti hawa vibaka kwenye mapori?
Nadhani hata kipande cha Manyoni Tabora maeneo karibu na Kazikazi au Gang 48 kuna sehemu umetembea mtandao ukawa haupatikani kabisaMiaka 60 baada ya uhuru bado tunayaogopa mapori yetu wenyewe kweli? Kwa nini kusiwe na network hicho kipande wakati hiyo ni highway? Sina lengo la kukushambulia wewe personally but nataka hoja zangu ziwafikie wahusika kwa sababu hatuwezi kupiga maendeleo kwa staili hii.
Mkuu unazungumzia mambo ya zamani sana hayo!!sio kwa sasa,kwanza barabara ni lami tupu,ni hiyo sheria itakuwa imeanza hivi karibuni tu,mimi nimepita sana hilo poli la IPOLE na INYONGA,mala nyingi sana usiku mnene kwa basi.Shukuru sana kwa jambo hilo kuna mapori makubwa sana hiyo baranara nakumbuka tulitaka kutekwa na BUS la SABENA sijui kama lipo. Kuna wahuni sana wa Kirundi na Kinyarwanda hasa pori la Inyonga. Polisi hawa wazembe hawana uwezo wa kuwadhibiti hao wahuni na Wakorofi. Sehemu zote za maporini ukiona kuna Waarabu wanakaa hapo muda mrf tia akili. Tulia kupambazuke mbelembele ya Sikonge jiandae na Nzi pori Mbung'o.
Ni kukurupuka tu mbona siku zote utaratibu huo haukuwepo?hata mwaka jana mwanzoni nimetoka dar asubuhi nimefika mpanda saa 11 alfajiri na MAJINJA BUS?!!Kwanza kabisa mimi sio na sifanyi kazi LATRA.
Pili kwa experience yangu hayo mapori wanayoyasema ni kweli yapo lakini mbaya zaidi humo maporini hakuna network ya mtandao wowote inakamata na hakuna makazi so kwa usiku emergency ikitokea like gari imepata breakdown humo it's you on your own hakuna msaada mtapata labda itokee kuna gari nyingine ipite iwape msaada ila there is no way mtafanya mawasiliano hasa ya simu so possibly wanazuia kwa sababu hio maana pia kuna wanyama pori humo.
Kama ulikua na akili timamu 2000,hiyo njia hapo sikonge ndipo walupotekwa na kuimbishwa mtaji wa masikini,walivuliwa nguo na kuamuriwa kuchezaTuvumilie kwa sababu gani wakati mtu angefika Mpanda saa 6 usiku na kesho anaenda kazini au kwenye biashara zake?
Hoja yako ni nini hasa??Umeshakaa Tabora vijini? Kuna wanajeshi hao wakimbizi unatakiwa ujipange kuwadhibiti sio wakuwaendea kindezi unadhani hao polisi hawana hizo habari ama jeshi unajua kama kuna kikosi hapo cha 25KJ.
Achana na maisha ya barabara za mapori makubwa ama usiombee sakata la kutekwa unaweza kushangaa mzee wako anapigwa mjengo mbele yako. Kulaza gari Sikonge siungi Mkono bora hata Tabora mjini.
Nakubaliana na wewe huu utaratibu ni wa kukurupuka tuu na kusalimu amri kwa vibaka...Miaka ya 1980 Ma Bus njia za Dar to Mbeya, Dar to Arusha na kwingineko yalikuwa yanasafiri mpaka usiku, yaani saa 10 jioni unaenda Kisutu au pale Mnazi mmoja na alfajiri uko mkoani. Kumbuka kipindi hicho barabara zilikuwa mbaya sana na hakuna simu za mkononi kama sasa. Je tunaenda mbele au tunarudi nyuma kimaisha na kimaendeleo?Ni kukurupuka tu mbona siku zote utaratibu huo haukuwepo?hata mwaka jana mwanzoni nimetoka dar asubuhi nimefika mpanda saa 11 alfajiri na MAJINJA BUS?!!
Kwamba 2023 mapori yameondoka? Kama bado yapo basi jua jamaa nao bado wapoUnaleta habari za 2000 leo 2023 na barabara yote ni mkeka? Acheni kuishi kwa kukariri.
Sawa sio kwamba wanaweza kuisha kabisa lakini kwa barabara hiyo ya sikonge -mpanda kwa sasa ni salama kabisa,Kwa TZ mikoa iliyobaki na ujambazi jambazi ! ni KAGERA na KIGOMA.Hasa kigoma.Kwamba 2023 mapori yameondoka? Kama bado yapo basi jua jamaa nao bado wapo
Sent using Jamii Forums mobile app
Polisi nao wanakariri!?..unajua gari zinavyotekwa!?..acha ujinga,wanaolinda usalama wanakuambia hatari,wewe unang'ang'ana,nenda kwa miguu Kama una harakUnaleta habari za 2000 leo 2023 na barabara yote ni mkeka? Acheni kuishi kwa kukariri.
Kwa hiyo vibaka sasa wanadictate maisha ya raia siyo? Kwa hiyo Mungu kutubariki haya mapori na misitu mikubwa ndo imekuwa kama nuksi kwetu au laana kwetu?? [emoji12] Mungu angetupa jangwa tungelalamika pia.Kwamba 2023 mapori yameondoka? Kama bado yapo basi jua jamaa nao bado wapo
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana siyo ujinga ila tatizo ni wewe una mawazo ya kizamani sanaa wakati dunia inaenda kasi sana. Narudia hatuwezi kuendelea kwa kupoteza 8 to 10 hours kwa kisingizio cha usalama wakati kama nchi tuna majeshi ya kutosha kiasi kwamba wakati mwingine huwa tunaenda Congo DRC na kwengineko kuwasaidia wenzetu.Polisi nao wanakariri!?..unajua gari zinavyotekwa!?..acha ujinga,wanaolinda usalama wanakuambia hatari,wewe unang'ang'ana,nenda kwa miguu Kama una harak
Mawazo chanya tuliyoleta ndio yalifanya hiyo bara bara ikawekwa lami. Enzi izo nyie mlikuwa mnawaza utelezi tu...Daaah vijana mnawaza utelezi tuu aiseeee... Leta mawazo Chanya ya kuondokana na hili tatizo kijana..
Siku mkitekwa ndipo utaelewaTuvumilie kwa sababu gani wakati mtu angefika Mpanda saa 6 usiku na kesho anaenda kazini au kwenye biashara zake?
Urefu wa Hilo pori kufuata hiyo barabara ni kilomita ngapi!?..panatakiwa vituo vingapi vya ulinzi vya kuweka Askari!?..au escorts wangapi kwa kila gari!?..unajua kwamba polisi Haina Askari wa kutosha!?..ipi cheap kati ya kuzuwia usafiri usiku na kujaza Askari kwenye Hilo pori!?Hapana siyo ujinga ila tatizo ni wewe una mawazo ya kizamani sanaa wakati dunia inaenda kasi sana. Narudia hatuwezi kuendelea kwa kupoteza 8 to 10 hours kwa kisingizio cha usalama wakati kama nchi tuna majeshi ya kutosha kiasi kwamba wakati mwingine huwa tunaenda Congo DRC na kwengineko kuwasaidia wenzetu. Nitakupa mfano kuna mikoa ya ukanda wa magharibi (ziwa Tanganyika huko) ambako kuna changamoto ya uvamizi na uharibifu wa misitu ya hifadhi wamekuwa wanaungana Police, JW TZ, TANAPA nk kufanya doria kubwa kubwa ambapo wameweza kuwadhibiti wahalifu.