Hivi kwanini Mabasi kutoka Dar kwenda Mpanda, Katavi yanazuiwa kuendelea na safari yakifika Sikonge, Tabora?

Hivi kwanini Mabasi kutoka Dar kwenda Mpanda, Katavi yanazuiwa kuendelea na safari yakifika Sikonge, Tabora?

Mkuu hata mimi ndio njia yangu kwenda Swanga, Wewe umesema ukweli kinachoendelea. Naona mapoyoyo yanabishana kwamba hiyo barabara ina utekaji. Ukiwauliza ni lini Utekaji umetokea mara ya mwisho hawana majibu🤣🤣. Magufuli alipoingia mwaka 2015 akawaambia maRPC hataki kuskia utekaji na pia askari asipande basi kuescot hicho kitu njia hiyo hakijawahi tokea hata kabla ya hapo nadhan tokea 2013 yaani miaka 10 iliyopita hakuna tukio.
Sasa Magu kaondoka tumerudi zama za Mawe kuogopa Majambazi ndani ya Nchi huru.
Madereva wakatumia hiyo loophole wakaweka Vimada Sikonge sasa imekua kero kero kero.
Kuna siku tunatokea Mpanda wakavunga Coastline imeharibika 2 hrs madereva wameenda kupiga mjegejo....

Sikonge dunia nyingine kabisa unaswe na Mmanga ...dadeki
 
Mbona wametaja wenzangu msitu mnene,watekaji hakuna huduma za kijamii...mfano gari ikiharibika ktkt ya msitu kuna watu watashuka watataka kujisaidia kuvuta fegi...huoni ni hatari kuweza kudhuriwa na BM? na wasipate msaada, hayo machache unganisha dots zako pia..
Koboko huko ni homeland..hayo mapori ya akiba chini ya Wazee wa Nyati a.k.a TAWA....mbali na koboko BM kuna scorpion wakutosha....na kitu inaitwa BHOLEKASI hii balaa hatareee sana hata Bakongolee juwa hii
 
Kuna sehemu pia Katavi,Mpanda niliona hao Scorpion za kutosha lkn wenyeji hawaoni hatari wanacheza nao tuu
 
Kuna sehemu pia Katavi,Mpanda niliona hao Scorpion za kutosha lkn wenyeji hawaoni hatari wanacheza nao tuu
Mpanda patamu sana...Mtaa wa fisi ...mtaa wa Simba ..zedigital...kwa Manka....shuka kule kichangani...na ule mtaa live band yaani pisi mpaka buku halafu grade 1 ya chienyeji.....

Ikola....Mwese...Katuma...Kayenze...Karema...Kasekese ...Majimoto...nk
 
Oooh nimeishi hapo soko ya matunda na kota za madini karibu na mtaa wa simba, Mtaa wa Fisi hatari pia na ni mji unaokua haraka nadhani mazingira kama Pwani mchanga mchanga, joto ,minazi nk pako poa..
 
Oooh nimeishi hapo soko ya matunda na kota za madini karibu na mtaa wa simba, Mtaa wa Fisi hatari pia na ni mji unaokua haraka nadhani mazingira kama Pwani mchanga mchanga, joto ,minazi nk pako poa..
Mpanda pazuri kuishi Fedha ipo...maisha si ghali ....Na kambi yangu hapo mitaa ya Stendi mpyaa kule juu karibu na Lyamba Hotel kwa Pinda
 
Ule msitu wa inyonga kuelekea katavi au mlele majimoto ni mbaya sana na hakuna msaada wa haraka unaoweza kupata likitokea la kutokea sisi binadamu tunahisi kucheleweshwa lakini likitokea jambo baya tunaanza kulaumu serikali
 
Unafahamu kwamba nchi hii ina majeshi mengine zaidi ya Polisi? Unafahamu kwamba majeshi mengine pale inapohitajika amiri jeshi mkuu anaweza kutoa maelekezo yakaimarishe ulinzi au kufanya kazi yoyote nyingine? Kuhusu urefu wa hayo mapori jiongeze uingie Google Earth [emoji289] utajua juu... Narudia tena na tena huu si wakati wa kuwapigia magoti wahalifu kwa kuzuia watanzania kutosafiri usiku. Wahalifu wanatakiwa washughulikiwe ili waiogope serikali and not the other way around.
Kazi ya kulinda usalama wa raia na Mali zao ni ya polisi,jw kazi yao kulinda mipaka
 
Kazi ya kulinda usalama wa raia na Mali zao ni ya polisi,jw kazi yao kulinda mipaka
Tumewahi kuona JW kule Mtwara wakisaidia kwenye issues mbalimbali kama Korosho, mikoa ya ukanda wa Magharibi JW huwa wanatumika mara kwa mara kwenye kufanya doria kwenye hifadhi zetu za Misitu ili kupambana na uhalifu na ujangili, ambao wakati mwingine huhusisha wahalifu kutoka nchi jirani.
 
Kwa hiyo tuwapigie magoti vibaka na waporaji mkuu? Mbona Panya road hatukuwapia magoti?
walioweka utaratibu huo wanaelewa kwa undani nini kinaendelea eneo hilo. Mbona wanaokwenda kigoma wakifika kaliua wanalala ili wapite mchana mapori ya igagara-usinge na hawalalamiki?
 
walioweka utaratibu huo wanaelewa kwa undani nini kinaendelea eneo hilo. Mbona wanaokwenda kigoma wakifika kaliua wanalala ili wapite mchana mapori ya igagara-usinge na hawalalamiki?
Walioweka huo utaratibu ni binadamu kama wewe na hiki tunachotoa ni ushauri
 
Tumewahi kuona JW kule Mtwara wakisaidia kwenye issues mbalimbali kama Korosho, mikoa ya ukanda wa Magharibi JW huwa wanatumika mara kwa mara kwenye kufanya doria kwenye hifadhi zetu za Misitu ili kupambana na uhalifu na ujangili, ambao wakati mwingine huhusisha wahalifu kutoka nchi jirani.
uwe unaelewa,KAZI ya jw siyo kuokota korosho Wala kulinda barabara,KAZI Yao ni kulinda mipaka ya nchi
 
Shukuru sana kwa jambo hilo kuna mapori makubwa sana hiyo baranara nakumbuka tulitaka kutekwa na BUS la SABENA sijui kama lipo. Kuna wahuni sana wa Kirundi na Kinyarwanda hasa pori la Inyonga. Polisi hawa wazembe hawana uwezo wa kuwadhibiti hao wahuni na Wakorofi. Sehemu zote za maporini ukiona kuna Waarabu wanakaa hapo muda mrf tia akili. Tulia kupambazuke mbelembele ya Sikonge jiandae na Nzi pori Mbung'o.
Kunambuga kubwa sana hapo pia inaitwa ipemba mpazi mkuu
 
Pori lile sio poa, tumewahi zuiwa hapo enzi hamna lami, tunaitafuta Inyonga tupo na Land Cruiser LX ,tumetoka Sikonge kwenye majukumu X, tuliona Mjuba anatoka porini na chuma mgongoni kuingia kama anachungulia aone nani anakuja nahisi walikuwa wanalia mingo ndiga za abiria, tupo mwendo wa mateka, suka akatu alert tuwe tayari huku akiwa anapunguza mwendo, vioo vilishushwa na sisi upande wetu Wakurungwa wakazikoki kuzielekeza nje tayari kwa lolote kivyovyote. Yule mjuba akatokomea tena porini kama mshale na kukawa kimya na sisi tukaenda kusimama mbele maana kulikuwa na TaTa ya abiria tuliiacha nyuma kuisubiri. Ikapita tukaisindikiza tukaiacha tukasepa zetu bila kumstua dereva wala kuleta taharuki.
Lile poli enzi hakuna lami nakumbuka tulikua tunaenda mpanda kutoka sikonge kuipata koga tulitumia masaa nane sio poa
 
Nasikia Kuna tajiri kajenga hotel yake hapo kwa hiyo anahonga ili watu walale na kula hapo amefanya wasafiri wa mpanda ili apate wateja kwenye biashara zake.
Huo ni uongo mkubwa sikonge ni wilaya ambayo imeendelea sana Kuna hotel na gest za kutosha
 
Kwa hiyo 60 yrs baada ya kujitawala bado tuendelee kuwapigia magoti hawa majangili mkuu? Kwa nini sasa serikali inatumia matrilioni ya pesa kutandaza barabara za lami kila kona ya nchi?
Naona Serikali Haitaki Kutia Mkazo Maana Wakifanya Operation Za Zamani Tosi Na Helicopter Anamwaga Mijegeje Kwenye Mapori Manene Wanapungua Hatimaye Kwisha
 
Back
Top Bottom