Hivi kwanini mwanamke akifiwa na mume wake anaanza kupendeza na kunawiri?

Hivi kwanini mwanamke akifiwa na mume wake anaanza kupendeza na kunawiri?

Na hii ndiyo hoja yangu
Kwanini ameamua maoni ya 'wazungu'
Ona, achana na nani kasema. Angalia tu kimesemwa nini na je ni cha kweli. Sitawatetea tu hao wabongo kisa tumeshea damu tu. La.

Kunenepa, na kunenepeana kunaendeshwa na stress hormone inaitwa cortisol. Ni stress response.

Au basi ni mwitikio wa kujiandaa na stress baadaye. Aidha chaguo, kunenepa kunahusiana zaidi na stress kuliko raha.

Kwa hiyo hata ukimuona mtu amenenepa wakati wa raha zake, tambua kwamba kinachoendesha hayo manenepo ni 'stress za shida ijayo' ni kama mwili unasema "Hapa nimepata raha kidogo tu, nisijisahau. Nnajua shida zipo zinakuja hivi punde. Ngoja nijihifadhie chakula na nishati ya kutosha kwa ajili ya wakati wa dhiki"

Katafiti na wewe utapata majibu yako.
 
Kwanini umetafsi kuwa tafsiri ya wazungu ndio sahihi? Vipi kama ya kwetu ndio sahihi kuliko yao? Hivi wewe umewahi kuona mtu mwenye shida ananenepa na mwenye raha anakonda?
Ndiyo tena wa mama utakuta wanashida sana lakini wananenepa.
 
Mianamume mengi meusi yananyanyasa wake zao
Hayawatunzi yana gubu
So yakiondoka wake wanapata ahueni

✔️✔️
Hili ndio jibu Halisi.

Wengine wanajua kutunza lakini ni wanyanyasaji sana. Wanaume tunatakiwa tubadilike.

Mwanamke ukiishi naye kwa upendo siku ukifa anaweza naye akafa, na Maisha yake yaliyobakia anaweza kuishi kwa msongo wa mawazo.
 
Kwa hili isingewezekana kuacha kulinganisha madam Joanah.

Ndilo lengo la post kuonesha utofauti wa mila na desturi na imani kati ya wazungu na wabongo.
Wabongo: Kunenepa ni dalili ya maisha mazuri, no stress, raha hana mawazo☺

Wazungu: Kunenepa ni dalili ya maisha magumu, stress, shida fullu mawazo😢

Ukweli ni upi? Tafiti zinasemaje?

Maana isije kuwa mtu anapotaabika halafu sie tunasoma tafsiri tofauti kabisa. Badala tumpe pole, na kumsaidia... tunampongeza na kumuonea wivu
Bring back ur common sense, you got it wrong, labda uzungumzie madhara ya unene kwenye mtizamo wa tasnia ya utabibu
 
Nauliza jamani?

Ina maana wake zetu hawana furaha na sisi?...Ila wanatuvumilia tu
Akiwa na mume anajisahau au anakuwa Hana haja ya kupambana kujipendezesha avutie mwekezaji mwingine.
Mtu akitaka kuuza gari au nyumba iliyotumika ndipo hupaka rangi mpya na kufanya marekebisho mengine bidhaa ivutie.
 
Sababu wanakuwa huru na mishetani ya miguu mitatu. Midume ya kiafrica especially mitizii ina gubu na roho mbaya za ukatili na mikoloni
 
Hujiulizi why Baba akifilisika ...watoto wanamsaidia mama Yao tu??
Kina mama wana tabia ya kuwasema vibaya waume zao kwa watoto!! Matokeo yake wababa wakizeeka wanatelekezwa na watoto wao!! Mbaya zaidi kama baba na mama wakitengana!! Wamama acheni tabia hiyo mbaya!!
 
Kisaikolojia huwa wanajiandaa.

Ni mwanamke gani asiyejua kuwa mumewe ndio atakuwa wa kwanza kufa kabla yake?

Maisha lazima yaendelee kwa upande wao.
 
Kuna mmoja namfahamu miezi 6 ya kwanza alinenepa kweli ila saivi namuona ana stress tu pengo linaonekana.
 
Back
Top Bottom