Hivi kwanini mwanamke akifiwa na mume wake anaanza kupendeza na kunawiri?

Hivi kwanini mwanamke akifiwa na mume wake anaanza kupendeza na kunawiri?

Nauliza jamani?

Ina maana wake zetu hawana furaha na sisi?...Ila wanatuvumilia tu
Kuna mambo mengi yanayosababisha aliyeachwa au kufiwa kunawiri; mojawapo ni;
1. Unajua mara nyingi kufiwa huambatana na changamoto nyingi, inaweza kuwa kuuguliwa kwa muda mrefu nk. hii hufanya mwenza aumie na kuchoka sana. Hivyo baadae akirudi hali yake watu hufikiri amenawiri

2. Wanawake wengi wakisha olewa hujiachia kwani hufikiri wameshafikia malengo (Kupata mume)
Na mara wakiachwa hujitahidi kujirudisha ujana/kabla hawajaolewa

3. Kuna baadhi hunawiri kwa kuwa misaada kedekede humiminwa na ndugu/marafiki au watu walio ona fursa
4. nk nk nk
 
Kutoka kuwa vyetu na mume wangu mpaka kuwa vyangu peke yangu, kwa nini asinenepe? Ukiona mwanamke ananenepa baada ya mume wake kufariki achunguzwe pengine kamuwahisha mwenzie. Kama alikuwa na hali ngumu kwa mume wake kwa nini hakuachika?
 
Back
Top Bottom