Mmea Jr
JF-Expert Member
- May 20, 2016
- 798
- 1,871
habari zenu wakuu , moja kwa moja kwenye mada , siku ya jumapili nilipata nafasi ya kumtembelea mzee mmoja mstaafu maarufu sana hapa Iringa . Mzee huyu yeye alikuwa mwalimu ambaye enzi za utumishi wake alipata nafasi ya kufundisha katika shule mbali mbali hapa Iringa kama vile kleruu , mawelewe primary school nk. Katika mawili matatu mzee huyu alianza kuniadithia juu ya miundo mbinu mbali mbali ambayo ilijengwa na mjerumani katika moja ya shule maarufu sana hapa Iringa na Tanzania kwa ujumla shule hii ilifahamika kwa jina la mkwawa high school kabla ya kubadilishwa mwaka 2005 na kuwa Mkwawa college of education , MUCE.
- Anasimulia mstaafu huyu , inadai anadai miaka ya 1950 , shule hii ilikuwa ikifahamia kama st michael enzi cha mjerumani baadae st george enzi za muingeleza na pindi ilipofika mwaka 1964 shule hii ili badilishwa jina na baba wa taifa na kuwa na kuwa mkwawa high school . Anaendelea mzee huyu anadai mbaka kufikia 1970 shule hii ilikuwa ni mungoni mwa shule boraa kabisa nchini Tanzania kwani shule hii ilikuwa ina miundo mbinu yote wezeshi kwa wanafunzi , anasema shule hii ilikuwa na viwanja vya michezo vya kutosha , ndani ya shule hii kulikuwa na kiwanja cha GOLF, kulikuwa na uwanja wa riadha , basketball, netball , viwanja vikubwa viwili vya football vyenye viwango vya kimataifa .
Nikiiwa nimetulia huku nikimsikiliza , mzee aliniambia tisa kumi , shule hii ilikuwa ina njia za chini kwa chini ambazo ziliwawezesha wanafunzi kutoka darasani na kuelekea uwanjani au katika mabweni yao , njia hizi zilitumika sana katika kipindi cha mvua kwani hakukuwa na ulazima kwa wanafunzi kulowana pindi waendapo au waludipo katika viwanja vya michezo hasa katika nyakati za mvua , lakini katika njia hizi za chini kulikua na mifumo safi ya umeme , kulikuwa na maandaki kwa ajili ya kujificha nyakati za vita , pia kulikuwa na mabafu kwa ajili ya kuogea yaliyopatika huko huko chini.
mzee anaendelea mnamo miaka ya 1970's , kipindi cha uongozi wa nyerere ,waziri akiwa kawawa , amri ilitolea na waziri (mzee hakunifahamisha kawawa kipindi hichi alikuwa waziri mkuu au waziri wa elimu mzee hapa hakunieleza vizuri ) na kuzitaka ,maandaki , mabafu pamoja na njia zote cha chini kwa chini zilizopo katika shule ya mkwawa kutotumika na kuzibwa haraka iwezekanavyo .
swali langu , kwanini serikali ilipoonza kukifanyia marekebisho chuo hichi miaka 2003 hadi 2005 haikufikiria kufungua njia zote cha chini kwa chini pindi ilipomkabidhi mkandalasi afanya maboresho ya mazingira na miundo mbinu yote iliyopo katika shule ya mkwawa high school kabla hakijaanza kutumika kama chuo kikuu kishirikishi cha Dar es salaam ??.