hivi kwanini njia (under ground ways ) cha chini kwa chini za shule sekondari mkwawa (kwasasa mkwawa college of education ,muce ) zilifungwa ??.

Mmea Jr

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2016
Posts
798
Reaction score
1,871
habari zenu wakuu , moja kwa moja kwenye mada , siku ya jumapili nilipata nafasi ya kumtembelea mzee mmoja mstaafu maarufu sana hapa Iringa . Mzee huyu yeye alikuwa mwalimu ambaye enzi za utumishi wake alipata nafasi ya kufundisha katika shule mbali mbali hapa Iringa kama vile kleruu , mawelewe primary school nk. Katika mawili matatu mzee huyu alianza kuniadithia juu ya miundo mbinu mbali mbali ambayo ilijengwa na mjerumani katika moja ya shule maarufu sana hapa Iringa na Tanzania kwa ujumla shule hii ilifahamika kwa jina la mkwawa high school kabla ya kubadilishwa mwaka 2005 na kuwa Mkwawa college of education , MUCE.

- Anasimulia mstaafu huyu , inadai anadai miaka ya 1950 , shule hii ilikuwa ikifahamia kama st michael enzi cha mjerumani baadae st george enzi za muingeleza na pindi ilipofika mwaka 1964 shule hii ili badilishwa jina na baba wa taifa na kuwa na kuwa mkwawa high school . Anaendelea mzee huyu anadai mbaka kufikia 1970 shule hii ilikuwa ni mungoni mwa shule boraa kabisa nchini Tanzania kwani shule hii ilikuwa ina miundo mbinu yote wezeshi kwa wanafunzi , anasema shule hii ilikuwa na viwanja vya michezo vya kutosha , ndani ya shule hii kulikuwa na kiwanja cha GOLF, kulikuwa na uwanja wa riadha , basketball, netball , viwanja vikubwa viwili vya football vyenye viwango vya kimataifa .

Nikiiwa nimetulia huku nikimsikiliza , mzee aliniambia tisa kumi , shule hii ilikuwa ina njia za chini kwa chini ambazo ziliwawezesha wanafunzi kutoka darasani na kuelekea uwanjani au katika mabweni yao , njia hizi zilitumika sana katika kipindi cha mvua kwani hakukuwa na ulazima kwa wanafunzi kulowana pindi waendapo au waludipo katika viwanja vya michezo hasa katika nyakati za mvua , lakini katika njia hizi za chini kulikua na mifumo safi ya umeme , kulikuwa na maandaki kwa ajili ya kujificha nyakati za vita , pia kulikuwa na mabafu kwa ajili ya kuogea yaliyopatika huko huko chini.

mzee anaendelea mnamo miaka ya 1970's , kipindi cha uongozi wa nyerere ,waziri akiwa kawawa , amri ilitolea na waziri (mzee hakunifahamisha kawawa kipindi hichi alikuwa waziri mkuu au waziri wa elimu mzee hapa hakunieleza vizuri ) na kuzitaka ,maandaki , mabafu pamoja na njia zote cha chini kwa chini zilizopo katika shule ya mkwawa kutotumika na kuzibwa haraka iwezekanavyo .

swali langu , kwanini serikali ilipoonza kukifanyia marekebisho chuo hichi miaka 2003 hadi 2005 haikufikiria kufungua njia zote cha chini kwa chini pindi ilipomkabidhi mkandalasi afanya maboresho ya mazingira na miundo mbinu yote iliyopo katika shule ya mkwawa high school kabla hakijaanza kutumika kama chuo kikuu kishirikishi cha Dar es salaam ??.
IMG_20220813_131729_910.JPG
 
Labda waliona haina maana au pengine sababu za kiusalama zaidi

Ngoja wajuzi watufahamishe zaidi
kwa mtazamo wangu mimi , nilikuwa nafikiri kwasababu sasa kimekuwa chuo , miundo mbinu hii iliyofungwa kama ingefunguliwa huenda ingeongeza sifa fulani katika chuo hiki ukizingatia kwa sasa wanaoyoitumia ni watu wazima tofauti na hapo mwanzo
 
yeah ni kweli kabisa mkuu
 
Sema wazungu kuna standard fulani wamejiwekea hatutakaa tuwafikie hata robo..

Ukiangali shule za sasa zinavyojengwa, ukafananisha na hizo za mkoloni ni mbingu na ardhi..

Majengo ya mkoloni japo yamejengwa miaka 60 mpaka 90 iliyopita ila bado ni masterpiece mpaka sasa.
 
habari zenu wakuu , moja kwa moja kwenye mada , siku ya jumapili nilipata nafasi ya kumtembelea mzee mmoja mstaafu maarufu sana hapa Iringa . Mzee huyu yeye alikuwa mwalimu ambaye enzi za utumishi wake alipata nafasi ya kufundisha katika shule mbali mbali hapa Iringa kama vile kleruu , mawelewe primary school nk. Katika mawili matatu mzee huyu alianza kuniadithia juu ya miundo mbinu mbali mbali ambayo ilijengwa na mjerumani katika moja ya shule maarufu sana hapa Iringa na Tanzania kwa ujumla shule hii ilifahamika kwa jina la mkwawa high school kabla ya kubadilishwa mwaka 2005 na kuwa Mkwawa college of education , MUCE.

- Anasimulia mstaafu huyu , inadai anadai miaka ya 1950 , shule hii ilikuwa ikifahamia kama st michael enzi cha mjerumani baadae st george enzi za muingeleza na pindi ilipofika mwaka 1964 shule hii ili badilishwa jina na baba wa taifa na kuwa na kuwa mkwawa high school . Anaendelea mzee huyu anadai mbaka kufikia 1970 shule hii ilikuwa ni mungoni mwa shule boraa kabisa nchini Tanzania kwani shule hii ilikuwa ina miundo mbinu yote wezeshi kwa wanafunzi , anasema shule hii ilikuwa na viwanja vya michezo vya kutosha , ndani ya shule hii kulikuwa na kiwanja cha GOLF, kulikuwa na uwanja wa riadha , basketball, netball , viwanja vikubwa viwili vya football vyenye viwango vya kimataifa .

Nikiiwa nimetulia huku nikimsikiliza , mzee aliniambia tisa kumi , shule hii ilikuwa ina njia za chini kwa chini ambazo ziliwawezesha wanafunzi kutoka darasani na kuelekea uwanjani au katika mabweni yao , njia hizi zilitumika sana katika kipindi cha mvua kwani hakukuwa na ulazima kwa wanafunzi kulowana pindi waendapo au waludipo katika viwanja vya michezo hasa katika nyakati za mvua , lakini katika njia hizi za chini kulikua na mifumo safi ya umeme , kulikuwa na maandaki kwa ajili ya kujificha nyakati za vita , pia kulikuwa na mabafu kwa ajili ya kuogea yaliyopatika huko huko chini.

mzee anaendelea mnamo miaka ya 1970's , kipindi cha uongozi wa nyerere ,waziri akiwa kawawa , amri ilitolea na waziri (mzee hakunifahamisha kawawa kipindi hichi alikuwa waziri mkuu au waziri wa elimu mzee hapa hakunieleza vizuri ) na kuzitaka ,maandaki , mabafu pamoja na njia zote cha njini kwa njini zilizopo katika shule ya mkwawa kutotumika na kuzibwa haraka iwezekanavyo .

swali langu , kwanini serikali ilipoonza kukifanyia marekebisho chuo hichi miaka 2003 hadi 2005 haikufikiria kufungua njia zote cha chini kwa chini pindi ilipomkabidhi mkandalizi afanya maboresho ya mazingira na miundo mbinu yote iliyopo katika shule ya mkwawa high school kabla hakijaanza kutumika kama chuo kikuu kishirikishi cha Dar es salaam ??.View attachment 2322906
St. Michael na St. George na Kongwa European School zilikuwa za watoto wa wazungu tu, shule hii baada ya uhuru ilibadilishwa na kuwa Mkwawa ambapo wanafunzi wa kizungu walihamishiwa Mbeya School (IYUNGA SECONDARY SCHOOL) ambayo nayo kabla ya uhuru ilikuwa European School na kuwa shule ya kawaida ila ya kulipia ada. Kuna mambo mengi ya kufikirika ambayo yalisemwa yakidhaniwa kuwa yalikuwepo huku hayakuwepo kiuhalisia. Shule zote hizo zilikuwa na miundo mbinu ya hali ya juu sana yaani viwango vya ulaya, hili wanafunzi waliosoma Iyunga mpaka miaka ya sabini mwanzo wanaweza kuthibitisha.
 
Sema wazungu kuna standard fulani wamejiwekea hatutakaa tuwafikie hata robo..

Ukiangali shule za sasa zianavyojengwa, ukafananisha na hizo za mkoloni ni mbingu na ardhi..

Majengo ya mkoloni japo yamejengwa miaka 60 mpaka 90 iliyopita ila bado ni masterpiece mpaka sasa.
Shule za Sasa zinatengewa kaeneo kadogooo au inajengwa mlimani. Ngozi hii Ina tatizo sana
 
Wangezirudisha tu hizo njia kama kuna uwezekano, iwe ni sehemu ya utalii; vinginevyo labda iwe ni hatari kwa usalama wa watumiaji; kuhusu mambo ya kikubwa, wote wanaosoma hapo ni wakubwa kwa sababu wanamiaka zaidi ya 18, hakuna logic ya kuzifunga kwa sababu hiyo.
 
Niliwahi kusoma hapo,Nililala Shaban Robert East,lower wing.Mtaani Makanyagio kwa Chuwa tulikuwa tunanunua fegi tano kwa shilingi mia.
Long time sana.
Hizo handaki zilikuwa zimefunikwa.
mkuu hebu jazia nyama kidogo , yani zilikuwa hazipitiki au wakati ulifika uongozi ukaamuaa kuzifunga
 
Wangezirudisha tu hizo njia kama kuna uwezekano, iwe ni sehemu ya utalii; vinginevyo labda iwe ni hatari kwa usalama wa watumiaji; kuhusu mambo ya kikubwa, wote wanaosoma hapo ni wakubwa kwa sababu wanamiaka zaidi ya 18, hakuna logic ya kuzifunga kwa sababu hiyo.
mimi pia naungana na wewe kama kuna uwezakano ungefanyika utaffiti naa kama zinafaa basi zifunguliwe na kufanyiwa maboresho madam ramani zipo nadhan itakuwa kazi rahisi tu
 
Back
Top Bottom