Hivi kwanini Nyerere aliidhinisha kunyongwa Mwamwindi?

Ni kweli Wamarekani wanatekeleza sana hii adhabu na uzuri wao hawana double standards kwamba waangalie mkosaji ni nani au aliyeathiriwa ni nani ili i determine uharaka wa kutekelezwa adhabu husika
Wewe, Doble Standards ipo, sana maekani, Kule utakavyochuliwa wewe mweusi sivyo atakavyochukuliwa Mzungu.

Hivi unakumbuka kisa cha yule mtoto, wa kiafrica aliyenyongwa George Stanney, hebu fuatilia huko, utaona jela za huko uone weusi walivyowengi magerezani.

Hata hii adhabu ya kunyongwa inawahusu sana watu weusi, kuliko weupe.
Hizi nchi ziliondelea watu waziangalii mabaya yake, bali huziangalia kwa mazuri yake tu.

Sasa mfano wewe, kunyongwa kwa Mwamindi tu, mnaona alionewa wakati aliua kweli, kama wewe unasimamia haki, sheria insemaje unapoonewa hata kwa makusudi.

Inasema uuwe, na mahakama iamua kwa kutumia busara, jamani sheria haifanyi kazi kwa vikra zenu, bali sheria hufuata sheria.
 
KUTEMBEA NA MKE WA MWAMWINDI NI UONGO SI KWELI kulikuwepo na unyanyasaji aliwafanyia wenye mashamba makubwa pia siku ya kuuawa alitoa maneno ya kuudhi kwenye makabuli ya ndugu zake mwagito...... Rest in peace mnyalu
labda nikupe na hiyo link ya habari kamili mkabishanie huko na wajuzi ingawa bado nasema mada yetu kwanini Hati ilisainiwa haraka
Nyumbani kwa Mwamwindi na Mnara wa Dr
Sehemu Ya 4:Kwa nini Mkulima Mwamwindi alimuua RC Dr.Kleruu? – Joel Nanauka
 
Hii ndo sababu nilopewa na babu yangu kwan alikua kiongoz katika kipind icho na alikuwepo iringa pia
 
Mkuu ungepata Habari kamili kutoka kwa Blog ya Mjengwa na nyinginezo ambazo wakazi wa Iringa wanajieleza ndio ungejua ukweli wa huyu jamaa ambaye nyuma yake alikuwa a kundi kubwa lililotaka kumtetea likaogopa Dola ni km enzi tu za Dr Ulimboka na migomo ya MaDr lkn ipo siku Historia ya yote itaandikwa hata km si kwa kizazi hichi chetu cha woga
 
Shukrani san mkuu, ngoja niisake hiyo blog ya Mjengwa kama ina habari za kina kuhusu hii issue
 
Sibishi kwamba alipatikana na hatia kama alivyokiri mwenyewe na hukumu aliyopata ni stahili yake. Hoja ni kwamba kwanini Nerere asi sign za wengine waliouwa kwa ukatili mkubwa na akaidhinisha Mwamwindi anyongwe haraka?
Kwa maoni yangu Nyerere alikuwa mjamaa sana na Kleruu alikuwa mfuasi mkubwa wa siasa za Nyerere. Kipindi kile mtu yeyote aliyenda kinyume na siasa za kijamaa alikuwa adui mkubwa sana aliyestahli kifo
Ilkuwa ni vita kali dhidi ya mabepari na ubeberu
Pamoja na hukumu ya mahakama mwalimu angeweza kuchelewa kusaini lakini kwa sababu aliyeuawa alikuwa mjamaa na jemadari wa mwalimu katika itikadi zake nafikiri hii ilisaidia kuhitimisha kunyongwa kwake.
 
Inawezekana pia ikawa hivyo mkuu
 
Kipindi kile nyimbo zilizoimbwa mashuleni na majeshini, mazungumzo baada ya habari na jumbe mbalimbali ziliashiria ujamaa ulikolea na hapakuwa na mchezo mtu aliyejaribu kwenda kinyume kingempata cha umpata na hivi alitoa fundisho wengine wasijejaribu jambo kama lile, hata sasa unaweza kuona kuwa mtu anayejaribu kwenda kinyume na wito wa hapa kazitu reaction inakuwaje! Bila shaka ni msaliti na wameshadokea dawa ya msaliti
 
Na hata baada ya kifo cha Dr Kleruu zilitungwa nyimbo nyingi sana kumsifia na pia kulaani mauji yake ambayo yalielezwa yalipangwa na kutekelezwa na wapinga maendeleo

Sina hakika kama ugomvi wa RC Kleruu na mkulima Mwamwindi ulikua una element zozote za tofauti za kiitikadi za kisiasa, kwamba ujamaa/mjamaa dhidi ya ubepari/bepari au ukabaila/kabaila kama terminologies zilivyokua zinajulikana wakati huo
 
Enzi zile hakukuwa na vitu kama Jamii forums, facedook. NGOs. Makundi ya haki za binadamu. hakukuwa na vyombu binafsi vya habari kwa hivi mtawala alikuwa na nguvu sana kutekeleza aliyotaka huku pembeni aakiwa amezunukwa na kila aina ya wapambe, waandishi, manasiasa kila mtu kwa hivi yeyote aliyeathiri dhamira yake aasingepenya au kupata mpiga debe
 
Haswa uko sahihi na yule mwanzilishi wa siasa za kijamaa asingependa kuona akizuiwa na yeyote adhabu kubwa ilikuwa kifo kama onyo kwa wapinga ujamaa na mabepari kwa ujumla.
 
Tuwekee mifano ya waliosamehewa adhabu ya kifo ili tulinganishe.
mifano ipo mingi tu km unaweza fuatilia
Kabrasha la Kunyongea Mada ya Mshana post #340 tu
 
Kipindi kile kama ni udikteta ulikua ni udikteta kamili. Kiongozi yoyote anayeanza kuhutubia ilikua ni LAZIMA aanze na 'ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI WA CHAMA" hahahaaa tumetoka mbale sana kama Taifa aisee
 
Utaona hata katika dunia ya leo watawala wenye nia na mwelekeo wasiotaka upingwe wana hasira sana na watajaribu kuvisakama vyombo vyote vinavyokuwa kikwazo katikakutimiza dhamira zao. mfano watavifungia vyombo hivyo au kuvipiga marufuku, watatunga sheria mbaya ili mradi tu azma yao itimie. dunia ya leo ni tatizo kwa watawala kama hawa kuliko dunia ya jana
 
Ugomvi haukuwa na element za kiitikadi tatizo ni tukio la uuaji na aina ya mtu aliyeuawa. lilikuwa vita dhidi ya ujamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…