Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,101
- Thread starter
-
- #81
Ndio maana Mwalimu Nyerere akakasirika sana labda?Ugomvi haukuwa na element za kiitikadi tatizo ni tukio la uuaji na aina ya mtu aliyeuawa. lilikuwa vita dhidi ya ujamaa
2007 Nyerere alikuwa rais?mifano ipo mingi tu km unaweza fuatilia
Kabrasha la Kunyongea Mada ya Mshana post #340 tu
unakijua unachokiuliza au unataka kumegewa kila kitu2007 Nyerere alikuwa rais?
βKutokana na mifumo yetu, hatuna uhakika kama anayehukumiwa ni kweli ametenda kosa. Wapo wengi waliohukumiwa kunyongwa, lakini wakashinda rufaa na sasa wapo huru,β anasema.
Sungusia anaeleza zaidi kuwa adhabu ya kifo imepitwa na wakati kwa sababu imejikita katika msingi wa βjino kwa jinoβ.
Hoja ya Sungusia inapata uzito kwa kuangalia hukumu kadhaa. Desemba 18, mwaka 2007, Jaji Frederick Werema
Eti wanamuita mwenye heriHuyu jamaa kwangu bado ni shujaa sana lakini najiuliza hao wanaotaka kumpa Mwalimu utakatifu wanatumia vigezo gani ilhali mtu alikua ana sign hati za vifo?
Saaana sio waafrica tu hadi huko dunia ya kwanza .. hiii ndio sababu inayonifanya nisipende kuwa kiongozi wa juuKuna suala jingine, kuna kitu kinaitwa extra judicial killings, viongozi wengi wa Kiafrika inawezekana wakawa hawaonekani kwamba wana idhinisha hati za hukumu za vifo kwa waliohukumiwa adhabu hiyo lakini wameua sana katika mauaji yasio ya kisheria, kimyakimya
Ni kama Leo umuue Bashite,Jiwe anaweza akahukumu mwenyewe kesi yakoTunaambiwa katika kipindi chake chote cha cha miaka 23 kama Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere alisaini hati chache sana za kunyongwa watu waliopatikana na makosa mahakamani na kupewa adhabu ya kifo. Miongoni mwa hati za kunyongwa alizowahi kuziidhinisha ni ile ya aliyekua mkulima mkubwa wa enzi hizo mkoani Iringa Bwana Saidi Mwamwindi aliyeshtakiwa kwa kosa la kumuua aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Iringa wakati huo Dr Kleruu
Kama umewahi kupitia hati za mashtaka, mwenendo wa kesi na maelezo ya hukumu ya watu waliopatikana na makosa ya kuua kwa kukusudia utagundua kwamba wengi wao walitekeleza mauaji hayo kwa ukatili sana wengine ukijiuliza hawa kweli walikua ni binaadamu wenye roho!? Pengine haitakupata huruma kwa hukumu inayopitishwa juu yao
Said Mwamwindi ni kweli aliua, na wala hakuisumbua mahakama kwani alikiri hivyo mwenyewe na akahukumiwa kunyongwa hadi kufa. Ila kuna simulizi nyiingi sana zinanazohusiana na mauaji aliyofanya na hata baadhi ya watu wanahalalisha kitendo alichofanya na kukiita cha kishujaa!
Wengi ya wanaomuana kua ni shujaa wanasema RC Kleruu alikuachanzo cha mauaji yake mwenyewe. Alikua kweli anamnyanya sana huyu Bwana Mwamwindi. Kwanza alikua anatoka kimapenzi na mkewe halafu alikua anamfatafata sana na kumtolea lugha za kashfa(abusive languages). Kibinadamu hiyo ni dharau na ni adhabu kubwa sana kumpa mwanaume mwenzio hasa kama umemzidi kwa cheo au hata pesa
Kwa intelijensia aliyokua nayo Mwalimu Nyerere lazima atakua alijua chanzo halisi cha Mkulima Mwamwindi kumpiga risasi RC Kleruu., na ingawa mazingira yaliyomfanya atende kosa lile yalikua hayampi nafuu yoyote kisheria linapokuja suala la adhabu kwa maoni yangu hati ya kunyongwa Said Mwamwindi haikupaswa kusainiwa harakaharaka hasa ikiwa inajulikana (angalau kwa uwazi) kua Nyerere hakupenda adhabu ya kifo
Nawauliza wakongwe waliopo JF wenye kujua vizuri historia ya tukio hili na yaliyotokana na jambo hilo, haraka ya Nyerere kusaini hati ya kunyongwa hadi kufa Said Mwamwindi ilitokana na;
1. Hasira za Nyerere kuuliwa RC wake?
2. Mauwaji aliyofanya Mwamwindi yalikua ni ya kikatili kuliko wauwaji wengine walioua kwa kukusudia?
3. Chuki za Nyerere kwa aliowaita Makabaila(wamiliki wa mashamba makubwa) ambapo Mwa
mwindi anaangukia hapo?
4. Double standards wanazokua nazo wanasiasa wengi hasa wa kiafrika katika kuwatendea
watu wao?
Naomba kuelimishwa wakuu
Hii ilikuja kukemewa na sokoine .. Aisee mchonga aliwaburuza Sana watuKipindi kile kama ni udikteta ulikua ni udikteta kamili. Kiongozi yoyote anayeanza kuhutubia ilikua ni LAZIMA aanze na 'ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI WA CHAMA" hahahaaa tumetoka mbale sana kama Taifa aisee
Ulikua na fursa hiyo mkuu? I mean ulikua kwenye siasa na nafasi ya kupanda kwenye nyadhifa za juu ulikua nayo? What happened then?Saaana sio waafrica tu hadi huko dunia ya kwanza .. hiii ndio sababu inayonifanya nisipende kuwa kiongozi wa juu
Hata Doris Liundi alihukumiwa hivyohivyo mbona hakunyongwa?Mahakama ndo ilioamua anyongwe baada ya kumkuta na hatia..Nyerere hausiki hapo
Hahahaaaa, yawezekana mkuuNi kama Leo umuue Bashite,Jiwe anaweza akahukumu mwenyewe kesi yako
That's my point mkuu?Hata Doris Liundi alihukumiwa hivyohivyo mbona hakunyongwa?
Hahaa mkuu hayo mambo sio ya kuyamwaga hapa ... utanisamehe tafadhaliUlikua na fursa hiyo mkuu? I mean ulikua kwenye siasa na nafasi ya kupanda kwenye nyadhifa za juu ulikua nayo? What happened then?
Na kuna conspiracy theories nyiingi kuhusu kondoka kwa Sokoine, wengine wanasema haikua accident as suchHii ilikuja kukemewa na sokoine .. Aisee mchonga aliwaburuza Sana watu
Nimekuelewa kiongozi wangu, nimekulewaπππHahaa mkuu hayo mambo sio ya kuyamwaga hapa ... utanisamehe tafadhali
Yeahhh hizo conspiracy zipo nyingi sana ... na zina elements za ukweli kiasi chakeNa kuna conspiracy theories nyiingi kuhusu kondoka kwa Sokoine, wengine wanasema haikua accident as such
Ama kweli utawala wa nchi ni SIRIKALIYeahhh hizo conspiracy zipo nyingi sana ... na zina elements za ukweli kiasi chake
Dah! Wengine wanasema ilikua ni risasi iliyommaliza palepale kwenye "eneo la tukio", yaani yapo maelezo mengi tofauti tofauti kuhusu hilo jamboYeahhh hizo conspiracy zipo nyingi sana ... na zina elements za ukweli kiasi chake
Wengine wanasema kwamba sokoine mpaka ana fikishwa moro hospital alikuwa mzima ila ila kuna daktari mmoja wapo alikuwa kwenye jopo la wanaompatia huduma alikuwa ni usalama akampigia simu mchonga na kumwambia kuwa jamaa bado hajavuta kamba " mchonga akatoa amri wammalizie kisha yeye akakimbilia haraka sana kutangaza kuhusu msiba wa sokoine ....
Usingeweza kumuachia huru mkuu, mikono yako ingefungwa na sheria maana Mwamwindi alikiri mwenyewe mahakani kua alimuua RC mwenyewe akimuita mbwa wa serikaliNi hoja nzuri inayohitaji hekima . Ila ningekuwa hakimu ningemuachia huru .
Ndio hivyo mkuu "Dah! Wengine wanasema ilikua ni risasi iliyommaliza palepale kwenye "eneo la tukio", yaani yapo maelezo mengi tofauti tofauti kuhusu hilo jambo