Hivi kwanini tunawabadilisha watoto wetu majina asilia baada ya ubatizo au kubadili dini?

Hivi kwanini tunawabadilisha watoto wetu majina asilia baada ya ubatizo au kubadili dini?

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,113
Reaction score
65,124
Wasalaam,
Hivi kwanini mtoto alizaliwa anaitwa Mkwavinyika lakini baada ya kufanyiwa ubatizo anaanza kuitwa Paulo.

Au mtu alizaliwa anaitwa Mushaija lakini baada ya kutaka kumuoa Maiumuna anasilimu na kuanza kuitwa Juma.

Sasa nataka kufahamu haya yote yanatokana na nini:
Je, majina yetu asilia yanakuwa na walakini au yanabeba nuksi fulani hivi kwa mtoto ?

Au, hayo majina hutumika kama utambulisho wa dini ya mtu fulani kama ilivyo kwa kabila ?
 
Unajua sielewi mfano Ghana SA, wanatumia majina ya asili na wanaenda church na misikitini, sasa sisi sijui kwann hatuitani majina ya kiasili wenye vyeti vya ubatizo au, Uislam.

Tunaambiwa yanabeba maroho na mapepo wachafu! Inasikitisha mno!

Everyday is Saturday............................. 😎
 
Ingependeza zaidi kama na ww ungetumia Mkwavinyika ama Jina lolote lenye asili hiyo na sio Malcom.
Hili nalo litategemea asili yangu ni wapi, maana kwa wengine Malcom, Mohamed au Patel ni majina yao asilia.
 
Ni ujinga na upumbafu tu wa watanzania..Mtu yuko radhi umuite fox ila ukimuita mbweha mtakosana...ila mi watoto wajianadae kwa majina ya kiasili.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Nadhani hili limetokea sehemu nyingi sana Afrika hasa baada ya kuletewa dini kutoka Uarabuni na Ulaya.
 
Tuliaminishwa na Wazungu jina lako ni lazima liendane na la Mtakatifu mmoja. Inawezekana kuna Mtakatifu Mainda lakini hakuna records zake hivyo nikaitwa Judith.
Lakini bahati mbaya sana kuna majina mengine ya Kiislamu au Kikristo yalikuwepo hata kabla ya hizi dini kuzaliwa.
Mfano Julius, lile lilikuwa ni jina la kilatini ambalo limekuwa likitumika na Waroma hata kabla ya Yesu kuzaliwa.
 
Back
Top Bottom