Usifemoyo
Member
- Dec 26, 2017
- 62
- 53
Tumeaminishwa kuwa majina ya kizungu/kiarabu ni bora zaidi kuliko majina yetu ya asili na pia tumeaminishwa kuwa kutumia majina haya mapya ni aina fulani ya ustaarabu au kuelimika.Wasalaam,
Hivi kwanini mtoto alizaliwa anaitwa Mkwavinyika lakini baada ya kufanyiwa ubatizo anaanza kuitwa Paulo.
Au mtu alizaliwa anaitwa Mushaija lakini baada ya kutaka kumuoa Maiumuna anasilimu na kuanza kuitwa Juma.
Sasa nataka kufahamu haya yote yanatokana na nini:
Je, majina yetu asilia yanakuwa na walakini au yanabeba nuksi fulani hivi kwa mtoto ?
Au, hayo majina hutumika kama utambulisho wa dini ya mtu fulani kama ilivyo kwa kabila ?
Lakini pia tumedanganywa kuwa baadhi ya majina yetu ukimpa mwanao atarithi tabia za jina hilo kama liliwahi pengine kutumiwa na wazee wa zamani katika ukoo wenu, hivyo majina yetu tunaya-associate na urithi wa mizimu, hivyo ili kuepuka chain ya mizimu ya kiukoo ni bora eti utumie jina la kizungu/kiarabu. Hapa napo ndipo tumedanganywa na tukadanganyika kweli kweli.
Binafsi nilipokuwa mdogo nikiwa na miaka kama 14 hivi nilibatizwa nikachagua jina la kizungu. Nilikuja kutafakari kwa kina nikiwa na miaka 25 hivi nikaona hiki tulichoaminishwa ni ujinga kabisa. Maana tumedanganywa na tukaamini kuwa ni kweli eti majina ya kizungu/kiarabu ni bora zaidi na wengi huwa tunaamini kuwa ni lazima utumie jina la kizungu/kiarabu unapobatizwa/kusilimu.
Baada ya tafakari yangu ya kina niliamua kubatizwa upya ili nizaliwe upya kwa kutumia jina langu la asili na sio lile la awali nililojipa kipindi nabatizwa mara kwanza. (Nashukuru Mungu baba alipokuwa anaenda kutuandikisha shuleni alikuwa anatuandikisha majina ya asili na pia hata la kwake alikuwa anatumia la asili. Hivyo shuleni nimekuwa nikitambulika kwa majina ya asili ie first name na surname ni ya asili).
Siku ya ubatizo ya nilipoamua kubatizwa mara pili ili kufuta lile jina kizungu nitumie majina yangu ya asili, mbatizaji aliponiuliza jina langu nilimtajia majina matatu yote ya asili, nashukuru Mungu hakuwa na pingamizi juu ya majina hayo hivyo alinibatiza kwa majina yangu ya asili ie jina langu ni la asili, baba naye jina lake ni la asili (japokuwa yeye ana jina la ubatizo la kizungu), jina la babu pia ni asili. Hivyo hayo ndio majina yangu kila mahali kuanzia mtaani, kazini, na kanisani.
Na nimeazimia kuwa wanangu wote lazima watumie majina ya asili. Labda waje waamue kujipa wenyewe hayo ya kizungu/kiarabu wakiwa wakubwa.