Fursa Pesa
JF-Expert Member
- May 30, 2012
- 4,631
- 3,527
Kwa sababu yanajengwa kwa sadaka na harambee,lakini pia sehemu ya fedha zinazochangwa zinaweza kusaidia masuala mengine ndani ya shirika nyingine kukua.Tangu nakua kule Keko Magulumbasi, kunapokuwa na ujenzi wa Kanisa la KKKT huwa miaka na miaka ujenzi haukamiliki.
Mifano ipo Mingi tu. Tangu mwaka 1998 Kanisa la pale Korogwe Kimara KKKT ujenzi haujaisha.
Segerea mwisho hadi kesho bado ujenzi haujaisha.
Kibamba shule njia ya Kibwegere ujenzi haujaisha.
Kumara Suka karibu na Temboni ujenzi haujaisha.
Hii ni baadhi ya mifano michache tu, hivi shida nini?
Hata hivyo kupanda Kwa gharama za vifaa vya Ujenzi nayo ni sababu mojawapo.
Nyingine ni kuhama kwa Washarika watoaji.
Lakini pia kuhamishwa kwa Wachungaji kunapopelekea anayekuja kuwa mtizamo tofauti.
Mwisho,kuwa na wasimamizi wasio waaminifu katika utunzaji na matumizi mabaya ya fedha,ingawa hii si sababu muhimu sana.