Hivi kwanini ukiwa mahali alipo Rais Magufuli unajisikia amani sana!

Hivi kwanini ukiwa mahali alipo Rais Magufuli unajisikia amani sana!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nipo hapa Ikulu kwenye mkutano wetu sisi wafanyabiashara na mkuu wa nchi, kwa kweli najisikia amani sana.

Nimewahi kufika mahali hapa katika awamu zilizopita lakini safari hii najisikia amani zaidi kuwepo mahali hapa.

Ule wasiwasi na mashaka havipo kabisa yaani najihisi nipo mahali salama kabisa.

Mungu mbariki Rais Magufuli
Mungu wabariki wafanyabiashara
Mungu wabariki watanzania.

Amina!
Maendeleo hayana vyama!
 
We haupo ikulu

Humo huingii n.a. SIMU MWALIKWA KAMA WEWE
 
Inawezekana huwa akiongea humuelewi au mafanikio yako yanakufanya usijali anachosema kwakuwa tayari unachotafuta ni kulindwa tu maslahi yako. Lakini kuna hili pia, huenda wewe umezoea kujipendekeza maana hizi ndo kauli za watu wa tabia hiyo.
 
Umeingiaje na simu? Manaake kwa waliopo humo updates mpk watoke. Visimu vyote viko getini kwenye locker...unless we staff
 
Inategemeana na ufahamu wako na utegemezi wako pale Lumumba. Wengine tunajisikia kinyaa na kichefuchefu!
 
HUNA AKILI WEWE NA FAMILIA YAKO IMEPATA HASARA, KWA HIYO MAGUFULI NI MUNGU WAKO,kuna kitabu kwenye biblia kinasema alaaniwe yeye yaan mwanadamu amtegemeaye mwanadamu mwenzie we ni jinga na una laana,wazazi waliokusomesha ni hasara tupu
 
Hawaruhusu watu wasiojulikana kufanyizia watu hapo hapo nyumbani.
 
Kabla ya mambo yote, tuambie huo wasiwasi na mashaka uliokuwa nao ilikuwa wa nini au ilikuwa unasababishwa na nini.

Kwa mawazo yangu, hapo unajipendekeza tu
 
Hata ng'ombe mjinga anaweza kujisikia amani akipelekwa machinjioni.

Magufuli alisema (kwa uongo) kwamba kampeni yake haijachukua hata senti tano ya mfanyabiashara, ujumbe ulikuwa kwamba yeye ni msafi sana na pesa zote za wafanyabiashara ni chafu.

Wafanyabiashara wakubwa wanatimka. Dangote kiasi kikubwa kasepa, Etihad wamesepa, Exxon Mobil wamesepa, tumebaki kufanya biashara za danganya toto kwa wakulima wa korosho.

Sasa hivi watu wenye international strategy kina Bakhressa ndio wanapeta, biashara Tanzania imekuwa ngumu sana, kwa sababu rais kichwamaji.

Ali Mufuruki alijifanya kumpigia chepuo mwanzo, yeye mwenyewe analalamika sana jinsi Magufuli alivyofanya nchi iwe si rafiki wa wafanyabiashara.

Huyu ni rais anti-business, kalikoroga sasa anaona hawezi kuendesha nchi bila ushirikiano wa wafanyabiashara, anatapatapa.

Hawa makada wengine wapo kazini tu wanatupa hagiography kama kawaida.

Huyu alishamuweka Magufuli sawa na Mungu kwake, siwezi kushanga akileta vituko hapa.
 
Back
Top Bottom