Hata ng'ombe mjinga anaweza kujisikia amani akipelekwa machinjioni.
Magufuli alisema (kwa uongo) kwamba kampeni yake haijachukua hata senti tano ya mfanyabiashara, ujumbe ulikuwa kwamba yeye ni msafi sana na pesa zote za wafanyabiashara ni chafu.
Wwafanyabiashara wakubwa wanatimka. Dangote kiasi kikubwa kasepa, Etihad wamesepa, Exxon Mobil wamesepa, tumebaki kufanya biashara za danganya toto kwa wakulima wa korosho.
Sasa hivi watu wenye international strategy kina Bakhressa ndio wanapeta, biashara Tanzania imekuwa ngumu sana, kwa sababu rais kichwamaji.
Aali Mufuruki alijifanya kumpigia chepuo mwanzo, yeye mwenyewe analalamika sana jinsi Magufuli alivyofanya nchi iwe si rafiki wa wafanyabiashara.
Huyu ni rais anti-business, kalikoroga sasa anaona hawezi kuendesha nchi bila ushirikiano wa wafanyabiashara, anatapatapa.
Hawa makada wengine wapo kazini tu wanatupa hagiography kama kawaida.
Huyu alishamuweka Magufuli sawa na Mungu kwake, siwezi kushanga akileta vituko hapa.