Hii kitu tangu miaka ya 2000 wachambuzi wanasema Marekani itapitwa na China na Leo tupo 2022.
Mwaka 2011 kuna report ya IMF ilisema kwamba China itaipita USA kiuchumi 2016
2016: when China overtakes the US | Mark Weisbrot
Kuna nyingine ilisema China ingeipiku USA mwaka 2020 lakini Leo tupo 2022 na Ngoma bado mbichi.
Na sasa hivi reports zinasema China itaipiku Marekani 2030s au 2050.
Marekani itakuja kupitwa kiuchumi lakini sio Leo wala kesho ukizingatia Kwasasa uchumi wa China haukui kwa Kasi kama ulivyokua unakua mwanzoni Kwa double digit Kwa sasa unakua kwa 6-5 asilimia na kila siku Kasi inapungua,pia China inasumbuliwa na tatizo la uzee,rasilimali watu (watu hawazai Sana),viwanda vinahama vinahamia nchi nyingine km Vietnam nk sababu gharama ya uzalishaji inazidi kuongezeka (China).Tuombe Mungu atupe uhai tuone itakavyokua,lakini km trend ikiendelea hivi siioni China ikiipiku USA kiuchumi Karne hii.