Hivi kweli hili taifa la Marekani (USA) litakuja kupitia kiuchumi?

Hizo tawala zote ulizotaja ilikuwa ni race moja, kamwe dunia haiwezi kuwaliwa na race moja, lazima utaanguka tu. Unapozungumzia Marekani unazungumzia race zote za dunia, makabila na mataifa yote ya dunia, yaani wahaya, wahindi, wachina, wakorea, wasomali, wakerewe, waarabu, waajemi, nk. Kwa kifupi wamarekani ni watu wa makabila yote ya dunia. Yaani kwa lugha nyingine ni akili kutoka Kona zote za dunia zimeungana kutengeneza kitu kimoja. Kwenye jeshi la Marekani kuna hadi wachanga, kwa hiyo usilinganishe kabisa na hizo tawala zingine zilizopita, Marekani ni mkusanyiko wa dunia nzima hakuna mwenyeji pale.
 
Kwa hoja yako, Marekani itatawala milile?
 
usisahau ulimwengu ni pamoja na Asia , Afrika na Amerika , ntajie taifa lililoweza kutawala kote huko ukiacha Uingereza na Ufaransa ambao walitawala karibu nusu ya dunia , mtawala wa dunia kwenye historia ni USA tu
 
Kikeshi & ki-anga Mrusi amisha mzidi USA,kiuchumi ndio huko China anaenda kumpiku ni swala la muda atanguka jumla jumla.

Hiyo ya kuwa watu wa race zote kwenda hata ikitokea Tanzania Leo ndio super power kila mmoja atataka kuja, kama ilivyo Dar es Salaam.
 
usisahau ulimwengu ni pamoja na Asia , Afrika na Amerika , ntajie taifa lililoweza kutawala kote huko ukiacha Uingereza na Ufaransa ambao walitawala karibu nusu ya dunia , mtawala wa dunia kwenye historia ni USA tu
USA anaitawala Dunia kupitia hela yake,kitu ambacho Nchi nyingi zinaanza kukataa mfumo huo.
 
Hakuna kitu kama hicho. Wachina hawamiliki hata asilimia moja ya uchumi wa marekani ndani ya marekani ila marekani anamiliki zaidi ya asilimia 50 ya uchumi wa China.
 
Hii kitu tangu miaka ya 2000 wachambuzi wanasema Marekani itapitwa na China na Leo tupo 2022.
Mwaka 2011 kuna report ya IMF ilisema kwamba China itaipita USA kiuchumi 2016
2016: when China overtakes the US | Mark Weisbrot

Kuna nyingine ilisema China ingeipiku USA mwaka 2020 lakini Leo tupo 2022 na Ngoma bado mbichi.

Na sasa hivi reports zinasema China itaipiku Marekani 2030s au 2050.
Marekani itakuja kupitwa kiuchumi lakini sio Leo wala kesho ukizingatia Kwasasa uchumi wa China haukui kwa Kasi kama ulivyokua unakua mwanzoni Kwa double digit Kwa sasa unakua kwa 6-5 asilimia na kila siku Kasi inapungua,pia China inasumbuliwa na tatizo la uzee,rasilimali watu (watu hawazai Sana),viwanda vinahama vinahamia nchi nyingine km Vietnam nk sababu gharama ya uzalishaji inazidi kuongezeka (China).Tuombe Mungu atupe uhai tuone itakavyokua,lakini km trend ikiendelea hivi siioni China ikiipiku USA kiuchumi Karne hii.
 
usisahau ulimwengu ni pamoja na Asia , Afrika na Amerika , ntajie taifa lililoweza kutawala kote huko ukiacha Uingereza na Ufaransa ambao walitawala karibu nusu ya dunia , mtawala wa dunia kwenye historia ni USA tu
Kwani U.S.A anatawala nchi ngapi mfano Uingereza alivyotawala karibia nusu ya dunia ? Nitajie angalau mataifa 10 yaliyo chini ya amri ya U.S.A Kama ilvyokuwa kwa Muingereza, Ujerumani, Egypt,Roman Empire , Greece
 
China haijawahi kusema wataifikia U.S.A 2020 Bali target yao waliipachika jina Economic Mission/Vision 2050 hii ndio target waliopanga kumfikia U.S.A kiuchumi
 
Hakuna kitu kama hicho. Wachina hawamiliki hata asilimia moja ya uchumi wa marekani ndani ya marekani ila marekani anamiliki zaidi ya asilimia 50 ya uchumi wa China.
We jamaa unajua asilimia 50 kwe uchumi wa nchi ikoje? Yaani 50 ya uchumi wa China unashikiliwa na U.S.A Kama ingekuwa ni rahisi hivo Kama unavyosema Trump angeishaifanya china kuwa Kama Sirlanka . Fatilia vikwazo walivyowekeana Kati ya china na marekani wakati wa utawala wa Trump Nani aliumia na Nani ukuaji wake wa uchumi ulidorora Kati ya U.S.A na china .U.S.A alijuta kumuwekea Vikwazo vya kibiashara mchina
 
Ile ilikuwa issue ya trade balance, china walikuwa wananufaika zaidi na marekani kwasababu ya purchasing power ya US hivyo trump alitaka kupunguza deficit. Hapa tunaongelea suala la nani anamiliki uchumi wa mwenzake.
 
Mbona Uingeleza aliweza?
 
China haijawahi kusema wataifikia U.S.A 2020 Bali target yao waliipachika jina Economic Mission/Vision 2050 hii ndio target waliopanga kumfikia U.S.A kiuchumi
Hakuna mahali nimesema China imesema itaifikia USA 2020 bali nimesema report za IMF ndo zilitabiri hivyo.

Kumbuka hata Japan miaka ya 1990s ilitabiriwa itaipiku USA miaka ya 2000s lakini mpaka Leo haijafanikiwa na imepitwa na Uchina. Kwa trend hii inayoenda sasa sidhani Kama China itaipiku Marekani kiuchumi. Tuombe uhai tuone itakavyokua.
 
USA kabalance. GDP na per Capita vyote ni kubwa tofauti na mchina
 
Kwani U.S.A anatawala nchi ngapi mfano Uingereza alivyotawala karibia nusu ya dunia ? Nitajie angalau mataifa 10 yaliyo chini ya amri ya U.S.A Kama ilvyokuwa kwa Muingereza, Ujerumani, Egypt,Roman Empire , Greece
Kitendo cha kutumia Android, symbian, appstore ushatawaliwa na apa tulipo tunatawaliwa pia kupitia izo platform
 
Hakuna kitu kama hicho. Wachina hawamiliki hata asilimia moja ya uchumi wa marekani ndani ya marekani ila marekani anamiliki zaidi ya asilimia 50 ya uchumi wa China.
Reference pls [emoji41][emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…