Hivi kweli mtu anaamni Marekani hakuna madini? Africa tujitathmini sana

Uongo mkubwa sana huu na matangopori ya vijiweni tu, unahitaji kuwa kichwa panzi sana kuamini ujuha na propaganda kama hii.
Mkuu,
Don't argue with a FOOL or else he'll drag you down to his level..
Utafiti hupingwa kwa utafiti, ila pimbi kama hilo haliwezi kukuwekea hapa data za kiutafiti. Linakuja tu na uongo wa kupika kutoka kichwani kwake. Ukimuomba rejea (reference) ya andiko lake hana!
 
Tuiite Marekani ya wazungu, wakoloni, waliovamia na kidogo kuwaua Wahindi wekundu wote au Marekanj ya nani?! Mleta mada ebu tuelimishe...
Ukisemq hivo waaarabu africa nao walivamia na kuua weusi wote na kuzifanya nchi za kiarabu kwanzia mosri mpaka morocco
 
Ukiambiwa reserve ya mafuta aliyonayo Marekani hutaamini. Utajiuliza kwa nini anunue mafuta toka nje jibu ni kwamba anayatunza mafuta yake kwa matumizi yake iwapo kutatokea uhaba wa mafuta duniani. Marekani ni ya tisa Ulimwenguni kwa wingi wa mafuta .
 
HAKUNA NCHI ISIYOKUWA NA RASILIMALI........HATA JANGWANI MADINI YAPO CHANGAMOTO NI WAKAT WA EXPLORATION
 
Unajua hata mafuta(petroleum)yalianza kugunduliwa marekani?ama unajitoa akili.

Mmarekani yeye anachofanya raslmal zake hatumii anavuna kwengine anajiwekea reseve ya kutosha.
Marekani haweki reserve ya mafuta wala gas. Anachofanya analinganisha gharama za kuchimba, sio kila mafuta yanachimbwa kwa gharama sawa. Saudi Arabia na Kuwait wanatumia nguvu kidogo sana kuchimba mafuta hivyo hata wakiuza kwa bei ndogo wanapata faida. Wakati Marekani inabidi ifanye cracking ikitaka kujitosheleza. Pia Marekani inatumia mafuta mengi sana, kwa siku wastani wa pipa milioni 20. Wakati Marekani mwaka jana ilizalisha wastani wa pipa milioni 13 kwa siku, ikifuatiwa na Saudi Arabia na Urusi.

Kwahiyo Marekani inachimba mafuta yanayofikika kwa gharama nafuu kwake, then inachukua nje kujazia deficiency. Ikitokea bei ya mafuta imepanda sana duniani ndipo Marekani inaweza tumia cracking kujitosheleza sababu breakeven itafikiwa na kutakuwepo economic justification.

Kuna nchi kama Venezuela ina mafuta mengi sana kwenye reserve ila yanahitaji gharama kubwa kuyachimba. Investors are not interested, wanaishia kuchimba visima vichache.
 
Usiamini sana takwimu za hao vinyeo..sasa kama USA ndio inaongoza kwa mafuta kwanini wanakomaa na mwarabu na kama wana madini ya kutosha kwanin wamejazana congo..muafrica hana reasoning kila anachokisoma anaamini bila kufikiri. Angalia impact ya mafuta UAE angalia mjia wa Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ajman, Umm Al-Quwain na Fujairah miji imejengwa na mafuta na imejengeka kisasa sasa hiyo marekani imejengwa na nini kama sio watumwa na dhuluma marekani ni ileile aliyoenda babu yako 1960 na wewe ukienda leo hakuna tofauti??
 
Madhara ya moshi wa mwenge. Bure kabisa.
 
Toka jf imeanza kusambaza link Facebook, na vilaza wa fb wakajazana huku, jf hatupumui....

Kwenye huu uzi kuna watu wanashusha PUMBA TUPU tena kwa kujiamini mpaka unashindwa hata kumsahihisha....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…