Hivi kweli mtu anasomea Pharmacy miaka 4 kuja kugawa dawa tu? Serikali rekebisheni hili

Safi sana
 
Sasa viwanda vyenyewe havipo tufanyeje?
Serikali ina wajibu wa kuwawezesha wasomi wake ikiwa ni pamoja na kuwapa mikopo ili waweze kuanzisha viwanda! Aidha serikali ina wajibu wa kuwakaribisha wawekezaji wakubwa wenye makampuni ya madawa kuanzisha matawi ya makampuni yao hapa nchini!
 
Kutest dawa as How?
Maana michakato yote ya madawa wanafanya Pharmacist..
Ila swala la Kuotesha wadudu Hapo utagombana na Scientist (Lab scientist) watakuja juu na wenyewe Hapa πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Maana wao ndo wanaohusika na shughuli zote za Maabara pamoja na Wadudu wote iwe ni microbiology au parasite

Na maswala ya Udongo watu wa SUA ma Agrochemistry watakuua 🀣🀣
 
Wewe jamaa umemuelekeza kwa hekima sana.
 
Naam mkuu,tusaidie kuchambua na mchango wa Watu wa Maabara upoje katika tiba.
Kama umesoma vyema, hakuna anaeweza kusema ni muhimu zaidi kuliko mwingine. Wote tunashirikiana.

Daktari anapofika sehemu na Differential diagnosis, huitaji mtu wa maabara kumtatulia utata kwa labda kuthibitisha au kukanusha mambo. Kama mtu wa maabara akiamua atafute umwamba kwa mtoa huduma mwingine basi tutaokota watu wengi mtaani. Ukipewa majibu ya sukari iko juu, tayari utaenda kuua. Ukiambiwa hana malaria wakati anayo hapo ni shida.

Hivyo, tunahitajiana kwa kiasi kilekile kwa kila/fani au mmoja mmoja ni suala la kuthamini kazi ya mwenzako hata kama una exposure nayo.

Ni kila mmoja atimize wajibu wake na kufuata miongozo.
 
Daktari ni mtaalamu wa tiba ambaye anajihusisha na utambuzi, matibabu, na kuzuia magonjwa. Wanaweza kuwa na ujuzi katika fani mbalimbali kama vile upasuaji, ndani ya dawa ya ndani, au upasuaji wa akili.

Mfamasia, au mtaalamu wa dawa, ni mtaalamu wa dawa na anajishughulisha na utoaji wa dawa na ushauri wa kiafya kuhusu matumizi sahihi ya dawa. Wanaweza kufanya kazi katika maduka ya dawa, hospitali, au kampuni za dawa.

Kwa ujumla, daktari ni mtaalamu wa tiba anayefanya utambuzi na matibabu, wakati mfamasia ni mtaalamu wa dawa anayetoa huduma za dawa na ushauri kuhusu matumizi sahihi ya dawa.
 
Nje ya mada,, hivi hii mitihani ya leseni huwa ina umuhimu gani? Wakat mtu kashafaulu mitihani yote kwanzia level ya kwanza mpka level ya mwisho.... yaan mtu unasoma mwaka wa kwanz mpka wa mwisho unafaulu vizuri alf tena unatakiwa ufanye mtihan wa leseni na maswali yanayo toka yanaanzia mwaka wa kwanza semestr ya kwanza mpka mwaka wa mwisho semestr ya mwisho...ni kwamba hao Pharmacy council wanataka wajiridhishe kwa lipi?? Alf maswali yenyew unakutana na snalio za kutosha??
Mwenye uelewa jamn anisaidie
 
Nimewahi kuwaza hili ingawa Mimi siko kwenye tasnia ya afya.
Anayeandika au kuamuru mgonjwa atumie dawa ipi ni doctor, anayeamua mgonjwa atumie vipi dawa ni doctor. Sasa rule ya pharmacist ni nini?

[emoji28][emoji28][emoji28] yani vituko tu,wafamasia walipaswa wawe viwandani au kwenye maabara kugundua na kutengeneza dawa sio kungangania dirisha la kugawa dawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…