Hivi kweli mtu anasomea Pharmacy miaka 4 kuja kugawa dawa tu? Serikali rekebisheni hili

Hivi kweli mtu anasomea Pharmacy miaka 4 kuja kugawa dawa tu? Serikali rekebisheni hili

Hakuna daktari hakuna mfamasia , hizi ni kada zinazotegemeana sana .

Daktari kuna semister katika usomaji wake anakutana na kitu tunaita pharmacology lakini vivyo hivyo mfamasia kuna muhula ambao anasoma pia habari za prescription .

So kikawaida hawa watu inawapasa kutegemeana sana kuliko inavyodhaniwa ila shida inakuja pale tunapojaribu kuikuza kada ya udaktari kiasi cha kuwapuuza wafamasia .
Kwa zaidi ya 99% ya Zahanati hapa Tanzania hazina mfamasia, hazijawahi kuwa na mfamasia na wala hazihitaji mfamasia, zina Daktari na muuguzi na zinapiga kazi fresh. Hapo utasemaje?

Kwangu mimi Daktari na muuguzi ndio uti wa mgongo wa utoaji huduma za afya kwenye ngazi zote za vituo. Bila uwepo wa watu hao kwa hakika huduma za afya ni kama hakuna.
 
Haruhusiwi hata kutibu, lakini anatibu kuliko hospitali, wanawake na Watoto wana complication sana matatizo yao, sasa jamaa anaelewa vizuri mpaka Dawa, na Dawa nyingine unaweza kumuandikia mtu aitafute kwenye pharmacy kubwa na ukipata tatizo limeisha.

Namjuwa kwa zaidi ya miaka 20 yupo vizuri sana.
Hata kwa Dr Mwaka watu wanajaa.
 
Hivi kweli mtu anasomea Pharmacy 4 yrs, kuja kugawa dawa tu? Serikali rekebisheni hili,how comes Dr.medicine arecommend dawa?

Wakati mtaalam yupo lakini hafanyi kazi yake?
Mfamasia kazi yake ni kutengeneza dawa na siyo kigawa dawa. Mfamasia anatakiwa akafanye kazi kwenye kiwanda cha kuzalisha dawa na siyo duka la dawa. Bahati mbaya sana Tanzania hakuna viwanda vingi vya dawa hivyo wanaishia kugawa dawa.

Acha kulinganisha mfamasia na daktari (MD) hao ni watu wenye taaluma tofauti, mfamasia amebobea katika chemistry ya dawa na daktari MD amebobea katika biology ya mwili wa binadamu na namna ya kuutibu unapokuwa na matatizo.

Kwa kifupi mfamasia anatengeneza dawa kwa maekekezo ya daktari.
 
Hivi kweli mtu anasomea Pharmacy 4 yrs, kuja kugawa dawa tu? Serikali rekebisheni hili.

Medical officer ana recommend dawa akiwa hana uzoefu wowote wala Elimu kuhusu dawa, hii sio sawa. Viongozi wetu wa juu Kuna sehemu mnakwama sana, waacheni wafamasia WAFANYIE kazi walichofundishwa darasani.
Umesomea ufundi dawa, fungua kiwanda utengeneze dawa.
 
Argument yako haiko sahihi.
Mabishano ya kisayansi katika taaluma ya utabibu (diagnosis, treatment (prescription) ni jambo la siku zote, la kawaida, lipo dunia nzima. Hivyo sio issue.

Kuhusu mfamasia kuamua huo ugomvi wa dosage hapo Ilala, unatupa picha hii.
-Madaktari walikuwa na uelewa tofauti katika dosage ya dawa kwa mgonjwa.

-Mfamasia ametumika kama msaidizi mtaalamu (consultant) katika kusaidia hitimisho ya mjadala wa dosage. Na hivyo ndivyo taaluma ya utabibu inataka.
Yawezekana pia wako kwenye level tofauti. Mmoja labda ni CO na mwingine ni MD. Na ndiyo maana Tabibu akishaona mgonjwa tatizo lake ni complicated basi humpa Rufaa kwenda kuwaona Tabibu wengine wa level tofauti.
 
Kwa zaidi ya 99% ya Zahanati hapa Tanzania hazina mfamasia, hazijawahi kuwa na mfamasia na wala hazihitaji mfamasia, zina Daktari na muuguzi na zinapiga kazi fresh. Hapo utasemaje?

Kwangu mimi Daktari na muuguzi ndio uti wa mgongo wa utoaji huduma za afya kwenye ngazi zote za vituo. Bila uwepo wa watu hao kwa hakika huduma za afya ni kama hakuna.
Umeongea kiwepesi sana labda kwakua huelewi shida inayotokea huko kuanzia kwenye huduma inayotolewa,hasara ya serikali inayopata kutokana na mnyonyoro wa ugavi usivyo sahihi,katika zoezi la kugawa nyota vituo vya kutolea huduma pharmaceutical personnel anatakiwa awepo katika ngazi hadi ya zahanati kutokuwepo inabaki kuwa gap tu la serikali ila sio kwamba Kuna huduma bora inatolewa,,,,Kuna baadhi ya zahanati Kuna muuguzi tu na medical attendant tuu halafu kwakua watu wanapewa huduma utasema mambo yanaenda? Tukiacha kuzauriana kada ya afya itafika mbali maana unakuta Co anamdharau CA MD anamdharau Co specialist anamdharau MD super specialist anamdharau specialist,wengine wanamdharau surgeon wanasela MA surgeon akili zao zimawaza kukata tuuu! Tukiendelea hivi hatutofika mbali
 
Kwa zaidi ya 99% ya Zahanati hapa Tanzania hazina mfamasia, hazijawahi kuwa na mfamasia na wala hazihitaji mfamasia, zina Daktari na muuguzi na zinapiga kazi fresh. Hapo utasemaje?

Kwangu mimi Daktari na muuguzi ndio uti wa mgongo wa utoaji huduma za afya kwenye ngazi zote za vituo. Bila uwepo wa watu hao kwa hakika huduma za afya ni kama hakuna.
Nachelea kubisha usemacho ila narejea kwenye minajili ya mada tajwa .

Ikiwa tungelikuwa tunasema ni akina nani ni muhimu zaidi katika mambo ya afya nisingesita kukubali kuwa daktari na muuguzi ni uti wa mgongo wa mambo wa afya hasa kwenye nchi yetu .

Ila nilieleza katika hali ya mada ilivyoletwa .
 
Hivi kweli mtu anasomea Pharmacy 4 yrs, kuja kugawa dawa tu? Serikali rekebisheni hili.

Medical officer ana recommend dawa akiwa hana uzoefu wowote wala Elimu kuhusu dawa, hii sio sawa. Viongozi wetu wa juu Kuna sehemu mnakwama sana, waacheni wafamasia WAFANYIE kazi walichofundishwa darasani.
Bloggerboy ni yule wa Maswa yetu?
 
Back
Top Bottom