Hivi kweli mtu anasomea Pharmacy miaka 4 kuja kugawa dawa tu? Serikali rekebisheni hili

Hivi kweli mtu anasomea Pharmacy miaka 4 kuja kugawa dawa tu? Serikali rekebisheni hili

Nimekuwepo hospital kwa miaka kadhaa sasa kama medical student
Katika vitu nilivyoona na kushuhudia ni
1. Mgonjwa anafikia kwa daktari ambapo daktari humsikiliza na kuyafanyia kazi maelezo Yale na kuja na provisional na differential diagnosis ya shida inayomsumbua mgonjwa
2. Ili kupata uhakika wa kile kinachomsumbua mgonjwa, daktari huagiza vipimo mbali mbali ...hapa ndipo kazi ya lab technician na watu wa radiology huonekana (maana Kuna vipimo vingine ni vya mionzi kama x ray, CT scan, ...)
3. Baada ya majibu kurudi, daktari huyafananua na kupata uhakika wa shida ya mgonjwa na hapo humuandikia sawa (kama inahitajika)
4. Ni kazi sasa ya mfamasia kupokea maelekezo kutoka kwa daktari kwamba mgonjwa huyu anahiyaji dawa hii na Ile Ili kutibu shida yake
5. Kama mgonjwa atalazwa/kupumzishwa, basi nurse huchukua jukumu la kumhudumia akiwa wodini (kumpatia dawa, na kufanya follow-up ya maendeleo yake)
Kiufupi, Kila idara inamhitaji mwenzake, though inaonekana kama vle daktari yupo top na in charge of everything kwa kuwa yeye amesoma vitu vingi kuliko Hawa wengine
 
Upo sahihi.
Kitu nilichojifunza kwenye career life ni kuwa ni rahisi kuichuikulia poa field ya mwenzio kwa sababu ya mtazamo wa nje kama outsider, Ila ukipata bahati ya kuielewa au kuifanya hata kwa siku tu. Utabadili mtazamo wako
 
Kusema daktari Hana uzoefu wa dawa, inaleta ukakasi kidogo!
Amesoma magonjwa na dawa za Kila ugonjwa, management na hata jinsi ya kutoa dozi
Kwahyo uzoefu wake kwenye madawa ni mkubwa na usiotilia shaka
 
Hii ni obvious chai kabisa. Hakuna pharmacist anaweza kutibu zaidi ya Medical Officer, this is very wrong. Wanaweza wakawa na uelewa sahihi na wa kushahibiana kwenye prescription za dawa ila kwenye kutibu (taking hx, knowing what right investigation to do and formulating right diagnosis) Medical Officer knows and can do a lot compared to hao watu wa dawa. Na hii, hiko wazi wala haina uhitaji wa ubishi. Na get to know this, kisheria huyo mtu wako wa dawa haruhusiwi kufanya hayo anayoyafanya hapo kwenye maelezo yako.
Endelea kuwa na mawazo mgando ..

Wafamasia wengi wameamua kujishusha wenyewe ....
Lakini wanajua vitu vingi sana ..

Inategemea mfamasia kasomea wapi ...na ubobezi wake
 
Ila Bongo kuna Wafamasia wanawazidi madaktari.

Yupo mmoja namfahamu ana famasi yake na laboratory hapo na anatibu wagonjwa hasa wanawake na Watoto, hilo Nyomi lake si la kitoto, anapiga sana pesa.

Jamaa anajuwa Dawa nadhani ndio siri ya mafanikio yake.
Kama ni kijijini kwenye uhaba wa madaktar au matabibu basi kuna excuse anaweza fanya hivyo lakini kama ni mjini na anafanya hivyo basi ni kosa...vijijini uko kwenye uhaba wa madaktari/matabibu basi hadi wauguzi wanafanyakazi ya udaktari
 
Kusema daktari Hana uzoefu wa dawa, inaleta ukakasi kidogo!
Amesoma magonjwa na dawa za Kila ugonjwa, management na hata jinsi ya kutoa dozi
Kwahyo uzoefu wake kwenye madawa ni mkubwa na usiotilia shaka
Kumbuka mfamasia anasoma Magonjwa na dawa za ugonjwa ..
Hata management na dose pia ..

Wafamasia wanasomea utengenezaji wa dawa pia ...
 
Nimekuwepo hospital kwa miaka kadhaa sasa kama medical student
Katika vitu nilivyoona na kushuhudia ni
1. Mgonjwa anafikia kwa daktari ambapo daktari humsikiliza na kuyafanyia kazi maelezo Yale na kuja na provisional na differential diagnosis ya shida inayomsumbua mgonjwa
2. Ili kupata uhakika wa kile kinachomsumbua mgonjwa, daktari huagiza vipimo mbali mbali ...hapa ndipo kazi ya lab technician na watu wa radiology huonekana (maana Kuna vipimo vingine ni vya mionzi kama x ray, CT scan, ...)
3. Baada ya majibu kurudi, daktari huyafananua na kupata uhakika wa shida ya mgonjwa na hapo humuandikia sawa (kama inahitajika)
4. Ni kazi sasa ya mfamasia kupokea maelekezo kutoka kwa daktari kwamba mgonjwa huyu anahiyaji dawa hii na Ile Ili kutibu shida yake
5. Kama mgonjwa atalazwa/kupumzishwa, basi nurse huchukua jukumu la kumhudumia akiwa wodini (kumpatia dawa, na kufanya follow-up ya maendeleo yake)
Kiufupi, Kila idara inamhitaji mwenzake, though inaonekana kama vle daktari yupo top na in charge of everything kwa kuwa yeye amesoma vitu vingi kuliko Hawa wengine
Uzi ufungwe. Maelezo yako yanatosha.
 
Hivi kweli mtu anasomea Pharmacy 4 yrs, kuja kugawa dawa tu? Serikali rekebishenu hili

Medical officer ana recommend dawa hakiwa Hana uzoefu wowote Wala Elimu kuhusu dawa, hii sio sawa,
Viongozi wetu wa juu Kuna sehemu mnakwama sana, waacheni wafamasia WAFANYIE kazi walichofundishwa darasani.

Mods: rekebisheni heading hapo juu isomeke "rekebisheni"

Uzi umerun 3 hrs ,mods wanazetuana tu Maxence Melo

Hivi mbona threads nyingine hazichukui dk 1 wamefuta au kuunganisha Ila hii, kurekebisha title TU masaa 3?
Na hii ni kwa sababu nchi hii haina Viwanda vya madawa.

Kama kungekua na Viwanda vinavyo tengeneza dawa, au atleast hata ku repack dawa vya kutosha hawa jamaa wangeheshimika.

Any way. Tuendelee kupambana
 
Nimeeleza kwenye post za juu, kuna mama yangu Fulani tumezika kwa sababu ya Dawa zilikuwa zinashusha immunity badala ya kumtibu, sitaki kutaja jina la hospitali itakuwa si uungwana lakini hospitali kubwa tu

Mkuu hizi dawa zina Side effects na Adverse effects, kwahiyo ni kawaida hizo changamoto kutokea.
 
Hakuna daktari hakuna mfamasia , hizi ni kada zinazotegemeana sana .

Daktari kuna semister katika usomaji wake anakutana na kitu tunaita pharmacology lakini vivyo hivyo mfamasia kuna muhula ambao anasoma pia habari za prescription .

So kikawaida hawa watu inawapasa kutegemeana sana kuliko inavyodhaniwa ila shida inakuja pale tunapojaribu kuikuza kada ya udaktari kiasi cha kuwapuuza wafamasia .
 
Back
Top Bottom