Renegade
Platinum Member
- Mar 18, 2009
- 7,949
- 8,590
Sio lazima uajiriwe,Elimu ni maarifa unaweza kuyatumia unavyotaka, Lengo ni kumudu maisha ako.Nielewesheni nielewe wakuu wangu.
Sio lazima uajiriwe,Elimu ni maarifa unaweza kuyatumia unavyotaka, Lengo ni kumudu maisha ako.Nielewesheni nielewe wakuu wangu.
Tafsiri yangu ya elimu ni maarifa, ufahamu na akili ya kuweza kuyatawala mazingira.Nielewesheni nielewe wakuu wangu.
Kuoana tu tunabet iwe elimu😝Halafu unakuta wanakuja kuikanyagia betting
Here on earth, Everything is gambling
😅😅😅 Kufanyiwa research hapa ndipo tunapo bolongaKaka nakubaliana na wewe lkn ni mtazamo tu ndio unafanya haya yawe yalivyo! Hakuna nchi yenye mtaala unaosema muhitimu akajiajiri ila wanasaidia msomi kupata elimu kubwa kwa kumuonyesha resources tu then msomi mwenyewe ataona na atavutwa kujiajiri bila Profesa kumwambia lolote!
Philosophy ya elimu inataka msomi wa chuo kikuu kukesha na kushinda library kusoma na kujifunza extensively, mtaala ni scope ya mitihani tu lkn msomi anatakiwa kuwa na uwezo na ufahamu mpana mara elfu ya program anayofanya! Kwa kuwa sisi tunatazama huo mtaala na mabadiliko yake ndio maana msomi wa degree wa kibongo hana tofauti na fomfoo, period! Msomi wa kibongo anakuwa kakariri madude ya fani yake tu, akitolewa nje tu hana analojua hata sumni!
Wenzetu wa nchi zinazoendelea, anayefanya Masters ile disertation yake huwa ni project kabisa, yani anapograduate anaenda kuexecute na kuajiri, wengine wanaanza kuajiri wakiwa shule au wanadrop! Sisi tunafanyiwa hata research, nilishaona hapa JF watu wanatangaza wanachuo wanaotaka kufanyiwa proposals waende PM! Pathetic
Sio lazima uajiriwe,Elimu ni maarifa unaweza kuyatumia unavyotaka, Lengo ni kumudu maisha ako.
Lengo la elimu ni kupata maarifa ili uweze kutatua changamoto za dunia, ukishapata maarifa, unaweza ukaajiriwa au ukaajiajiri.
Ndio maana kuna madaktari walioajiriwa na waliojiajiri, kuna walimu walioajiriwa na wenye shule zao.
Kuajiriwa au kujiajiri, ni maamuzi yako, sio outcome ya elimu.
Mmenena vyema. Sasa nimeelewa.Tafsiri yangu ya elimu ni maarifa, ufahamu na akili ya kuweza kuyatawala mazingira.
Ukiona elimu haiwezi kukufanya utawale mazingira yanayo kuzunguka basi hiyo elimu ni scam..elimu inatakiwa iweze kutatua CHANGAMOTO ZAKO ZA KILA SIKU.
Mfano una degree fulani na hujapata ajira..inatakiwa hiyo elimu ikusaidie kuweza kutatua na kukupa maisha..
Hizi ndizo project niliwai kizifanya kipindii elimu / taaluma ilipo acha kunipa pesa..nilianzisha projects za kilimo cha mchicha hichi kilipipa sana kipato, kutengeneza maandazi nikayaita MAANDAZI CLASSIC..Nili uza sana sanaa.
NB. All in all, Elimu ni Yale maarifa ufahamu UNAO bakia nao KICHWANI baada ya ku graduate..hiyo ndio elimu..kama huwezi kumbuka chochote ulicho soma/ au ulicho soma hakikusaidii kutatua CHANGAMOTO ZAKO basi hiyo elimu ni SCAM.
Tena siku hizi kwenye ulimwengu wa Information Technology, kuna kitu mpaka kinaitwa "Infopreneurship" au uuzaji wa taarifa. Wewe ni mwalimu, tengeneza vipindi vyako vya tuition, piga promo, uzia wazazi subscription 3000Tzs kwa mwezi, ukipata wanafunzi 1,000... umetoboa! Huna darasa wala dinning hall la kujenga.Mmenena vyema. Sasa nimeelewa.
Ukisikia neno ajira, akili yako inakwambia nini?Inategemea na Lwngo la anayesoma...
Waalimu kibao walituaminisha kwamba tusome ili tuje tupate ajira au tusisome tukabebe mizigo, hii ni mentality mbaya sana kuwaambia vijana.
Sikuwahi kuona mwallimu akisema au akihamaisha watu wakimaliza kusoma wawaze kufanya biashara na kujitafuta nje ya Elimu.
Jambo la msingi ni kusoma kwa ajili ya mahitaji yako binafsi unataka nini au unataka kuwatumikia watu kwenye fani ipi hapo baadae.
Ukiwaza kwamba kusoma kutakufanya uwe tajiri hapo ni kosa, kusoma naona binafsi lengo ni kuwatumikia watu kwenye fani husika..
Suala la kupata hela inabidi lifanyike Nje ya taaluma.
Mfano unaweza kuamua kuwa mtaalamu wa saikolojia na malezi ukaamua kuwatumikia watu katika nyanja hiyo lakini pembeni unafanya mishe mishe zako za biashara mpunga unasoma..
Unaweza. Kuamua kuwa. daktari wa upasuaji lakini pembeni una Biashara zako zinaenda poa tu..
Sioni mahusiano ya kusoma na kupata hela ya maana kwenye kpzi nyingi ni kuwatumikia watu tu......
Ajira zimegawanyika sehemu mbili..Ukisikia neno ajira, akili yako inakwambia nini?
Tena siku hizi kwenye ulimwengu wa Information Technology, kuna kitu mpaka kinaitwa "Infopreneurship" au uuzaji wa taarifa. Wewe ni mwalimu, tengeneza vipindi vyako vya tuition, piga promo, uzia wazazi subscription 3000Tzs kwa mwezi, ukipata wanafunzi 1,000... umetoboa! Huna darasa wala dinning hall la kujenga.
Unanikumbusha mamaangu anavyopenda kuniambia kiupole mi mwenyewe hakuna aliyenipa mwanangu unatafuta nwenyewe nasikiaga kulia🤭Mimi binafsi,
Wazazi wangu walinipeleka shule nisome ili Niajiliwe.
Na walikua wananisisitizia kabisa, Hatuna cha kukuachia Mwanangu, Urithi wako ni Elimu 😀🙌
Mungu sio athumani, Wala Abduli Ka elimu kangu kananilipia Kodi
Kuelimika, kuongeza ufahamu na maarifa ili kuweza kuishi mazingira yote na ukiweza uyabidili kuwa boraNielewesheni nielewe wakuu wangu.
Lengo la wagonjwa kutakiwa kwenda hospital kutibiwa na madaktari au kupewa dawa ni kupona ila sio wagonjwa wote wanaoenda kutibiwa hospital au wanaopewa dawa huwa wanapona, wengine huwa wanakufa kabisa, sasa ukiuumwa uamuzi ni wako kusuka au konyoa.Hiki ndo kilichofanya niulize swali. Wazazi waliambia nisome Ili niajiriwe nipate pesa. Nikajiuliza iwapo iwapo lengo la kusoma ni kupata pesa, na wenye pesa wote wamesoma?
Inategemea na hali ya uchumi wa familia.Nielewesheni nielewe wakuu wangu.
Wapo masikini wengi tu waliotoka kupitia Elimu.Inategemea na hali ya uchumi wa familia.
Ikiwa mna mtaji kwenye familia kusoma kwako kutasaidia kuundeleza, ikiwa familia ni kapuku utakuwa bidhaa na utapewa na bei (mshahara) kwa kumfaidisha mwenye mtaji.
Unanikumbusha mamaangu anavyopenda kuniambia kiupole mi mwenyewe hakuna aliyenipa mwanangu unatafuta nwenyewe nasikiaga kulia🤭