Hivi lengo kuu la kusoma (elimu) ni kupata kuajiriwa?

Lengo la elimu ni kupata maarifa ili uweze kutatua changamoto za dunia, ukishapata maarifa, unaweza ukaajiriwa au ukaajiajiri.

Ndio maana kuna madaktari walioajiriwa na waliojiajiri, kuna walimu walioajiriwa na wenye shule zao.

Kuajiriwa au kujiajiri, ni maamuzi yako, sio outcome ya elimu.
 
Nielewesheni nielewe wakuu wangu.
Tafsiri yangu ya elimu ni maarifa, ufahamu na akili ya kuweza kuyatawala mazingira.

Ukiona elimu haiwezi kukufanya utawale mazingira yanayo kuzunguka basi hiyo elimu ni scam..elimu inatakiwa iweze kutatua CHANGAMOTO ZAKO ZA KILA SIKU.

Mfano una degree fulani na hujapata ajira..inatakiwa hiyo elimu ikusaidie kuweza kutatua na kukupa maisha..

Hizi ndizo project niliwai kizifanya kipindii elimu / taaluma ilipo acha kunipa pesa..nilianzisha projects za kilimo cha mchicha hichi kilipipa sana kipato, kutengeneza maandazi nikayaita MAANDAZI CLASSIC..Nili uza sana sanaa.

NB. All in all, Elimu ni Yale maarifa ufahamu UNAO bakia nao KICHWANI baada ya ku graduate..hiyo ndio elimu..kama huwezi kumbuka chochote ulicho soma/ au ulicho soma hakikusaidii kutatua CHANGAMOTO ZAKO basi hiyo elimu ni SCAM.
 
😅😅😅 Kufanyiwa research hapa ndipo tunapo bolonga
Yan mtu anatumia miaka 25 kusoma kiima na kiarifu
Mara uchambuzi wa sentence Yan mambo ya hovyo yasiyokuwa na uhusiano na maisha arf hyu mtu ndo tunategemea alete mabadiliko katika jamii
 
Sio lazima uajiriwe,Elimu ni maarifa unaweza kuyatumia unavyotaka, Lengo ni kumudu maisha ako.
Mmenena vyema. Sasa nimeelewa.
 
Mmenena vyema. Sasa nimeelewa.
Tena siku hizi kwenye ulimwengu wa Information Technology, kuna kitu mpaka kinaitwa "Infopreneurship" au uuzaji wa taarifa. Wewe ni mwalimu, tengeneza vipindi vyako vya tuition, piga promo, uzia wazazi subscription 3000Tzs kwa mwezi, ukipata wanafunzi 1,000... umetoboa! Huna darasa wala dinning hall la kujenga.
 
Ukisikia neno ajira, akili yako inakwambia nini?
 
Mimi binafsi,

Wazazi wangu walinipeleka shule nisome ili Niajiliwe.

Na walikua wananisisitizia kabisa, Hatuna cha kukuachia Mwanangu, Urithi wako ni Elimu 😀🙌

Mungu sio athumani, Wala Abduli Ka elimu kangu kananilipia Kodi
 

Bongo hii hii au Nchi gani?
 
Mimi binafsi,

Wazazi wangu walinipeleka shule nisome ili Niajiliwe.

Na walikua wananisisitizia kabisa, Hatuna cha kukuachia Mwanangu, Urithi wako ni Elimu 😀🙌

Mungu sio athumani, Wala Abduli Ka elimu kangu kananilipia Kodi
Unanikumbusha mamaangu anavyopenda kuniambia kiupole mi mwenyewe hakuna aliyenipa mwanangu unatafuta nwenyewe nasikiaga kulia🤭
 
Hiki ndo kilichofanya niulize swali. Wazazi waliambia nisome Ili niajiriwe nipate pesa. Nikajiuliza iwapo iwapo lengo la kusoma ni kupata pesa, na wenye pesa wote wamesoma?
Lengo la wagonjwa kutakiwa kwenda hospital kutibiwa na madaktari au kupewa dawa ni kupona ila sio wagonjwa wote wanaoenda kutibiwa hospital au wanaopewa dawa huwa wanapona, wengine huwa wanakufa kabisa, sasa ukiuumwa uamuzi ni wako kusuka au konyoa.
 
Inategemea na hali ya uchumi wa familia.
Ikiwa mna mtaji kwenye familia kusoma kwako kutasaidia kuundeleza, ikiwa familia ni kapuku utakuwa bidhaa na utapewa na bei (mshahara) kwa kumfaidisha mwenye mtaji.
Wapo masikini wengi tu waliotoka kupitia Elimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…