Hivi Leo bado Kuna kile kizazi mpaka sasa mama yupo, bibi yupo na mama wa bibi pia yupo?

Hivi Leo bado Kuna kile kizazi mpaka sasa mama yupo, bibi yupo na mama wa bibi pia yupo?

Wapo, hujawahi kuhudhuria mazishi ya vikongwe wenye vizazi vinne? Wanaweka mashada mpaka vilembwekwezi, unakuta kikongwe ana miaka mia na ushee kazaliwa zama za mjurumani miaka ya 1800. Kuna watu wamejaliwa kuishi umri mrefu mjuba
 
Dah😭😭
Nadhani kwa sasa watu watakuwa wanakata moto mapema sana.
Vizazi vitatu-vinne vinapotea!!
 
Kama mtu anazaa akiwa na miaka 15, huyo mtu anaweza kuona mpaka vilembwezi, kizazi chake cha nne
 
Nimebahatika kuona moja Kilombero nilipokwenda kununua mchele kwaajili ya biashara.

Mungu amewasaidia bado wana nguvu hata za kwenda shamba pamoja na Uzee wao

Kwa kizazi cha sasa chenye Matumizi makubwa ya Pombe Kali/shisha/ngono zembe za kuruka ukuta/mwendo Kasi barabarani, sio rahisi kufikia ule umri 🙌
 
Mimi ni kilembwekeze kwa bibi yangu, huko bush kila siku wanandugu wanafanya maombi afe mizimu imegoma, anadai walimpakia juu ya mbuzi utoto, hivyo hatakufa hadi kizazi cha elfu 1 cha huyo mbuzi kipite, wazee wa zamani bwana ni shida sana aiseee!
 
Wapo kuna shem mmoja anao bibi zake tena na ndg wa bibi zake ambao ni dada wa bibi yake huyo wapo, na hapo wanavyo vitukuu vikubwa tu vyenye 18+ bila shaka hata vilembwe wanavyo
 
Back
Top Bottom