Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Nimefika Dar es salaam nikafanikiwa kupanda magari ya mwendokasi nikajiuliza viongozi wenye dhamana wameisha DSM? Mabasi yamechoka, yanajaza abiria hadi milango haifungi, yapo machache na hakuna msimamizi serious unayemwona mwenye lengo la kuyatunza yadumu.
Kwa namna mabasi haya yanavyoendeshwa na kwakuzingatia utaratibu mzima wa ukataji tiketi, ukaguzi wa tiketi na usimamizi wa ulinzi wa abiria niseme fedha za walipa Kodi zinatumika vibaya.
Watu wetu weusi hao hao wanamiliki mabasi ya mikoani na siku zote huduma unaona zinaboreshwa; wamepewa mradi wa serikali hakuna mwenye uchungu nao hadi aletwe Mzungu aje atusaidie kukata tiketi, kupakia abiria, kulinda NK......Nani katuloga?
Kwa huduma hizi mbovu bado unasikia IPO mamlaka ya serikali imepandisha nauli.....unasikia MTU anasema tumepandisha nauli kumvutia mwekezaji huku wananchi wakiteseka.
Kampuni hata chenchi zakuwarejeshea wateja haina kweli? Kwamba mradi wa serikali watu wanaamua kutotafuta chenchi Kwa lengo lakuwadhulumu wananchi kidogo walichonacho! Kwamba abiria asiye na pesa kamili Hana Haki, viongozi mpo wapi? Au mnasubiri waziri mkuu au Mhe. Rais atembelee huu mradi wakaulize kwanini wananchi wanalazimishwa kuja na chenchi kamili? Wakaulize kwanini watu wanajazwa Hadi kuyafanya magari kuaribika mapema?
Watu tunatafuta kazi hatuna then wapo watu wanaunderperfom mnawafumbia macho kisa ajira za undugu...poa