Hivi mabasi ya mwendokasi yana mwenyewe? Au yanajifia kama daladala za UDA?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Nimefika Dar es salaam nikafanikiwa kupanda magari ya mwendokasi nikajiuliza viongozi wenye dhamana wameisha DSM? Mabasi yamechoka, yanajaza abiria hadi milango haifungi, yapo machache na hakuna msimamizi serious unayemwona mwenye lengo la kuyatunza yadumu.

Kwa namna mabasi haya yanavyoendeshwa na kwakuzingatia utaratibu mzima wa ukataji tiketi, ukaguzi wa tiketi na usimamizi wa ulinzi wa abiria niseme fedha za walipa Kodi zinatumika vibaya.

Watu wetu weusi hao hao wanamiliki mabasi ya mikoani na siku zote huduma unaona zinaboreshwa; wamepewa mradi wa serikali hakuna mwenye uchungu nao hadi aletwe Mzungu aje atusaidie kukata tiketi, kupakia abiria, kulinda NK......Nani katuloga?

Kwa huduma hizi mbovu bado unasikia IPO mamlaka ya serikali imepandisha nauli.....unasikia MTU anasema tumepandisha nauli kumvutia mwekezaji huku wananchi wakiteseka.

Kampuni hata chenchi zakuwarejeshea wateja haina kweli? Kwamba mradi wa serikali watu wanaamua kutotafuta chenchi Kwa lengo lakuwadhulumu wananchi kidogo walichonacho! Kwamba abiria asiye na pesa kamili Hana Haki, viongozi mpo wapi? Au mnasubiri waziri mkuu au Mhe. Rais atembelee huu mradi wakaulize kwanini wananchi wanalazimishwa kuja na chenchi kamili? Wakaulize kwanini watu wanajazwa Hadi kuyafanya magari kuaribika mapema?

Watu tunatafuta kazi hatuna then wapo watu wanaunderperfom mnawafumbia macho kisa ajira za undugu...poa
 
Tanzania tunaonyesha kushindwa kuendesha miradi ya public transportation, fuatilia UDA, Christiania, First Choice na wengine.
 
Alafu kuna pimbi mmoja unakuta anampondea late Hayati Dr. JJPM... yule mwamba dah🙌 Bongo inatakiwa ipate kichwa kama kile, Huwezi sema kiongozi ana mabavu wakati ukipewa mabae hana mabavu unafanya uzembe ku-cost taifa, Unataka uchekewe?
 
Mabasi yana hadi kunguni
 
Kila siku mnakuja mitandaoni kulialia eti *viingozi mko wapi?"
Nani kiongozi wako
Kama huwezi kujisimamia unalia nini ?
Tulia, tulieni
 
Kuna boya mmoja somewhere kakaa stand by anabuni mradi wake hapo anachora michoro ya mitumba atakayoenda kutubebea na kutuambia ni mipya, magari yakibuma tu anaingia ubia na Serikali anawauzia mitumba ya mwendokasi ndio kilichobakia kufa kufanana,
 
Alafu kuna pimbi mmoja unakuta anampondea late Hayati Dr. JJPM... yule mwamba dah🙌 Bongo inatakiwa ipate kichwa kama kile, Huwezi sema kiongozi ana mabavu wakati ukipewa mabae hana mabavu unafanya uzembe ku-cost taifa, Unataka uchekewe?
Kile kichwa kingekuwa kinakubali kushauriwa kingekuwa hai hadi leo.
Alikuwa muoga kukosolewa kiasi cha kupoteza wakosoaji wake kina ben saanane ETC.

Apumzike kwa amani.
 
Uzuri wake kupanda hayo mabasi sio lazima.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
Aisee nasikia ukiingia mule kituoni unalipia 650 unaweza kwenda popote unapotaka unapanda gari lolote la mwendokasi kwa hio hio 650 Ila sharti tu usitoke ndani ya kituo cha mwendokasi, ndio maana watu hawaishi wanazurula tu humo humo vituoni kwa 650
 
Lile la kushindilia watu kwenye bus kama gunia la viazi,
Ndy nachoka kabisa na mwendokasi.
 
Mali ya umma watu hawanaga uchungu nayo

Ova
Rais mbovu ndiyo sababu serikali yote imegeuka genge la wahuni na walevi
mabasi yanashindwa hata kusafishwa vumbi na tope BRT inaongozwa na wapumbavu bila shaka yoyote.
 
Ile milango bro...gari aitembei hata ikibidi uminye kitambi kwa muda ili mlango ufunge safari ianze.
Watu kubanana sana milangoni kunaharibu milango Kuna wakati milango Ina jam haifunguki inabidi bus liende gereji na kupunguza idadi ya mabasi kwenye route. Nchi hii Kuna menejimenti nyingi zina watu wajinga
 
Back
Top Bottom