Hivi makomando wa JWTZ wako competent kweli kulinganisha na wenzao wa nchi nyingine?

Polisi kingai anawageuza na kuwagalagaza kila apendapo.
Hii miaka 60 kwao ni michache labda sherehe ya sitini mingine watatoka kivungine
 
Tatizo lako unakuja na majibu yako kwenye yangu...
Nimekwambia nina facts... mfano kwenye missions walizoenda ni mara ngapi tunasikia wamezidiwa nguvu??

Nawaheshimu sana wana JWTZ wetu lakini tusiwapumbaze wakajiona wapo vizuri...
Una facts yes, but facts lazima ziwe supported withe evidence.
Okay weka hizo facts zako? Mission walizoenda ikiwemo outvome ya hizo mission?
 
Wangetunzwa vizuri unadhani wangekuwa mateja serikali yako ya ccm haiwathamini watumishi wake
 
Afande Goodluck Minja kawapigisha push-up tu akina Ling'wenya pale Central wanalialia kuteswa![emoji16].

Je wangepitia doso kwa wale jamaa wa Guantanamo Bay?
Ukimpa commando push up ni sawa na kumpa baunsa avunje biscuit kwao hilo sio zoezi.
 
Kubeba hivyo ni show tu ila inasaidia vitani kwani wanaweza kubeba majeruhi wenzao kwa uzoefu ama kubeba silaha nzito, hata hao SEAL TEAM huwa wanafanya mazoezi ya kubeba mawe mazito kwenye mabag hayo na kukimbia mwendo mrefu
Wanaziitaga "rock sack" unakimbia nazo mlimani
 
[emoji44][emoji44][emoji44][emoji44][emoji44] hebu angalia BUDS class then uangalie intro yao,,, ukishaangalia rudi tena urekebishe andiko lako
 
Mtoa mada Utoto unakusumbua, vitu vingine hupaswi hata kuuliza watu unajiuliza mwenyewe na kukaa kimya.

Nchi zilizoendelea zimewekeza kwenye tools, kwakuwa sisi hatuna tools za kutosha tunawekeza kwenye man power.

Mwanajeshi ni binadamu pia anapokuwa vitani anahitaji mahitaji muhimu, nchi zilizoendelea wanavifaa vya kutosha na kisasa kwajili ya kifikisha mahitaji kwa askari wake.

Kwakuwa sisi hatujafika huko inabidi vijana wetu wawe na uwezo wa kujibebea mahitaji muhimu wao wenyewe.
 
Una facts yes, but facts lazima ziwe supported withe evidence.
Okay weka hizo facts zako? Mission walizoenda ikiwemo outvome ya hizo mission?
2017: 14 waliuawa DRC

2013: 7 waliuawa Sudan Majina saba ya askari walio uwawa Sudan

Anza na hizo hapo...
Alafu inasemwa kwamba JWTZ hawapendi sana kujihusisha na missions za kimataifa. Juzi hapo tu Cabo Delgado, Mozambique tukashindwa kutimiza majukumu yetu tukamuachia Rwanda.
 
Umeongea moja nzuri sana kiongozi
 
"the so called commandos wa JWTZ" hii ni sentensi iliyojaa dharau kubwa kwa jeshi na kukosa uzalendo. Mtu kama wewe unastahili uwe jela hata miezi sita ili ukitoka uwe na nidhamu.
 
Hawa si walikua wanalia juzi tu wanekamatwa na polisi ?

Vuta picha labda wangekamatwa na wajeda wa russia ingekuaje
Siyo hawa waliokuwa uwanjani wale wa Gaidi Mbowe ni Unfit ndiyo maana walifukuzwa JW kwa sababu ya uvutaji madawa ya kulevya. Wameathirika na madawa ya kulevya hao usiwalinganisha na hawa waliotimamu kwa kazi.
 
Na wewe ficha ujinga wako...SEAL ni nini kama sio comando? Kwani makomandoo duniani kote si wanaitwa special forces?!
SEAL ni kokosi maalum
wanaofanya mafunzo ya kupigana kutokea baharin SEA angani AIR na àrdhini LAND (SEAL) ndio maana wanaitwa hawa jamaa wana kuwaga na mission maalum vitan mfano kuokoa mateka, kumtungua /kumkamata mtu wanae mlenga ,msaka hawa jamaa sio marine troops.
Hata Tz tunao elite forces lkn sio commandos
 
Una uhakika na unachoongea
 
We mleta uzi usifananishe jeshi lenu la Burundi na jwtz,, ukitaka kujua uwezo wao kiundani basi yatimbe uone,,, pumbavu kabisa wewe,, hiyo mizigo wangebeba hao unaowasifia ungekuja na hoja hapa,, wenzenu majeshi yao askari wao wana uwezo wa kuhimili kubeba mizigo mikubwa kwenye uwanja wa mapambano,,
 
Lakini mbona hata hawa makomandoo wa kwetu wanaenda nje kwenye training regularly! Kilichokuwa kinaonyeshwa uwanja wa taifa ni show off nasi uhalisia wa kwenye battle field.

Hao seal team 6 unaowasifia wako simple wamekuwa deployed hapo na armed vehicle ( gari lisilopitisha risasi) halafu kwa juu angani wanasaidiwa na drone inayo locate alipo adui na kushambulia pia,unataka wabebe mabegi ya nini yenye vyakula na vimiminika wakati badae wanakuja kubebwa na gari au helicopter kurudishwa kambini kucheza pool,kulewa nakucheza games.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…