Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Inawezekana hii ndo haswa sababu itayofanya hii nchi kuendelea kuwa maskini milele, inawezekana pia ni jambo la kimkakati wa kisiasa kuzidi kuwatawala watu kadri upendavyo.
Kwa sababu kwa lugha ya picha, kama nchi ni maskini na raia wengi ni maskini, na wengi wao hawajakomboka kifikra, inakuwa ni rahisi sana kuwaaminisha hawa watu kwamba mwanasiasa bora ni yule tu anayetusaidia 'vitu' - Chakula, fedha kidogo, nguo, viatu....
Misaada ya vitu kwa maskini, haina historia ya kubadilisha maisha ya masikini wa nchi hii, sana sana hii misaada wanaopewa maskini, naweza kusema ndio imekuwa ikichangia umasikini wa hawa watu. Inawaletea kudumaa kiakili na kuamini hawana haja ya kutafuta mali zao, ingali wanaweza kuomba kwa wengine na kupata.
Ni kwanini hawa viongozi wasitumie resources walizonazo kutengeneza mazingira ya hawa masikini kuweza kutengeneza utajiri?
Je kiongozi mwenye fikra zilizolenga kuwapa masikini samaki badala ya kuwafundisha namna ya kuvua, je ni kiongozi kweli mwenye uwezo wa kuleta maendeleo ya kweli?
Haya maswali ukitafakari uyajibu, utakuja kwenye conclusion kwamba 'VIONGOZI WA TANZANIA WAMEISHIWA MBINU ZA KUONDOA UMASIKINI'
Huwezi kuondoa umaskini kwa kumpa mtu milioni tano, halafu unamuacha akibakia na akili zile zile zilizomfanya yeye akawa maskini (ni sawa sawa uchukue 1,000 uzidishe na 0 utegemee kupata 10,000) never....