Hivi mbona watoto wa siku hizi hawachezi michezo tuliyocheza zamani kama kombolela?

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Wadau hili ni kuwa michezo tuliyocheza zamani imepitwa na wakati au kama vile ukuti, kombolela, rede, kibaba na kimama, magari ya udongo, kuendesha matairi au kufunga kamba na kuendesha kama basi unapakia abiria. Hii michezo sioni kwa watoto wetu wa sasa.

Je, imepitwa na wakati?
 
Sasa mtoto anaenda skul 3yrs atacheza saa ngapi hyo michezo Zaid ya kwenda kugeuzana huko mashulen na vitoto vye nzao ndio michezo wanayoweza
 
Kwa huu uandishi wako sidhani kama hata hiyo michezo ulicheza
 

Yaani kwa Elimu yako hiyo na Kujiita kote Great Thinker Ndugu umeshindwa tu Kuelewa kuwa Nyakati zetu zile tulikuwa hatuko so exposed na Mambo mengi ya Kimaendeleo ( ya Kidunia ) kutokana na Mapinduzi ya Viwanda duniani yaliyokaribisha hata Ubunifu zaidi na Teknolojia Kuongezeka hivyo hivi sasa Watoto wetu Fikra zao zimehamishiwa kutoka zile zetu na Wao wamejikita zaidi katika Michezo ya Kisasa kama ya Video Game na mengineyo ambayo haiwalazimishi wao Kuzurula hovyo Mitaani pamoja na kuwa na tabia zetu zile za Uswahili Uswahili. Kila zama za Kizazi kinakuja na Mabadiliko yake ya Kimfumo katika Jamii iliyopo.
 
Coders tunao ila ni wachache wenye competency ya maana wengi wamemeza tu wanahangaika mitaani........acha watu tu wasome wanachopenda.........kusoma kitu isiwe trend kama fashion flani
Nini maana ya kusoma unachopenda.
 
Ni kweli mambo yanabadilika lakini kuna baadhi ya michezo enzi hizo ilikuwa inawasaidia watoto hasa kwenye ubunifu na kutumia akili.

Nakumbuka tulikuwa tukiunda magari kwa kutumia vipande vya mbao na kandambili kama matairi bila kusahau tunaweka mpaka steering wheel kwa kutumia kamba fulani hivi, halafu tunatumia makoa kama springs, huu ulikuwa ubunifu wa hali ya juu.

Kama usemavyo zama zimebadilika, lakini nadhani kwa zama hizi na hawa watoto wetu suala la ubunifu litakuwepo kwa kiwango kidogo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…