Ni kweli mambo yanabadilika lakini kuna baadhi ya michezo enzi hizo ilikuwa inawasaidia watoto hasa kwenye ubunifu na kutumia akili.
Nakumbuka tulikuwa tukiunda magari kwa kutumia vipande vya mbao na kandambili kama matairi bila kusahau tunaweka mpaka steering wheel kwa kutumia kamba fulani hivi, halafu tunatumia makoa kama springs, huu ulikuwa ubunifu wa hali ya juu.
Kama usemavyo zama zimebadilika, lakini nadhani kwa zama hizi na hawa watoto wetu suala la ubunifu litakuwepo kwa kiwango kidogo sana.