Naby Keita
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 12,893
- 20,089
Kula mbakishie baba........ huu mchezo kama ulikua na afya mbovu ilibidi ukae pembeni tu........watu walikua wanakula ngumi hadi mtu anacheua damu halafu hio ngumi kakutandika mtoto mwenzioMICHEZO YA VIDEO GAMES unayoita ya kisasa haimfanyi mtoto kuwa na nguvu za kiakili na kimwili.Toto linakuwa dormant na ujasiri na nguvu zero
Mfano michezo ya kiswahili kuna ile ya watoto kuruka kamba.Watoto wawili wanashika kamba wanaizungusha mmoja anaruka katikati inajenga misuli ya mikono na miguu kwa mrukaji na matumizi ya akili kwa pamoja na kujenga team work na watoto wenzie.
Na akishindwa kamba ikimpiga miguuni anatolewa nje analetwa mwingine yule anayeweza sana anasifiwa kwa uwezo wake na wenzie na kumjengea sprit ya kupenda kushinda kwenye maisha.Hiyo mitoto micheza video games nguvu haina kabisa za mikononi wala miguuni wako kama kuku wa mdondo
Kuna michezo kama ukuti ukuti wa nazi wa nazi watoto wanazunguka kijeshi kwa spidi ya mwewe utachoka mwenyewe amri toka kwa kamanda mwimbishaji jeshi litoke nyuma akitoa amri watoto wanatua chini kama ndege ya boeing inatua uwanja wa kimataifa kwa spidi.WAtoto mtaani wanajuana wanajenga urafiki ambao haukatiki maisha yao yote sababu walicheza pamoja .Wa video games rafiki yake robot aliyeko kwenye computer game hapati muda wa kutengeneza marafiki sababu ratiba yake iko tight .Asubuhi shule mpaka jioni hana muda wa ku make friends .Akirudi ana homework ,akimaliza homework anaingia kucheza video games!!! Huyo hatengenezwi kuwa binadamu unatengeneza li robot!!