Nadhani Africans ndio watu pekee tunaoongoza kusifia mambo ya zamani hata kama yalikuwa na ujinga wa kiwango cha kusikitisha.
tukianza na kombolela- huu mchezo umesababisha watoto kuanza ngono mapema na kuwaharibu akili zao tangu utotoni, fikiria kitoto cha miaka 11 au 7 kinafanya huo ujinga.
Alafu leo nimwache mwanangu acheze kombolela seriously?.
Michezo ya watoto ya kiswahili ni gender based!! wasichana wanacheza peke yao na wavulana peke yao.Hakujawahi tokea michezo ya mchanganyiko ya watoto wa kiume na wa kike ya kiasili.Ya kizungu ndio ina shida ya hiyo mitatizo ya ngono
Kwa taarifa nchi zote zinazothamini mambo ya zamani ndizo ziko developed.Mfano uingereza bado wana ufalme sisi uchifu tuliua, Japan pia,Norway,Sweden,DENMARK nk
Ukienda china wengi hawamezi panadol wanakunywa chinese traditional medicine dawa zao za zamani ni ziko juu hasa
Mwaka 1949 CHINA KULIFANYIKA kitu kinaitwa cultural revolution ambako mao tse tung alifunga mipaka yote ya china akasema marufuku ku import kitu chochote toka nje ya nchi na marufuku ku export chochote kiwe mila na destuiri dini nk akafunga uchumi (closed economy) Wakasema mzee tutaishije akasema bunini vya kwenu.Ndipo wachina waliopanza ugunduzi wa hali ya juu kwenye kila eneo ili watimize mahitaji ya wachina sasa hivi china soko limefurika wamekuwa giants wa exports hakuna nchi afrika hata tanzania hakuna nyumba isiyo na kitu cha kichina iwe cha ujenzi,jikoni ,stationary nk
Ona wahindi wanavyoenzi vitu vya zamani vya kwao wana hadi vyuo vikuu vya traditional medicine wanatoa hadi PHD wana maandishi yao ya zamani wanafundisha elimu kwa kutumia lugha yao na maandishi yao toka chekechea hadi phd
WACHINA,WAJAPAN,WAHINDI NA WAARABU wana maandishi ya kwao yasiyo haya ya mzungu ya a,b,c,d nk na lugha yao vitu vya zamani na wanavitumia kufundishia kuanzia chekechea hadi PHD kwa lugha na maandishi yao
Sisi waafrika ni homeless ni breed isiyo na chake cha zamani kazi kudakia dakia tu vya wengine kama mabwege.Hata michezo tu mtu una import video games si ubwege huo.Huwezi buni hata mchezo wako au ukafufua wako wa kale .Hata kucheza tu unataka kucheza kizungu!!! very funny!!
Sisi waafrika ndio peke yetu duniani ambao vyetu vya zamani tuna vizomea!!! tunachekelea mi video game ya wazungu na kuzomea vyetu.Hivi unaona raha gani hadi mtoto michezo a import toka nje ya nchi!!!