Nikiwa Kama mwanachama kindaki ndaki wa Yanga Sc ninayelipa ada ya uanachama kila mwaka ninayohaki ya kujua (kujuzwa) /kuuliza/kuhoji mapato ya timu pale ninapokua sijui.
Hili la Mkataba wa "WHIZMO" limekuja kitofauti nimeona watu wanapaa juu juu uzinduzi wa jezi, @NALIANGWENA nilisubiri maelezo kutoka kwa viongozi kuwa mkataba wa "WHIZMO" umeingiza kiasi gani lakini sikuona Hilo.
Na Mimi mwanayanga lialia nahitaji kujua/kutambua mkataba huu unaingiza shilingi ngapi kwenye timu yangu (Yanga Sc) ?? Kama tulivyowekwa wazi kwenye mkataba wa ZIRA, ZIPA kule zenji na mikataba mengineyo iliyo pita Kama "HAER"
NB: Kama hujui kitu Kama Mimi ni Bora kukaa kimya lakini siyo kuja kwenye Uzi kuporomosha matusi na lugha za kejeli Kama vile kwenu hakuna wakubwa.
Nawasilisha hoja.
View attachment 2841978