Hivi mkataba uliosainiwa na Yanga sc "WHIZMO" ni mkataba unayoiingizia timu shilingi ngapi?

Kwanza naomba nijue WHIZMO ni kitu gani? Kuuliza si ujinga
PITIA HAPA

Nikiwa Kama mwanachama kindaki ndaki wa Yanga Sc ninayelipa ada ya uanachama kila mwaka ninayohaki ya kujua (kujuzwa) /kuuliza/kuhoji mapato ya timu pale ninapokua sijui.

Hili la Mkataba wa "WHIZMO" limekuja kitofauti nimeona watu wanapaa juu juu uzinduzi wa jezi, @NALIANGWENA nilisubiri maelezo kutoka kwa viongozi kuwa mkataba wa "WHIZMO" umeingiza kiasi gani lakini sikuona Hilo.

Na Mimi mwanayanga lialia nahitaji kujua/kutambua mkataba huu unaingiza shilingi ngapi kwenye timu yangu (Yanga Sc) ?? Kama tulivyowekwa wazi kwenye mkataba wa ZIRA, ZIPA kule zenji na mikataba mengineyo iliyo pita Kama "HAER"

NB: Kama hujui kitu Kama Mimi ni Bora kukaa kimya lakini siyo kuja kwenye Uzi kuporomosha matusi na lugha za kejeli Kama vile kwenu hakuna wakubwa.

Nawasilisha hoja.

View attachment 2841978
Genta hatukuelewi, uko Simba au Yanga?
 
Ila hizi timu zetu mbili ni pasua kichwa kwenye kuficha mikataba,wakati mwingine nahisi hata figure wanazoandika kwenye mikataba siyo halisi wanapunguza ila wanapiga parefu
 
TENA KIPINDI KAMA HIKI MASHABIKI WAMEFURAHI TIMU ZOTE ZIMEFUZU WATU HAWAWEZI KUHOJI MAMBO YA MKATABA.
 
Kama Mo, imagine mbet kifuani wamesema wanalipa bilioni 7, Mo ana matangazo manne kwenye jezi basi kwa vile siyo kifuani angelipa hata bil 3 kwa kila tangazo ingekuwa bil 12,ila analipa mil 300 ambayo hata haijulikani kama ni ukweli,hela zote za kuingia robo mara nne hakuna mchanganuo,acha kufuzu hizi hatua za chini,hela za AFL bil 5 wamepata na bado anakuambia anapata hasara, Mo kawa tajiri wa 12 baada ya kuingia Simba,je simba haijachangia utajiri wake?
 
NGOJA WAJE WENYE TIMU YAO WATAKUTUKANA NAHIVI WAMESHINDA GOLI 6
 
Back
Top Bottom