Hivi mkataba uliosainiwa na Yanga sc "WHIZMO" ni mkataba unayoiingizia timu shilingi ngapi?

Hivi mkataba uliosainiwa na Yanga sc "WHIZMO" ni mkataba unayoiingizia timu shilingi ngapi?

Nikiwa Kama mwanachama kindaki ndaki wa Yanga Sc ninayelipa ada ya uanachama kila mwaka ninayohaki ya kujua (kujuzwa) /kuuliza/kuhoji mapato ya timu pale ninapokua sijui.

Hili la Mkataba wa "WHIZMO" limekuja kitofauti nimeona watu wanapaa juu juu uzinduzi wa jezi, @NALIANGWENA nilisubiri maelezo kutoka kwa viongozi kuwa mkataba wa "WHIZMO" umeingiza kiasi gani lakini sikuona Hilo.

Na Mimi mwanayanga lialia nahitaji kujua/kutambua mkataba huu unaingiza shilingi ngapi kwenye timu yangu (Yanga Sc) ?? Kama tulivyowekwa wazi kwenye mkataba wa ZIRA, ZIPA kule zenji na mikataba mengineyo iliyo pita Kama "HAER"

NB: Kama hujui kitu Kama Mimi ni Bora kukaa kimya lakini siyo kuja kwenye Uzi kuporomosha matusi na lugha za kejeli Kama vile kwenu hakuna wakubwa.

Nawasilisha hoja.

View attachment 2841978
Kama wewe ni mwanachama kwa nini usiende kuuliza kwenye ofisi za Yanga. Na je wakikuambia itakusaidia nini au utafanya nini.
 
Back
Top Bottom